Mch. Kimaro wa KKKT niliziona Mbio zake nikajua mwisho hautokuwa mzuri

Inatafunwa na Nani?. Kanisa gani? Shilingi gapi? Unapotoa allegations toa na evidence. Usiwe kana Mchungaji Kimaro.
Inatafunwa na viongozi wa kabisa na Miata wachungaji na mapadre
 
Wakristo wa kileo (kisasa) hawapendi kuambiwa ukweli
 
Kimaro ameongea kama illiterate person.
Huwezi ku ganeralize kauli bila kufanya utafiti.

"Waislamu ni waaminifu kupita Wakristo"
Ni kauli ya kipumbavu kabisa.

Inamaana hata yeye sio mwaminifu.
Na kanijumuisha hata na mimi ambaye hanijui tabia yangu.

Kimaro lazima atuombe radhi Wakristo kwa kauli yake hii.

Na ajiuzulu Uchungaji maana kashindwa kazi ya utumishi.
Asilimu ajifunze kuwa Imamu wa Kiislamu.
 
Mpaka mwisho wa andiko sijaona walau mfano wa kuburi na majivuno... Au uzi utaendelea baadae mkuu?
 
Acheni unabii jamani.

Inawezekana labda ni taaluma yangu imenifanya kuwa hivi, kwasababu hadi sasa siko upande wa viongozi wa KKKT wala upande wa Mch. Kimaro.

Moja ya kanuni za haki ya asili inasema, huwezi kuhukumu mtu bila kumsikiliza.

Mm nitauhukumu Uongozi wa Kanisa au Mch. Kimaro baada ya kusikiliza pande zote mbili kwa kina tena maelezo yao yakiambatana na vielelezo (kama vipo).

Acheni kuendeshwa na mihemko; mtatenda dhambi bure.
 
Kwanini mnataka kuficha WIVU na CHUKI kunwa mliyonayo juu ya binadamu wenzenu kwa kuleta visingizio vya maandiko, acheni wivu na acheni chuki, kuna haja gani sasa ya kufanya kazi kwa bidii kama hakuna nafasi ya kujimwambafai?!

Yaani nichekee chooni kisa naogopa wachawi kama nyie?!
 
Natamani mtafute mtu asiye na Dini ( e.g mchina) ambaye afanye research bila ya hisia ya kidini ( islam or Christian)...
Achague mada / topic aliyo ileta mchungu Kimaro..

Nina uhakika atakuja na conclusion ya KIMARO..

Yako mambo kubisha green ni blue ni kupoteza muda...

Kuna dini hata siku moja haikubali hoja bali hisia tu na matamanio..
 
Halafu hao ambao sio waaminifu anataka sadaka zao!!!!!
 
Mchungaji alianza kutoka nje ya mstari… Kanisa liligeuka kijiwe cha udaku mipasho kusutwa kusutana…Ndio maana aliweza kuitia najisi madhabahu ya Mungu kufananisha Wakristu na Waislamu…. Uaminifu ndio alinganishe imani za watu? Uongo uaminifu uchawi upendo etc ni tabia ya mtu
Alitegemea Kanisa kama Kanisa likae kimya?

Ajirebishe ……
Kanisa ni nyumba za ibada na kuabudu sio porojo majungu na ufitinishaji
Masikio yalianza kuzidi kichwa..
 
Kwani alichoongea ni uongo?
 
Mashehe tena? mbona zipo wazi hujazitafuta tu. Hakuna aliye salama dunia hii.
Sasa mtu anawake wanne,kapungukiwa na nini?utamfananisha padir anayesalisha huku anatizamana na warembo baadhi yao wamevaa nguo fupi?tuwe wakweli jamani
 
Hivi unajua Vibaka, Panyaroad, Kesi za Ulawiti, Ubakaji na Mauaji ukipata takwimu Waislamu ndio wamejaza mahabusu zetu
Na huko mikoani?usiongee hivyo wakati unajua Dar asilimia kubwa ya wenyeji ni waisilamu
 
Lucifer alitaka kuwa kama Mungu. Ila pia Lucifer alidhani ananguvu kuliko Mungu. Kimaro ametenda jambo lisilo faa mbele ya Kristo na wakristo na amefanya akijiamini hakuna wakumgusa tena hakuna kama yeye kumbe Mungu anawatu wengi. Sina wivu na mtumishi kwa sababu hatuwezi sote kuwa watumishi. Ila dhihaka na mipasho yake nje ya kumtaja Yesu imemshusha japo Mungu ni wetu sote ajuwa vile atafanya. Ila ameudhalilisha umma wa Wakristo ina maana mafanikio ya wakristo ni wizi God have a mercy on us. Amen
 
Wale maustaadhi wanaolawiti watoto madrasa ni Wakristo!!!??
Huko (Kwenye Uislam) ndipo uchafu ulipoanzia.
 
Ndiyo alitakiwa awabadilishe siyo kuwakebehi. Kukiri maana yake kashindwa kazi ya Mungu ya kuwabadilisha hao uliowataja!!!!
Amewakemea na kuwakemea ni bora zaidi kuliko kuwachekea kinafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…