Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Soma na hii taarifa ya November 2023Inasemekana kuwa mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Simanjiro.
Amekimbizwa hospitali katika juhudi za kupambania maisha yake.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
Hakuna alie salama..!!
---
Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambulia gari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.
Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.
View attachment 2948550
"Katika hali ya kuishiwa na akili za uongozi, Ole Sendeka ameendelea kusababisha vurugu na kushawishi wananchi kuvamia mashamba ya wawekezaji halali. Baada ya vikao anavyodai vya siri na baadhi ya wanachi ,Jana tarehe 11/12/2023 na leo 12/12/2023 wananchi wa Naberera walienda kuvamia shamba la Rotiana Social Investment Ltd Ole Sendeka akiwa nyuma yao.
Bila aibu na hali akijua mashamba hayo yanamilikiwa kihalali na yanaendeshwa na Kampuni ya Rotiana Ole Sendeka amesema uongo kuwa mashamba hayo hayana mmiliki na kuwambia wananchi wayachukue kwa nguvu.
Ikumbukwe kuwa Ole Sendeka 2018 hadi 2022 aliendesha uovu kama huo kwa shamba la Marehemu Yese ambae alikua rafiki yake lililopo Ngage Wilayani Humo Simanjiro hadi alipoumbuliwa na Naibu Waizir wa Waklatyi huo Ridhiwan Kikwete na pia kuzodolewa na binti mkubwa wa Yese."
Isije ikawa ni REVENGE. Maana Ole Sendeka ni mtu wa DEAL chafu