Mchanganuo tozo za LUKU kuanzia August 20-2021

Ndio maana watu wakapendekeza iitwe kodi ya luku/ umeme/ meter kwa sababu inatozwa kwa meter sio jengo.

Jengo lenye meter 2 litatozwa 2,000 kwa mwezi wakati kimsingi kodi ya jengo inatakiwa iwe 1,000/- kwa jengo.
Kwa nini jengo moja ulete mita 2? Utavuta nyaya ngapi toka nguzo kuu kama unataka mita 6?
 
Sasa nyumba yenye luku zaidi ya moja itakuwake?
Jana nilimsikia mmoja wa watu wa TRA akisema,"mmiliki wa nyumba yenye wapangaji tu na mwenye nyumba haishi hapo anaweza kwenda Tanesco na kuainishi mita zinazotakiwakukatwa kodi "
 
Mwenye nyumba wa kuwarudishia hio pesa labda ni kwa wale ma Don ila wapangaji wa Manzese, Vingunguti na Kiwalani mjiandae kisaikolojiaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Kwahio ishu ni kuwapata wenye nyumba kumbeπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… hapa kimeeleweka
 
Hapa inabidi waongeze Kodi kwa ajiri ya kutunisha mfuko/bodi ya mikopo Ili vijana wetu wawe na uhakika wa kupata mikopo ya Elimu ya juu
Hio Elimu ya juu inawasaidia nini zaidi ya kwenda kugombania kazi nafasi 5 watu elfu 20
 
Tatizo sio kutozwa kodi, zinatumikaje?
Wakiendelea kuzifuja kwa mambo yasiyo na tija, vizazi vijavyo watatushangaa sana.
matumizi ya kodi zetu yataonekana wazi, tutaona mabadiliko ya barabara, maji, elimu, matundu ya vyooo, zahanati, dawa hospitalini, n.k
 
Kuna wapumbavu wanaamini kutokulipa kodi au kulipa kodi ndogo zaidi ndio maendeleo kwa wananchi...hamna nchibiliyoendelea ambayo wananchi wake wanalipa kodi ndogo...hamna, na hayo maendeleo yanachangiwa ktk hizi tozo...
Ila pia hamna nchi ilioendelea kwa kukumbatia katiba ya kipuuzi kama tulionayo ambayo wanasiasa wanajilimbikizia mali kifisadi na kuachiliwa huru tu wazurure mitaani!

Hakutakuwa na maendeleo kama hio mitozo itakuwa haisimamiwi vilivyo na ikaenda kufanya yale yaliokusudiwa. Kama watu watagawana hizo tozo kwenye sandarusi na katiba hii tulionayo kuna kipi mtakifanya πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
matumizi ya kodi zetu yataonekana wazi, tutaona mabadiliko ya barabara, maji, elimu, matundu ya vyooo, zahanati, dawa hospitalini, n.k
Una uhakika gani katika hili? Je, miaka yote hio huko nyuma ambapo serikali ilikuwa ikifanya majukumu yake bila tozo mbona majengo yalijengwa mengi tu? Shule zilijengwa, hospitali zilijengwa why today?
 
Kuna mahali katiba imeruhusu watu kujilbikizia?
Katiba mpya ni chaka tu linatimiwa wala sio mwarobaini wa changamoto zilizopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…