Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!

Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!

Nadhana mtoa mada jibu analo.
Mkuu wa Inchi hawako vizuri na Mbunge wetu.
Mkuu wa Inchi ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya Kiserikali kuhusu kuendeleza miradi ya maendeleo.
Mbunge Mwigulu ana conflict of interest na Mkuu wa Inchi kwa sababu Mwigulu bado anautaka Urais kama sio 2020 basi 2025.
Bado kuna maandishi yaliyoandikwa juu ya majabali mengi kando kando ya bara bara za Singida Arusha na Singida Dar kuwa Mwigulu ni Rais 2015. Mwandiko unafanana kwenye majabali yote na hadi leo takriban miaka 4 hayajafutwa.
Kwenye BASI la Timu ya Singida United kwa nyuma kuna picha kubwa ya Mwigulu ambayo inamtangaza Inchi nzima bila kuwekwa wazi kuwa yeye ni mfadhili au mlezi.
Wengi wanatafasiri kuwa hizi nazo ni Kampeini za kuutafuta Urais 2025.
Katika haya yote tumwombee afanikishe ndoto yake ya kuupata Urais ili mradi havunji kanuni na Sheria za Inchi.
Itakuwa ni Heshima kubwa kwa Wana Singida kama Rais atakuwa Mwigulu kwa mwaka 2025.
Kwa mwaka 2020 aungane na Rais wetu wa sasa katika kumfanyia kampeini ili ashinde kwa kishindo katika nafasi yake ya kikatiba ya kugombea Urais kwa awamu ya pili.

Mwigulu aungane na rais wako kumfanyia kampeni ili ashinde kwa kishindo, kwani yeye hajui kuwa rais hahitaji kampeni au kura hata moja ili kuwa rais? Rais anahitaji tu jeshi linaloweza kumtii na tume ya uchaguzi itakayotangaza idadi ya kura atakazo. Kama kutakuwa na upigaji wa kura ni ili kuwazuga wazungu kwamba ameshinda kwa kura, lakini kura sio kikwazo cha yeye kutangazwa mshindi. Mazingira ya ushindi wa figisu Mwigulu anayajua vyema.
 
tindo
Upumbavu uliojitokeza wakati ule kuanzia Lowassa na wafuasi wake na maumivu yake sidhani kama kuna mtu ndani ya Chadema anaweza kuurudia na hata kuuzungumzia tena.
Lakini yote in yote, hakuna kuzungumzia sijui uchaguzi utakuaje au nini, habari iwe tume huru ya uchaguzi tuu. Viongozi wasipotumia nguvu zao kwa hiyo agenda nasi kuwaunga mkono basi nchi imekwisha!

Mkuu hilo la tume ya uchaguzi naona ni sisi tu tunaongelea humu mitandaoni, lakini sioni vyama vya upinzani wakizungumzia hilo. Leo nimesikia wanaongelea kuhusu wito wa viongozi wa ccm huko ikulu.
 
Mkuu huu ushauri unaoutoa kwa Mwigulu ni kama unamdanganya tu, Mwigulu hana uwezo wowote wa kuwa na maisha ya juu nje ya siasa za mbeleko za ccm. Na hana uanaume wowote kama hana mbeleko ya vyombo vya dola. Mwigulu uliyekuwa unamuona jasiri ni kwakuwa alikuwa anazungukwa na vyombo vya dola, na alikuwa anaweza kuagiza kufanyika ukatili wowote kutokana na madaraka yake. Nje ya madaraka Mwigulu ni sawa na kasichana ka shule ya awali. Atajijinyenyekeza kwa Magufuli taka asitake, kwani anajua aliyoyafanya kaburi likifukuliwa atakuwa mpishi huko jela.
....Nje ya madaraka Mwigulu ni sawa na kasichana ka shule ya awali! Nimeupenda huo mfano wa kweli.
 
