Yeye na wewe mko ktk ulimwengu tofauti. Huwezi kuelewa haya. Nuru na giza haviwezi kupatana. Wewe ni sehemu ya giza (ukosefu wa uelewa na ufahamu). Pole sana..
Unaweza kuwa wewe ndiwe hasa mgonjwa wa akili huku ukijidhania kuwa una hekima na nguvu kumbe ni kopo tupu kichwani..
Watu kama wewe walikuwepo hata kule Korintho ya kale.
Lakini Mtume Paulo katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho, anakupa hekima na maarifa ili upanue ufahamu wako ili uepuke hukumu
"....
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;..."
1 Kor 1:27-28 SUV
Wewe unamwona Mbarikiwa kama
mnyonge au
dhaifu na
kichaa, it's ok....
Lakini Mungu
hutumia wanyonge,
dhaifu na waonekanao kwa macho ya kibinadamu kama
vichaa ili
awaaibishe wenye hekima ya kibinadamu, wenye nguvu za kibinadamu na pia naaam,
avibatilishe vilivyoko..
Wakati wa kuaibika wajionao wana hekima na nguvu, ni huu umekwisha kuwadia...
Wakati wa Kila kitu kilichopo kubadilishwa, ni huu umekwishakuwadia..
Hili ndilo NENO LA BWANA...