Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

bahati ni kwamba meno ya bull dog hayana ncha kali kama german sherfad au rottweiler,meno yao yapo kama punje za mahindi,,lakini kiuhalisia bull dog hawana akili wala kumbukumbu nzuri,na ni wazito sana wakati kuwafundisha,ni mbwa niliobahatika kuwafundisha lakini kichwani hamna ki2 tofauti na german shrfad
Eti kichwani hamna kitu 😂
Empty set🤣
 
Ukifuga mbwa unatakiwa umzoeshe watu tokea akiwa mdogo, na uwe unampa mazoezi ya kutosha, haswa mbwa wakubwa wenye nguvu.

Watu wanakariri kufuga mbwa wa kizungu fashion, kama unamnunua ili akae bandani atoke usiku tu bora uache.
Sasa anakuzoea halafu anapoteza kumbukumbu nawe ndio unajikuta unampigia mzluzi Kama hujashangaa kaondoka na mdomo wako
 
Daah watu wanafuga Simba bila kujua hao sio mbwa wa kawaida na wana nguvu mno niliwahi kuona jamaa alimfunga na mnyororo wa kawaida kwenye pick up yake nyuma akamwacha baadae yule Bulldog alitoka kama ajafungwa kitu na kuruka nje ya gari bahati nzuri aliemfata kumjeruhi alimchapa risasi bila kujiuliza ilikua maeneo ya Centurion na muhuni aliondoka kama hakuna tukio lililotokea..
Eti Simba😂
 
Wazoefu wa mifugo wanasema

Kuwa mifugo kama hiyo ina mda maalumu wa kufugwa yaani ana mda maalumu wa kuwa naye hapo nyumbani kwako na akizidi huo mda anakuwa ana chukua tabia za kibinaadamu yaani anakuwa na wivu na watu wanaomfuga anakuwa na wivu kwenye chakula anataka ale kama anayemfuga au zaidi ya anayemfuga anakuwa na wivu upande wa mapenzi kama utakuwa na mpenzi wako na mapenzi yenu yatakuwa moto moto anakuwa anakuonea wivu yaani atatamani huyo mpenzi wako mke/mme wako awe naye yeye yote hayo ni kupita mda wa kuwa hapo nyumbani na wewe/nyie , mbwa wowote wale wawe wamapambo au wale wa ulinzi hali hiyo inawakuta

Wale wa mapambo huwa wanasusa na kuamua kuondoka kwenye nyumba’ mfano kama umeshawahi kusikia mbwa anatafutwa na picha watu wanaiweka mtandaoni wanaweka na ofa kwa atayempata atapewa kiasi fulani

Wale wa ulinzi uwa wanajeruhi na kuleta madhara kama hivyo

Hii ni kwa wanyama wote wanaokaribishwa nyumbani kama ulinzi au mapambo,chui,simba,mbwa,paka yeyote yule hata awe mamba ilimradi amekaribishwa nyumbani awe rafiki inatakiwa elimu itolewe kama kuna mda fulani ukishapita wapelekwe pahala pa uangalizi wa taifa wao watajua wawafanye nini? Kwani haitakiwi kuishi naye nyumbani tena

Poleni sanaa majeruhi M/Mungu atawapa na nafuu
 
Asee, Pole sana kwa familia.
Huyu sio Bulldog na sio pure Pitbull.

Huyu nahisi amecross Pitbull na Boerboel.
Pitbull ni mbwa wa kufuga kwa upendo mkubwa mno, na hautakiwi kumfanyisha aggressive training yoyote. Yeye anafundishwa obedience tu.

Ukimfanya kama mbwa wa Ulinzi niamini mimi utalia na kusaga na meno especially ukiwa na familia na watoto wadogo.

All in all kibongo bongo hatujui kuwafuga hawa jamaa, My take ni kuacha kufuga hii jamii ya mbwa.

Hao ni special kwa kuwinda wale Wild Boar [Nguruwe Pori] and they are designed to bite and to kill na sio kujeruhi tu.
Eti utalia na kusaga meno🤣
 
bahati ni kwamba meno ya bull dog hayana ncha kali kama german sherfad au rottweiler,meno yao yapo kama punje za mahindi,,lakini kiuhalisia bull dog hawana akili wala kumbukumbu nzuri,na ni wazito sana wakati kuwafundisha,ni mbwa niliobahatika kuwafundisha lakini kichwani hamna ki2 tofauti na german shrfad
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2023 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985

Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

C & P FROM X
- Pdizaina05
Badili mwaka weka 2024
 
Back
Top Bottom