No Mwigulu sio mbumbumbu ni kichwa sana
P
Kwa mfano hii niliwahi kuisoma siku hizo ila sikutaka kuijibu kivyovote vile. Ila swali nililokuwa najiuliza ukiangalia Mwigulu kwenye records za Bunge Mwigulu anaonekana kuwa alizaliwa Mwaka 1975 hata juu anaonesha kuwa aliachia darasa la tano Mwaka 1985 akimaanisha kuwa wkt huo alikuwa na miaka kumi. Kwa tuliosoma miaka hiyo hiyo kitu hamna kabisa - kwamba Mwigulu alianza darasa lwa kwanza akiwa na miaka mitano. Ajabu sana! Huyu jamaa ni mjanja na mwongo sana!
 
Education wise he is brilliant, ana 1st class ya Economics from UDSM na aliajiriwa BOT.

P
Aaah Pascal, kupata 1st class UDSM na kuajiriwa BOT ndio kipimo cha competency yake ili kupewa kazi mashirika ya kimataifa akiomba? Kumbuka katoka lini chuoni na huko BOT, jee hii miaka baada ya BOT nini kafanya kwenye professional yake?
 
Pascal Mayalla, Tatizo Mwigulu akiwekewa mizengwe CCM anaweza kukimbilia wapi wakati hakuna ruhusa ya mgombea binafsi?

Shida ya Mwigulu wakati wa madaraka vyama vingine alivifanya adui na kuviona takataka nani anaweza kumpa nafasi hata kama anao wapiga kura wa kutosha?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama gia ilibadilishwa angani na mmoja wa waliokuwa ndani ya list of shame ya Mwembe Yanga sembuse, huyu ambaye hakuwemo kwenye list hiyo!!
 
Angalia uwongo huo - Mtu azaliwe 1975 halafu Mwaka 1985 aachie darasa la tano!

 
Paskali hapa ni kama unacheza tu na maneno, sio mara moja au 2 umekuwa ukileta hizo trend readings zako kama utabiri. Hilo la kwamba uchaguzi wa mwaka huu wapinzani wanaenda kuwa dumped umelichomeka ili kuupa utetezi wako nguvu.
No kila nikiweka trends readings nasisitiza kabisa sio utabiri!




P
 
Mkuu Pythagora unauliza ninataka kusemaje hapo wakati tayari nimeishasema au ulitaka nisemeje?.
P
Hahaaa nilitaka kuona una msisitizo gani maana umetuptia quote ya ulichoandika mwaka juzi kuhusu wasiojulikana, nilitaka kuona msimamo wako ni uke ule au imebdilika? Ni hilo tu Pascal Njaa.
 
Wewe ni Mchumi na siku zote wachumi huelezea uhalisia wa mambo kwa namba. Wataalamu wanadai "namba haziongopi".

Mheshimiwa umekosa ujasiri wa kusema mambo ambayo umeifanyia Iramba kwa sababu hamna ulichofanya ambacho unaweza kujivunia.

Au unataka kuongelea kwa mfano shule yako ya Kata yaani Kyengege kutoka nafasi ya 15 kimkoa Mwaka juzi na kufikia nafasi ya 8 kwa Mwaka jana hayo ni mafanikio?

Viko wapi visima vya maji ulivyoahidi katika vijiji mbalimbali vya Iramba, umeshinikiza vipi Mradi wa umeme wa REA kukamilishwa pale ulipokomea?

Ukiacha Kituo cha Afya cha Kinampanda wapi kwingine unapojivunia uliacha?

Ukweli ulikazania siasa za Kitaifa za kutaka uwe Rais - wapi sasa maendeleo uyaonayo yameletwa na siasa zako za Kitaifa zaidi ya kuzidi kunyongonyezwa tu wewe na Nape na Januari?

Na inadaiwa umewekewa TISS wa kumwaga tu hadi chumbani kwako!

