Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inasemekana kuwa mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Simanjiro.

Amekimbizwa hospitali katika juhudi za kupambania maisha yake.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
Hakuna alie salama..!!

---

Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambulia gari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.

View attachment 2948550

Soma pia > CCM imuadhibu Ole Sendeka kwa kuvamia mashamba na kuharibu amani

Sendeka kamaliza biashara ya Tanzanite Arusha watamuondoa tu. Kaaribu soko watalii hawawezi kwenye kununua Tanzanite migodini! Wachimba mawe hawatamwacha
 
Mwanasiasa Ole Sendeka amenusurika risasi, taarifa imetoka na polisi wamethibitisha.

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna mahojiano ya moja kwa moja na viongozi wake wa chama, bunge wala wanasiasa wenzake

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna Waziri aliyepost kwenye social media account kutoa pole na kukemea, hakuna mwanasiasa wa chama chake aliyejitokeza kulaani. Ila ingekuwa msiba.............

Kwanini sisi siyo wepesi wakurespond kwenye crisis? Pole ole Sendeka.

Mnaosimamia mitandao ya kijamii akaunti za viongozi kuweni active
Ole Sendeka ni mtu wa DEAL chafu sana. Isingekuwa siasa angekuwa jambazi. Muache apate mshahara wa dhuluma
 
Mwanasiasa Ole Sendeka amenusurika risasi, taarifa imetoka na polisi wamethibitisha.

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna mahojiano ya moja kwa moja na viongozi wake wa chama, bunge wala wanasiasa wenzake

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna Waziri aliyepost kwenye social media account kutoa pole na kukemea, hakuna mwanasiasa wa chama chake aliyejitokeza kulaani. Ila ingekuwa msiba.............

Kwanini sisi siyo wepesi wakurespond kwenye crisis? Pole ole Sendeka.

Mnaosimamia mitandao ya kijamii akaunti za viongozi kuweni active
Tumekuelewa bwana
 
Inasemekana kuwa mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Simanjiro.

Amekimbizwa hospitali katika juhudi za kupambania maisha yake.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
Hakuna alie salama..!!

---

Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambulia gari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.

Soma pia > CCM imuadhibu Ole Sendeka kwa kuvamia mashamba na kuharibu amani
Kuna mijitu Haina shabaha!
 
Mwanasiasa Ole Sendeka amenusurika risasi, taarifa imetoka na polisi wamethibitisha.

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna mahojiano ya moja kwa moja na viongozi wake wa chama, bunge wala wanasiasa wenzake

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna Waziri aliyepost kwenye social media account kutoa pole na kukemea, hakuna mwanasiasa wa chama chake aliyejitokeza kulaani. Ila ingekuwa msiba.............

Kwanini sisi siyo wepesi wakurespond kwenye crisis? Pole ole Sendeka.

Mnaosimamia mitandao ya kijamii akaunti za viongozi kuweni active
Tupe kwanza mazingira ya kukoswa koswa na hizo fisasi na mkasa mzima.
Kafumaniwa?
Amepora kitu?

Ole Sendeka anajulikana kwa maongezi yake ya kuudhi, hivyo hatushangai leo kakutana na mkora mwenziwe!
 
Akijieleza kwa Waandishi wa Ayo TV mh Ole sendeka amesema Baada ya kushambuliwa na Wasiojulikana alijibu Mapigo kwa kupiga risasi juu kwa kutumia Silaha nzito nzito na Wasiojulikana wanakimbia

Kumbe Tundu Lisu angekuwa na Silaha siku hawa Wasiojulikana walipomshambulia angeweza kuwadhibiti

Demokrasia ina gharama 🐼
 
Back
Top Bottom