Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amewakosea nini wale jamaa!!?

Huwa hawashambulii TU Bure wale jamaa!!Kuna kitu kafanya!!

de 'levis uko wapi !!?utupe clue!!?

Watu wanafikiri hata Lisu alishambuliwa kwa kuonewa!hapana !Kuna miiko ya kimfumo aliikosea ya wale jamaa ukiivuka TU wanakuijia hata kama wengi wataona unaonewa lakini lazima Kuna mambo utakua ulishaonywa lakini ukashupaza shingo!!

Itakua haikua safe process,tagert atakua alishtukia ndio maaana hawajafanikiwa kwa asilimia mia!!

Matukio ya wakubwa kupigwa risasi nchi hii hayajaanza Leo;-

RIP IMRAN KOMBE

LIVE LONG TUNDU LISU

LIVE LONG OLESENDEKA!!
Kama sio bashite au mwendazake kuna mmoja wao kahusika hapa
 
Tutaona hatua za serikali baada ya mbunge huyu mwingine kushambuliwa, huku aliyekuwa mbunge Mh. Tundu Lissu kesi yake hatupewi mrejesho uchunguzi wake umefikia wapi

Toka maktaba :
10 May 2023
Dodoma, Tanzania

Manusura mbunge wa CHADEMA Tundu Lissu akichechemea kutoka na majeraha aliyopata kutokana na kushambuliwa na watu wasiojulikana mwaka 2017 huku mpaka leo bado jeshi la polisi halijasema uchunguzi wa kipelelezi kama faili limefungwa au la na sababu za jeshi la polisi kuwa kimya, amefika katika ofisi za polisi kuliona gari lake lilolokuwa matundu ya risasi

1711746173526.png

Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Tundu Lissu apigwa risasi na watu ...

7 Sept 2017 — Mwanasiasa huyo amekimbizwa hospitali ya mkoa wa Dodoma na kupokea huduma ya kwanza na taarifa
 
Hapa sioni povu, ingekuwa kipindi kile kelele zingekuwa nyingi haya risasi zinatokea wapi?
 
Taarifa za ndani zinadai kuwa ni Bashite ndiye kafanya unyama huu kwasbb Ole Sendeka amekuwa akikosoa uteuzi wa Makonda kwenye vikao na makundi sogozi.

Makonda mtu hatari sana.
 
Amewakosea nini wale jamaa!!?

Huwa hawashambulii TU Bure wale jamaa!!Kuna kitu kafanya!!

de 'levis uko wapi !!?utupe clue!!?

Watu wanafikiri hata Lisu alishambuliwa kwa kuonewa!hapana !Kuna miiko ya kimfumo aliikosea ya wale jamaa ukiivuka TU wanakuijia hata kama wengi wataona unaonewa lakini lazima Kuna mambo utakua ulishaonywa lakini ukashupaza shingo!!

Itakua haikua safe process,tagert atakua alishtukia ndio maaana hawajafanikiwa kwa asilimia mia!!

Matukio ya wakubwa kupigwa risasi nchi hii hayajaanza Leo;-

RIP IMRAN KOMBE

LIVE LONG TUNDU LISU

LIVE LONG OLESENDEKA!!
Aisee!
Ingekuwa hivyo rushwa na ufisadi vingekuwa vimeisha nchini.
 
Toka maktaba uchaguzi wa ndani CCM 2015 :

Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto​

Gari la Ole Sendeka lavunjwa vioo,Ole Nangoro anusurika kichapo
· Nyumba yake yavamiwa na wanachama, wavunja taa na kumpiga mlinzi

Habari kwa kina :

Agosti 11, 2015

Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
1711747097021.png

·1711747007246.png
1711747049672.png

MwanganaMatukio

Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto​

Agosti 11, 2015



Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
·


Ripoti:
Na. Mohamed Hamad, Manyara

JESHI la polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara limetumia mabomu ya machozi na silaha za moto kuokoa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro na Christopher Ole Sendeka pamoja na kamati ya siasa ya Mkoa wa Manyara waliofika kuhakiki matokeo ya Ubunge

Awali wajumbe hao walizuiwa kwa mawe na magogo barabarani kata ya Engusero wasifike makao makuu ya wilaya ya Kiteto wakitokea Dodoma, hali iliyolazimu Jeshi la Polisi kuwaokoa kwa kuwapa ulinzi kwa kuwafikisha Kibaya kwaajili ya kuhakiki matokeo hayo
Baada ya kamati ya siasa ya mkoa kufika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto majira ya mchana walianza kuhakiki matokeo ya Ubunge ambayo yalidaiwa kulalamikiwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro aliyeambatana na wajumbe hao kutaka yahakikiwe