Kikubwa tumia akili achia ngazi mapema, tafuta kitu bora zaidi cha kufanya ili kuepukana na Rais Magufuli kwenye siasa kwa kuwa kwa vyovyote anavyokuchulia wewe ni threat kwake atahakikisha anakukata juu kwa juu na Ubunge hutopata!
Mwigulu Malipo ya Ubaya ni hapa hapa Duniani wala sio Mbinguni Mungu ana mambo mengi ya kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtabiri ni sheikh Yahaya, watabiri wanatumia nyota, au ramli etc, mimi ni msoma trends, kusoma trends ni kuangalia tuu mielekeo, mfano leo ni January uchaguzi ni October, nikikuambia kuna uwezekano hakuna hata Mbunge mmoja wa Chedema atakayerudi Bungeni, ikitokea utasema ni utabiri?. No sio utabiri ni trends tuu.

P

Kwa hili la kwamba hakuna mbunge wa upinzani atarudi bungeni hasa wa cdm uko sahihi sana, bila kujali ni trend readings au utabiri. Na sio kwasababu ccm wanakubalika sana ama cdm hawachaguliki, bali sababu hasa ni kwakuwa rais aliye madarakani hawezi siasa za ushindani, na ana chuki ya wazi dhidi ya cdm. Kwakuwa katiba yetu ina madhaifu, basi rais aliye madarakani anatumia nguvu yake ya kimadaraka kuamua nani awe kiongozi katika chaguzi zetu, na kwakuwa taasisi zilizopo pia zinatii kila atakacho rais bila kujali uhalali wake, basi lazima kiongozi anayemtaka rais awe ndio anayekuwa, bila kujali sauti ya box la kura. Hili wala halihitaji mjadala, kwani hizo siasa chafu kila mtu anaziona na kuzifahamu.
 
Kwenye hili la karma, naomba kumtetea Mwigulu.

Kuna viongozi wengi wametumbuliwa katika hao wanaotumbuliwa kuna baadhi kweli ni majipu na sababu za kutumbuliwa huwa zinawekwa. Lakini wengine wanatumbuliwa tuu kwa sababu nyingine na sio majipu, hawa wanaotumbuliwa ambao sio majipu, sababu za kutumbuliwa kwao huwa hazitolewi, Mwingulu Mchemba ni mmoja wa watu hawa, sasa kwa mujibu wa taarifa za koridoni zilizopelekea Mwigulu kutumbuliwa, naomba uniamini mimi, karma haitamhusu!.

Ukipitia bandiko hili, kuna kitu nilikisema kumhusu Mwigulu kabla hajatumbuliwa kilichopelekea akatumbuliwa ila huyu sio jipu!.

P
Ndugu Mayalla
Kweli yalioandikwa na mleta mada Kumbuka Mtu wa Mara,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi bado anavaa lile tambara shingoni kama alivyokuwa akijimwambafay?
 
Boss Mnambua Shilole ..... Katangaza nia ....


Wewe ni Mchumi na siku zote wachumi huelezea uhalisia wa mambo kwa namba. Wataalamu wanadai "namba haziongopi".

Mheshimiwa umekosa ujasiri wa kusema mambo ambayo umeifanyia Iramba kwa sababu hamna ulichofanya ambacho unaweza kujivunia.

Au unataka kuongelea kwa mfano shule yako ya Kata yaani Kyengege kutoka nafasi ya 15 kimkoa Mwaka juzi na kufikia nafasi ya 8 kwa Mwaka jana hayo ni mafanikio?

Viko wapi visima vya maji ulivyoahidi katika vijiji mbalimbali vya Iramba, umeshinikiza vipi Mradi wa umeme wa REA kukamilishwa pale ulipokomea?

Ukiacha Kituo cha Afya cha Kinampanda wapi kwingine unapojivunia uliacha?

