Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,566
Tujikumbushe kidogo!
Wakati wa spika Sitta,serikali ilisimamiwa ipasavyo na bunge!Ilipelekea mijadala mingi kupenya bungeni na kujadiliwa!Viongozi wa CCM walimlalamikia Sitta kwa kuiruhusu mijadala bungeni ambayo inaishambulia serikali!Sitta hakusikia na akaendelea kulisimamia Bunge kwa kufuata kanuni na taratibu zake.
Ilipokuja wakati wa kuchukua form tena ili kugombea uspika,Sitta alionesha nia ya kugombea tena!Akafanyiwa zengwe na wanaCCM ili asishike kiti tena,ikaletwa kauli ya ujanja ujanja ya kwamba sasa ni zamu ya mwanamke kuwa spika,Anna Makinda akashika usukani.
Hesabu za CCM kwa mara nyingine zikawa hazijaenda sawa kama walivyotarajia,bado bunge likawa linaibua hoja zenye mashiko kuiwajibisha serikali na mijadala hiyo ikawa inapenya vizuri tu bila zile "toa nje".
CCM wakaendelea kujipanga,wakaona Ndugai angeweza kuwasaidia maana wakati akiwa naibu alionesha viashiria vya ubabe dhidi ya wapinzani wakati Spika akiwa hayupo.
Ndugai akapewa Uspika.
Ili kuipanga safu vizuri,Tulia akapenyezwa kwa namna ambayo watu wengi walibaki na mshangao!Maana alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu,na kimaadili hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote!Ghafla akapachikwa ubunge wa kuteuliwa na kupewa kugombea unaibu spika ambapo alipita.
Safu ya kuling'oa meno bunge ikawa imekamilika.
Haya tunayoona sasa ni matokeo ya mchakato mrefu sana ndani ya CCM,ila kilichoongezeka awamu hii ni kuwa mamlaka iliyojichimbia chini zaidi imeonesha dhamira ya dhati kulishika Bunge.