Mch. Kimaro wa KKKT niliziona Mbio zake nikajua mwisho hautokuwa mzuri

Mbona inajulikana wazi kabisa kuwa raia wa Kenya ni wachapakazi kuliko raia wa Tanzania ambao ni wavivu.
Sasa mtu akiusema huu ukweli ndio asusiwe na kusimamishwa kazi kweli?Mbona haiingii akilini kabisa,pengine walikuwa wanamvizia tangu zamani kwa mambo yao mengine wakatumia hii kama sababu tu
 
Kwa hiyo wewe ulitaka mchungaji kabla ya kufanya mahubiri afanye sensa kwanza kisha ndio aje kuwahubiria waumini wake si ndio?Yaani unataka kusema mchungaji hatakiwi kusema ukweli ambao utawauma waumini wake hadi aje na vitabu vya research ila akisema mambo ya kuwasifia waumini hakuna haja ya vitabu vya research?Mambo ya dini hayaendi hivyo ndugu zangu acheni kuchanganya dini,usomi, siasa,na ujuaji wa mambo ya kidunia hivyo vitu kila kimoja kina mahala kwake
 
Acheni kumuingizia Yesu Kristo kwenye makosa yenu. Mchungaji mzima unakiri kwamba vijana wa kikiristo sio waaminifu na kwenye project zako umeajiri vijana wa kiislamu. Ndio maana mimi huwa nasema yule kimaro sio mchungaji ni motivational speaker.
Tatizo lenu mmezoea kudanganywa jibu hoja kwa hoja sio kwa mtizamo nimeuliza mbona Yesu alifanya hivyo pia jibu hoja.
 
Wewe una amini maneno ya Kimaro ?
Tuanzie hapo kwanza
 
Alichokisema Dr Kimaro kina ukweli, kuitwa Mkristo sio wote wa Kristo, wapo wengi wanaojiita Wakristo ila hawana sifa za Kikristo.
Wapo Wakristo sio waaminifu kabisa hawa ni wale wanaojiita Wakristo ila tabia zao hazimpendezi Kristo, kwa sababu wapo kanisani ila tabia zao ni mbaya.
Hata kwenye biblia wapo watu walisifiwa wasiomwamini Yesu Kristo, hii ikionyesha kuwa kuna kitu kizuri kilionekana kwao.
"Yule bwana akamsifu wakili asiyemwaminifu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru", Luka 16:8 SRUV.
Labda useme kiburi kingine ila sio hichi aliyoyasema haya maneno.
 
Awamu za Marais Waislamu hakuna Ufisadi ?
Ndivyo unavyo fikiri
 
Siku zote usiwe mwepesi wa kuropoka na kulaumu.Mm ni Mkristo na kwa neema ya Mungu najitahidi kuishi Ukristo japo najua pia mm siobmkamilifu lakini acha niseme ukweli Wapo Wakristo wanaofanana na alosema mch.Kimaro.Kwa hiyo kasema kweli na kama Kuna ukweli Mungu atamtetea.
 
Sijaona shida ya mchungaji hapo ninachoona ni ubinafsi na kujiona bora kuliko dini nyingine kwani kumsifia mtoto wa mama mdogo ni dhambi kisa tu hamjazaliwa tumbo moja.

Mungu hana ubaguzi nyie mmeshinda kubaguana. Mungu atupe macho ya rohoni
 
Farisayo mnafiki mkubwa
 
Acha wivu wa kike fanya kazi zako. Imani hailazimishwii mtu
 
Rose Mhando aliimba
Uniondolee majivuno
Komesha kiburi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…