Ukweli ulikazania siasa za Kitaifa za kutaka uwe Rais - wapi sasa maendeleo uyaonayo yameletwa na siasa zako za Kitaifa zaidi ya kuzidi kunyongonyezwa tu wewe na Nape na Januari?

Na inadaiwa umewekewa TISS wa kumwaga tu hadi chumbani kwako!

Kikubwa tumia akili achia ngazi mapema, tafuta kitu bora zaidi cha kufanya ili kuepukana na Rais Magufuli kwenye siasa kwa kuwa kwa vyovyote anavyokuchulia wewe ni threat kwake atahakikisha anakukata juu kwa juu na Ubunge hutopata!
 
Mkuu Mnambua, kwanza mimi sio mtabiri, mimi ni just a commentator,

Kazi ya kuwataja wagombea wa uchaguzi wa 2015 tuliianza toka 2011 kama ambavyo kazi ya kuwataja wagombea wa 2025 turaianza 2021.

kwenye wagombea wote zaidi ya 40 wa CCM, niliwagawa katika mafungu 10 na kutoa list yangu ya 10 bora katika kila fungu

Wengi Magufuli walimjua 2015 baada ya kuteuliwa, angalia akina sisi tulimtaja lini


Huu sio utabiri ni trends readings, usomaji mielekeo. Mfano mzuri ni mwaka huu, huu ni mwaka wa uchaguzi na Tanzania tuna vyama vingi, mwelekeo unaelekeza upinzani unakwenda kuwa dumped totally, Bunge lijalo ni Bunge la CCM predominantly. Hili likitokea utasema ni utabiri?. No sio utabiri ni mielekeo.
P
Mkuu Pascal Mayalla labda hujamuelewa hoja yake.... Anachosema yeye ww unabashiri kila kitu kwa pande zote alafu moja wapo likitick uonekane ww uliona mapema.

Mfano siku zitto anatimuliwa uliandika either zitto atapotea au Lissu atapotea..... Anyway ACT haikufurukuta 2015 so ukadai ni karma kwa zitto. Baada ya Lissu kupigwa risasi ukadai tena huenda ni karma kwa lissu kwa kumtesa zitto, bado hapo hapo uliuliza Je lissu anafaa kupambana na magufuli 2020??

Sasa ni hivi
ACT ikiwa KUB 2020 utasema ni karma kwa CHADEMA kwa issue ya zitto.

Lissu akishinda utafufua uzi uliodai anafaa kugombea u-Rais

CHADEMA ikishinda utafufua uzi wa 2011 uliodai chadema haijakua ila IMEPAA.

Yaani you predict both sides of the coins with vague,cryptic and open-ended predictions such that the probability of making a successful guess is imminent!!

tindo
 
Kama kuna mabaya alitenda kwa wanadai kulipia madaraka, akaombe msamaha watu/familia . Madaraka yanakiburi ujeuri
 
Hivi nyie mnaosena eti raising ndio ndio mwenye kuamua mustakabali wabnani awe mbuge mlitaka nani awe na kauli ya mwisho kwenye kamati ya uteuzi, kuna maana gani kuwa mwenyekiti halafu huna meno.Watu wasiokubaliana na unachokifanya wawe wabunge kuna maana gani ya wewe kuwa na power? Bunge ni sehemu ya serikali hivyo raisi lazima awe na watu wanaomsapoti na sikumuhujumu au kumpinga.Mambo Hays hayajanzia kwa magufuli bali J.K.N hivyo magu anafuata mkondo, muacheni afanye yake atakapotoka mtafanya yenu, msipangie watu wa kufanya nae kazi.
 
Wananchi wamewachoka wabunge wa kwenda bungeni wanashindwa kuwatetea wale wanaowachaguwa.Kila kitu ni kusema ndiyoo naunga mkono 100% wanatetea tumbo lao basi muda umetimia mkulima ,mfanyakazi ,wasiyojiweza,tegemea maswali yao .
 
Back
Top Bottom