Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

kwa uzoefu wangu wa picha hiyo hao mbwa sio bulldog....huyo ni boerbol ...kifupi kwa wafugaji wa mbwa hasa ukiwa na familia mbwa yeyote kama hawa jamii wa bulldog sio wakufuga.
Mbwa mzuri mwenye kukumbuka fadhila ni German Shepherd pekee. Kwa anayehitaji pure shepherd puppy anidm natuma mikoani pia
 
Inaonekana ulikazidishia msoto
Walisema niwe nakakung'uta ipasavyo katakuwa kakali na kweli kalianza dalili za ubabe hata kwa kuku na sungura ni mwendo wa kubweka nikasema mambo ndiyo haya .

Ila alipoweza kunitoroka hajarejea tena zaidi kawa mbwa wa mtaa na ukali alishaacha nimemfuatili kumkamata mara kumuomba msamaha ila kambwa kangu kamegoma kurudisha moyo nyuma [emoji849]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Nawasalimu kwa jina la Bull dog aka mbwa jeuri
Bulldogs zenyewe sura tu ni zaidi ya kauzu
Sura mbayaaa , sijui wanayapenda nini haya mambwa ya kizungu ,au ndio kuiga ?
Screenshot_20240109-154207~2.jpg
 
Ukifuga mbwa unatakiwa umzoeshe watu tokea akiwa mdogo, na uwe unampa mazoezi ya kutosha, haswa mbwa wakubwa wenye nguvu.

Watu wanakariri kufuga mbwa wa kizungu fashion, kama unamnunua ili akae bandani atoke usiku tu bora uache.
Mkuu hawa mbwa hata wakimzoea mtu wanaweza kumgeka muda wowote. Kuna watu wengi wameshapoteza maisha kwa sababu ya kushambuliwa, tena watu wa familia yenye mbwa.
 
Kuna matunzo ya kuwapa(tokea wakiwa wadogo) sema wabongo hatufatilii ni ujuzi kabisa unaitwa dog handling, hapo hatujazungumzia mafunzo(training).

Ukiona mbwa anasumbua, kapata malezi mabaya.

Itoshe kusema wabongo hatuwezi fuga hawa mbwa wakubwa wakubwa wakali, ni process.
 
Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2023 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985

Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

C & P FROM X
- Pdizaina05
Tatizo hapo ni moja tu hawa walioshambuliwa wamekuwa wakiishi na hao mbwa kama mbwa na si kama rafiki. Yawezekana mtu aliyetoka nje mara ya kwanza hana mazoea na hao mbwa. Na wakati anatoka ndani ya nyumba mbwa walikuwa upande mwingine hivo wamestuka kumwona na baada ya mbwa kumfuata hakuonyesha ishara kuwafaham mbwa ikiwa ni pamoja na kuwaita kwa majina.

Jambo la pili yawezekana hawa mbwa amewanunua wakiwa wakiwa tayari wakubwa na kuna baadhi ya tabia walikuwa nazo awali au kuna vitu walikuwa wanafanyiwa na sasa havifanyiki.

Jambo la tatu je hao mbwa wana mafunzo kwa maana ya kutii amri za master wao wao? mbwa wanaishi kwa tabia ya makundi maanake ni kuwa lazima kuwa na Pack na awepo master. Mfugaji usipochukuwa jukumu la kuwa master mbwa atatake over na yeye kuwa master.

Jambo la nne je kama familia wametenga muda wa kuwafanyisha mbwa wao mazoezi ili wasiwe bored na kujiona kama wana adhibiwa? Kama umeaamua kufuga mbwa wa kundi hili:- 1. Rottweiller 2. Bull Dog 3. American Pitt Bull 4. Great Dane 5. Bull mastiff 6. Pitt Bull Terrier 7. Cane corso na BoreBorel kama hauna muda wa kutosha kuwafanyisha mazoezi tafadhari achana nao. Fuga mbwa kama German Shepherd nk. Na endapo familia yako hawapendi mbwa weka mipaka mbwa wakishafunguliwa mtu asitoke nje.

Niliwahi kuandika kwa urefu sana kuhusu mbwa hawa wakizungu kwa wao wenyewe wazungu wanakwambia hiyo jamii hapo juu ni loaded guns on the table, muda wowote inaweza kufyatuka.

Again dogs are very friendly animals only if you know and understand their ABC. Pole sana kwa waanga na next time achukuwe somo ni namna gani ya kuishi na hawa viumbe. Mimi nimefuga hawa wadudu kwa muda mrefu na ninao jamii tofauti nyumbani kwangu mpaka mtaani wanaita kwa Mambwa lakini sijawhi pata kesi nyumbani zaidi ya kesi za mtaani ambapo nilikuwa na mbwa jamii ya Belgium Malinious ambaye alikuwa anaruka ukuta wa kozi kumi za block na kwenda kuattack wapita njia. Nilitafuta namna ya kumdhibiti ikiwa ni pamoja na kumhasi then hamna tena shida.
 
Asante kwa maelezo yalioshiba.
 
Kuna matunzo ya kuwapa(tokea wakiwa wadogo) sema wabongo hatufatilii ni ujuzi kabisa unaitwa dog handling, hapo hatujazungumzia mafunzo(training).

Ukiona mbwa anasumbua, kapata malezi mabaya.

Itoshe kusema wabongo hatuwezi fuga hawa mbwa wakubwa wakubwa wakali, ni process.
MAFUNZO MAFUNZO MAZOEZI MAZOEZI, SOCIALIZATION kama huyawezi haya achana na mbwa
 
Kuna matunzo ya kuwapa(tokea wakiwa wadogo) sema wabongo hatufatilii ni ujuzi kabisa unaitwa dog handling, hapo hatujazungumzia mafunzo(training).

Ukiona mbwa anasumbua, kapata malezi mabaya.

Itoshe kusema wabongo hatuwezi fuga hawa mbwa wakubwa wakubwa wakali, ni process.
Hata huko walikotokea wanaacha maafa mengi tu kila kukicha, info is free online.
Sio kila kitu wabongo this wabongo that
 
Back
Top Bottom