Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Hilo limbwa ni pitbull, haya mambwa hajawahi kua na akili timamu. Inaonekana jamaa alishikishwa kwa ni juavyo mimi bulldog ana miguu mifup na mkia mfupi. Sasa inaonekana jamaa aliangalia uso tu akajua ni bulldog kumbe ni pitbull jibwa wehu lilo pigwa marufuku kufugwa na nchi zaidi ya 50 ulimwenguni.
[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2023 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985

Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

C & P FROM X
- Pdizaina05
Kunju yupi huyu mfanya kazi wa GGML au?
 
Afrika ni zero brain,badala wapige risasi za usingizi kisha wachunguze kwa nini wamebadilika ghafla-wao wanaua.
Waliosema akili ni mali hawakubahatisha-kwa kweli.
Nadhani wewe ndio hizo akili hauna
Halafu baada ha hapo wanawapeleka wapi? Kwako eeh?

Mnyama akishakula damu ya binadamu it must die..
 
Hata kama ilifanyika maabara pepo akiona upenyo tu hutinga ndani ya bongo na kuuthibiti.
Sijasema kwamba mapepo huvamia bulldog pekee, mapepo yanaweza kuvamia mbwa koko, binadamu, nguruwe nk.
Nachokisema hapa sijakitoa kwa mchungaji bali nimechunguza mwenyewe kwa kusoma vitabu mbalimbali ikiwemo Biblia.
Kwani hiyo rabies inapokuja akili za mbwa huhamia wapi?
Pepo ndio kitu gani we mzee,achana na habari za kusadikika
 
Back
Top Bottom