Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2023 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985

Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

C & P FROM X
- Pdizaina05
bahati ni kwamba meno ya bull dog hayana ncha kali kama german sherfad au rottweiler,meno yao yapo kama punje za mahindi,,lakini kiuhalisia bull dog hawana akili wala kumbukumbu nzuri,na ni wazito sana wakati kuwafundisha,ni mbwa niliobahatika kuwafundisha lakini kichwani hamna ki2 tofauti na german shrfad
 
Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.
Mzee Kingunge naye alikumbwa na mkasa kama huu, ila kwa Misungwi huenda walikuwa mbwa mtu usishanga siku chacche kuwaona mbwa wamerejea wakiwa wazima na furaha
 
Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2023 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985

Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

C & P FROM X
- Pdizaina05
Cheki dude hili
images (44).jpeg
 
Back
Top Bottom