“Baada ya kusikia kuna kamati ya siasa mkoa wa Manyara imefika wanachama tulilazimika kufika ofisi za CCM kutaka kujua hatma ya ujio wao, kwani tumeshuhudia maeneo mengi matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa baada ya kutangazwa washindi”alisema mwananchi Rajabu Jagon

Alisema wajumbe hao waliingia ofisini ya CCM kwa zaidi ya masa 6 huku wanachama wakisubirinje hali iliyohofiwa kuwa huenda walilenga kubadilisha matokeo hayo na ndipo kauli za kejeli vitisho zikaanza kutolewa na baadhi ya wajumbe hao na kuwafanya wanachama wapandwe na jazba

Christopher Ole Sendeka mjumbe wa kamati ya Siasa mkoa wa Manyara baada ya kutoka nje alionekana kuibua malumbano na wanachama hao wakidai aliwakashifu hali iliyowapandisha jazba vijana hao na kuanza kurusha mawe kutaka kumpiga.Hali iliyowafanya polisi kuingilia kati kunusuru

Muda mfupi Christopher Ngubiagoi mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa aliyefuatana na kamati hiyo alitoka nje kutuliza mzuka wa wanachama hao bila mafanikio na ndipo mawe yalipoanza kurushwa na kuvunjwa kioo cha nyuma cha gari la Ole Sendeka na ndipo Polisi wakaanza kurusha mabomu na silaha za moto juu

Tukio hilo lilichukua takriban dakika arobaini na tano baada ya wanachama hao kupambana ana kwa ana na polisi ofisini hapo huku wakijaribu kuwaokoa wajumbe kwa kuwalazimisha watoke kwenye ofisi hizo kwa kurusha mabomu na kutumia silaha za moto

Hii ni mara ya pili kwa mbunge anayemaliza muda wake Ole Sendeka kupata wakati mgumu baada ya dereba wake kumwondosha katika ofisi hizo mithili ya kukwepa majambazi huku akiendelea kushambuliwa kwa mawe hadi alipotoweka katika viwanja hivyo

Katika sakata hilo Jambo leo limeshuhudia uharibifu uliofanywa na wanachama hao kwenye nyumba ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Ole Nangoro ikiwa imevunjwa taa za nje kwa kama ishara ya kutomkubali katika utawala wake

Kwa mujibu wa Christopher Ngubiagaji mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa aliwaambia wanachama hao kuwa hawakuja kubatulisha matokeo, alitumwa na Katibu wa CCM Taifa Abdurahmani Kinana kuhakiki matokeo hayo yaliyolalamikia na mmoja wa wagombea

Pia alisemba mbali na hilo alikuja kuona hali ya kisiasa kwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kama anaweza kupambana na mgombea kupitia umoja wa vyama UKAWA ili kuwezesha CCM kuendelea kutawala

Kufuatia kauli hiyo mjumbe huyo alisema “mwenye macho haambiwi tazama,hana shaka na kilichoamuliwa na wana-CCM Kiteto na kwamba ataenda kumwambia Kinana kuwa maamuzi wa wanakiteto yanaeleweka ili naye aweze kufanya maamuzi yake

Kauli hiyo iliungwa mkono na katibu wa CCM Wilaya Abeid Maila aliyesema kilichotokea Kiteto hakihusishwi na kiongozi yoyote, bali wananchi waliamua kutaka kujua hatma yao kuwa walichokifanya ni sahihi na wala hawataki kibadiliswe
Mwisho
 
Hapa ndio kuna tatizo.
labda anapinga ardhi ya wamasai kuporwa kupewa mwarabu awinde, wamasai wanafurumushwa na serikali kupisha ujenzi wa hoteli ya mwarabu ina trend dunia nzima isipokuwa tanzagiza tu ndo watu labda hawajui …
 
Kwa minajili ya kuendelea tunahitaji mambo manne
  1. Ardhi
  2. Watu
  3. Siasa Safi
  4. Uongozi Bora
Ardhi tunayo, Watu tupo, Siasa Safi hakuna, Uongozi bora hakuna. Hivyo kwa Mbunge Ole Sendeka kushambuliwa in plain light ni ushahidi mzuri wa kulegalega kwa vyombo vyetu vya usalama. Vipo bize kufukuzana na watu wadogo mitaani badala ya kuishi kwenye jukumu lao la Kikatiba
 
Back
Top Bottom