Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Hata ng'ombe kuna mmoja alishawahi kumuua Boss wake huko kijijini
Wengine wanakuwa na visirani na kuna mmoja ashawahi kunitimua mbio
Ndo mana nimeshauri Fuga mbuzi, ushawai sikia mbuzi kang'ata mtu wewe je ushawai sikia mbuzi kampiga free kick mtu.
walaa mbuzi Wapole unaweza ukamchinja bila kumfunga kamba ukamkanyaga miguu kama kuku mbuzi akatulia zake kutimiza ibada aliyoandikiwa na mola
 
Asee, Pole sana kwa familia.
Huyu sio Bulldog na sio pure Pitbull.

Huyu nahisi amecross Pitbull na Boerboel.
Pitbull ni mbwa wa kufuga kwa upendo mkubwa mno, na hautakiwi kumfanyisha aggressive training yoyote. Yeye anafundishwa obedience tu.

Ukimfanya kama mbwa wa Ulinzi niamini mimi utalia na kusaga na meno especially ukiwa na familia na watoto wadogo.

All in all kibongo bongo hatujui kuwafuga hawa jamaa, My take ni kuacha kufuga hii jamii ya mbwa.

Hao ni special kwa kuwinda wale Wild Boar [Nguruwe Pori] and they are designed to bite and to kill na sio kujeruhi tu.
 
Kama hujui ni heri uulize nikupe somo, mapepo yanaweza kuvamia kwa mnyama na kuweka maskani kichwani pake.
Hao ni Crossbreeding iliyofanyika maabara,ina maana hao mapepo wavamie bulldog tu wasivae hawa mbwa koko wetu wa mtaani?
Tumia hata ufahamu wako kidogo tu maana akili zote mmewaachia wachungaji wafanye chochote wanachotaka.
Halafu kingine unaijua rabies?
 
Duh! Pole sana kwa familia kwa majeraha.

Mbona ni balaa sana km vile unamfuga simba/chui.

Naona wamenikatisha kabisa tamaa ya kufuga mbwa sasa! Itabidi tu niwe na masai sasa!
Masai walikuwa zamani. Siku hizi ni wataalamu wa kuchora michoro na kuwapa ramani wezi. Utakuta nyumba inavamiwa na masai wako kafungwa kamba mikononi kama geresha tu.
 
Mimi na kambwa koko kangu nilikanunua sasa nikawa nakatrain kwa kukapiga na kukapa mateso kama walimu wa mbwa wa jamiiforums walivyosema , ajabu kalipopata mpenyo wa kutoka getini hili ni juma la tano hakajarudi nyumbani nikimuona mtaani ni mwendo wa mbio tu [emoji848]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Inaonekana ulikazidishia msoto
 
Ukifuga mbwa unatakiwa umzoeshe watu tokea akiwa mdogo, na uwe unampa mazoezi ya kutosha, haswa mbwa wakubwa wenye nguvu.

Watu wanakariri kufuga mbwa wa kizungu fashion, kama unamnunua ili akae bandani atoke usiku tu bora uache.

Huyo mbwa hata umfuge akiwa mdogo ana akili mbili tu akichukia anakulalua kama nyama na unakufa siwez kufuga aina ya hawa mbwa ni wakatili mno na wana nguvu kama powertila ogop sana na usijarib bora ufunge wale shefad dog ila hayo ptbl utashangaa siku yanaondok na kinyeo
 
Unafugaje mbwa mkorofi kwa wenyeji, kesi zao zimezidi ikiwezekana serikali ipige marufuku breed ya Bulldog.

Fugeni hawa umidogi hawana mbwembwe na ukifirisika hawakutishii usalama. Ni kitendo cha kuwafungulia wanazurula wanajua kila kona yenye msiba na harusi. Wakishiba wanarudi kulala nyumbani.

1000194035.jpg
 
Hao ni Crossbreeding iliyofanyika maabara
Hata kama ilifanyika maabara pepo akiona upenyo tu hutinga ndani ya bongo na kuuthibiti.
maabara,ina maana hao mapepo wavamie bulldog tu wasivae hawa mbwa koko wetu wa mtaani?
Sijasema kwamba mapepo huvamia bulldog pekee, mapepo yanaweza kuvamia mbwa koko, binadamu, nguruwe nk.
Tumia hata ufahamu wako kidogo tu maana akili zote mmewaachia wachungaji wafanye chochote wanachotaka.
Nachokisema hapa sijakitoa kwa mchungaji bali nimechunguza mwenyewe kwa kusoma vitabu mbalimbali ikiwemo Biblia.
Halafu kingine unaijua rabies?
Kwani hiyo rabies inapokuja akili za mbwa huhamia wapi?
 
Back
Top Bottom