Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Huwajui breed hii ya mbwa mzee!

Hawa hata wafugwe na malaika na wamzoee toka akiwa mdogo bado watamnyofoa mapumbu siku 1.

Hii breed hii ya mbwa hawanaga kumbukumbu, uwezo wao wa kufikiri haujafikia GB, siyo MB, ana memory capacity ya KB 11
Unakuta kuna bwege anajifanya anawajua anavyowatetea huwa nasema wewe fuga siku waje wakamate shingo ya mtoto wake aone walivyo hatari ndipo sasa ataiona ile kauli ya msiba usikie kwa jirani.
 
Hapana huyo anajua kila kitu, jambo la kwanza kwa mtu yoyote anapokwenda nunua kitu lazima ataulizia model ili ajue anafuga nini.

Huyu aliambiwa na alijua anachukua toleo gani la mbwa. Ni wale watu wajuaji wanapoambiwa kitu fulani hakifai yeye anataka kujifunza kwa gharama anata kuprove kuwa yeye ana maamuzi ya kitofuti.

Kuna m'moja hapo Arusha na yeye aliyachukua haya maumbwa akafuga, yalimuulia mtoto wake mdogo wa miaka 2. Hadi leo nadhani akiona hawa mbwa kwenye tivi anaweza vunja.

Imagine kupoteza mtoto wako kizembe sababu ya ujuaji mwingi na kujifanya wewe unajua sana mbwa. Maumbwa mawili yalikamata shingo ya mtoto yalimrarua huku mwingine amekata paja.

Nadhani jamaa akikumbuka ile tukio anakaa chini analia sana right kama angesikiliza maneno ya watu wenye hekima walipomwambia haya maumbwa sio ya kufuga yeye akasikiliza maneno ya dog trainer aliyekuwa anamwambia hawa mbwa ni wazuri ukiishi nae hivi na vile.
 
Mbwa hawezi kupoteza kumbukumbu. Inawezekana hao wanafamilia hawajazoea kuwa nje muda huo hivyo kupelekea mbwa kutowatambua badala yake wameonekana kama wavamizi, wezi n.k
Umeambiwa huwa wanawapaga chakula it means wameshachangamana nao. Mbona watu wengine mnakuwa na vichwa vizito kuelewa, unatetea vitu ambavyo ni hatari.
 
Hayo ndio madhara ya kufuga mbwa kama mbuzi. Mbwa ni mnyama hatari ila mwenye akili, unatakiwa umzoeshe na awajue wanafamilia wote kwa harufu na sura. Ila ukimfungia na kumtoa usiku matokeo ndio kama hayo.

Alafu kingine ni kwamba wanyama na Waafrika ni vitu viwil tofauti.
 
Afrika ni zero brain,badala wapige risasi za usingizi kisha wachunguze kwa nini wamebadilika ghafla-wao wanaua.
Waliosema akili ni mali hawakubahatisha-kwa kweli.
Wewe ndio huelewi nini kimefanyika hapo. Mbwa anaposhambulia watu especially wanaomfuga anatakiwa kuuwawa mara moja maana ni hatari ameshajifunza disobedience hatotii tena.
 

Bulldog ni wanyama wa mwituni sio wa kukaa maeneo ya makazi ya watu. Kwenye report za uvamizi wa mbwa kwa wamiliki wao, Bulldog wanaongoza. Wenzetu nje baadhi ya familia wameshaanza kutemana na hii breed.
 
Hao mbwa kama unamfuga hakikisha unafuata masharti yake kuanzia mda wakula, aina ya chakula, mazoezi, tiba, na watu maalumu wakuwahudumia ukikosea kidogo tu ni hasara kwako na familia, mbwa wa matajiri hao, wengine tufuge tu Hawa wanao zurura Koko beach
 
Kwani hawakuwa na risasi za kuwafanya wasinzie hawa maliasili.

Sema haya mabulldog inaelekea si ya kuyaamini maana nishasikia story nyingi za hata kuwageuka wenye nayo
Haya si ndiyo yalimwua mwanasoka wa zamani wa Zambia kule South Africa? Mnafuga madude gani haya? Bwana mdogo naye liliwahi kumgeuka bahati yake mafunzo ya kijeshi yakamwokoa akalidhibiti kama anadhibiti gaidi kwenye vita! Ilikuwa hatari sana!
 
Koko ukimfuga kizungu na mafunzo juu anakuwa mbwa poa tu 😀
Hivi hii inawezekana mkuu? Mimi napenda mbwa ila koko tu, hii kujifanya mjuzi sana wa haya ma mbwa breed zingine hapana.

Koko anakaa sawa tu ukimpa treatment za hizi breed zingine?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]eti mara mia ufuge Simba [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifuga mbwa unatakiwa umzoeshe watu tokea akiwa mdogo, na uwe unampa mazoezi ya kutosha, haswa mbwa wakubwa wenye nguvu.

Watu wanakariri kufuga mbwa wa kizungu fashion, kama unamnunua ili akae bandani atoke usiku tu bora uache.
Ndugu sio hao sijui Bulldog/pitbull. Hao ni mbwa wa hovyo kabisa kufuga na anayefuga huwa namshangaa sana. Yaani huwa sijui wanapataga wazimu maana kikinuka hata wewe mfugaji mwenyewe wanakujeruhi kama sio kukuua kabisa. Nikijua una hao mbwa kwako hautaniona milele hata uwe ndugu yangu wa damu siji kabisa. Mbwa gani ukikaa na mwenyeji anakuwa mpole kabisa anachezesha tu mkia kama rafiki subiri sasa mwenyeji ajisahau aingine ndani labda kuchukua simu yake inaita wee akirudi anakuta unavuja damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…