Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Yani wakulima ni watu fulani makaksi sana

Wao wanatuuzia mchele kwa bei ya kiwanja utafikiri sio watanzania wenzetu, saizi wanaona kuna plan B inaletwa wanaanza kulialia

Tena mi nasema serikali ikiwezekana mnunue na maharage huko huko nje, hawa wakulima wetu inaonekana mazao yao walikuwa wanatumia maziwa kumwagilia na ndio maana yana bei sana.
 
Kwa hiyo kwako bora tuanze kula makapi ya bei rahisi, umenikumbusha wale sangara na sato wa ziwa Victoria waliokuwa wakipandishwa ndege kwenda ulaya, huku wabongo tunakula mapanki, hakika tumeshazoeshwa kula mitumba, afya kwetu sio issue tena, muhimu tumbo lijae!.
Hayo makapi unakula kwa hiari yako kulingana na bajeti iliyopo mfukoni mwako

Hauletewi kama mfungwa gerezani kwamba huna option

Mchele kilo 5 huku si kukomoana mzee?

BTW mchele wa 2900 unaouzwa huku mitaani asilimia kubwa ni makapi

Sasa si bora hayo makapi watu wayale kwa 1500
 
Huo mchele utaingia lini nchini mbona kama wanachelewa kuleta, kwasasa kula wali imekuwa kama anasa kwa wananchi, naombeni serikali ifanye haraka, na wale walioficha mchele wabaki nao
 
Mtajua wenyewe. Nyinyi mnaona sawa kutuuzia kilo ya mchele kwa shilingi 3600! Si mlifurahia soko kufunguliwa, na hivyo kuuza chakula chenu nje ya nchi kwa bei mnayotaka!!

Sasa inakuwaje mnaanza tena kupagawa mchele kuingizwa nchini? Si ndiyo soko huria lenyewe hili!!! Nyinyi nendeni mkauze mchele wenu nje ya nchi kwa bei kubwa, na sisi tutanunua huo mchele wa kutoka nje kwa bei nafuu.

Ni wakati sasa wa kila mtu kushinda mechi zake. Msianze kulia lia hapa.
Upo sahihi kabisa nakuunga mkono mpaka mguu, wakauze michele yao huko kenya na sisi tutanunua michele ya kutoka huko Thailand.
 
"Msije kutuletea tena ule wa Thailand Nusu kilo manakula watu 18 na unabaki kiporo cha chai"🙌.......pitia Account za Instagram na Facebook za ITV zilizopost hii taarifa usome maoni utajifunza vitu vingi sana. hiyo ni moja ya comment
Waache kufanya figisu, hizo ni chama za wafanyabiashara wa mchele, hule mchele wa thailand upo gud tu hauna kelele wala ngebe.
 
Aisee hii habari njema , Sana , wakulima Uchwara wanatuuzia mchele mbovu kwa 4000 na maharage mabovu 4000


Sasa waache kulalamika tamaa zimewaponza
 
Mshapaniki tayari! Mtashusha tu bei, mtake msitake. Hamuwezi kutuuzia mchele kilo kwa shilingi 3600!! Hui ni uhujumu uchumi.

Na aliyeagiza hizo tani elfu 90, nampa pongezi za dhati. Na naamini atakuwa siyo yule kilaza Hussein Bashe.
Mbona ameagiza kidogo angeongeza na kufika tani laki mbili.
 
Mwaka huu nilitaka kulima mpunga ila kwa sera hii ya kuagiza nje - shastuka.
 
"Msije kutuletea tena ule wa Thailand Nusu kilo manakula watu 18 na unabaki kiporo cha chai"[emoji119].......pitia Account za Instagram na Facebook za ITV zilizopost hii taarifa usome maoni utajifunza vitu vingi sana. hiyo ni moja ya comment
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Hapa tatizo sio wakulima,tunawaonea sana wakulima. Tatizo ni hawa watu wa kati..madalali na walanguzi, tena humo humo wamo hadi wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa.
Kinacho wagharimu wakulima wapo kimya hawasemi ukweli kama hakuna faida wanazopata

Serikali inawaangalia wakulima wakubwa wakubwa tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakulima ndio wameamua kujidharau,bila kuwa na chombo Chao Cha sauti wataisoma namba.

Mwaka huu mchele shambani tutanunua 20,000 Hadi 25,000 na hapo ndio mkulima atakoma
Kapange upya hoja zako ndipo uandike. Sasa hiyo Bei uliyoweka ni kwa Kilo, Gram au Tonne? It's a vague comment
 
Back
Top Bottom