Huyu waziri wa nchi bwana Mchengerwa kwa mapovu anayotoa huenda wadau wamebinya penyewe.
Sasa anasema ikibidi kutoa uhai wake ili kulinda amani ya nchi basi atafanya hivyo na yupo tayari.
Kwa miaka ya karibuni huenda huyu ndiye waziri wa kwanza wa TAMISEMI akiongelea mambo ya ulinzi wa nchi. Sijawahi kuona mwingine!
Anaongea hivyo kwa kivuli cha wakuu wa wilaya na mikoa akisema wapo chini yake. Sawa lakini kuna wizara mahususi. Yeye ajikite kwenye ishu za miundombinu ambapo ndiyo kazi mama ya hiyo wizara.
Kutwa ni mambo ya amani amani amani...Au ndo kuteteana? Huyu waziri ana dhambi kubwa za ubaguzi kwa watu wa bara kwenye vyeo. Hapo tunamhifadhi.
Ndugu watatoa kila aina ya mlio safari hii.