Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Nadhana mtoa mada jibu analo.
Mkuu wa Inchi hawako vizuri na Mbunge wetu.
Mkuu wa Inchi ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya Kiserikali kuhusu kuendeleza miradi ya maendeleo.
Mbunge Mwigulu ana conflict of interest na Mkuu wa Inchi kwa sababu Mwigulu bado anautaka Urais kama sio 2020 basi 2025.
Bado kuna maandishi yaliyoandikwa juu ya majabali mengi kando kando ya bara bara za Singida Arusha na Singida Dar kuwa Mwigulu ni Rais 2015. Mwandiko unafanana kwenye majabali yote na hadi leo takriban miaka 4 hayajafutwa.
Kwenye BASI la Timu ya Singida United kwa nyuma kuna picha kubwa ya Mwigulu ambayo inamtangaza Inchi nzima bila kuwekwa wazi kuwa yeye ni mfadhili au mlezi.
Wengi wanatafasiri kuwa hizi nazo ni Kampeini za kuutafuta Urais 2025.
Katika haya yote tumwombee afanikishe ndoto yake ya kuupata Urais ili mradi havunji kanuni na Sheria za Inchi.
Itakuwa ni Heshima kubwa kwa Wana Singida kama Rais atakuwa Mwigulu kwa mwaka 2025.
Kwa mwaka 2020 aungane na Rais wetu wa sasa katika kumfanyia kampeini ili ashinde kwa kishindo katika nafasi yake ya kikatiba ya kugombea Urais kwa awamu ya pili.
Mwigulu aungane na rais wako kumfanyia kampeni ili ashinde kwa kishindo, kwani yeye hajui kuwa rais hahitaji kampeni au kura hata moja ili kuwa rais? Rais anahitaji tu jeshi linaloweza kumtii na tume ya uchaguzi itakayotangaza idadi ya kura atakazo. Kama kutakuwa na upigaji wa kura ni ili kuwazuga wazungu kwamba ameshinda kwa kura, lakini kura sio kikwazo cha yeye kutangazwa mshindi. Mazingira ya ushindi wa figisu Mwigulu anayajua vyema.