Pre GE2025 Mchengerwa kutoa Milioni 60 kwa ajiri ya ujenzi wa Studio ya Muziki! Wana Rufiji hiki ndicho mmemuagiza mbunge wenu awaletee?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duuh Rufiji gani hiyo yenye Barabara ya kiwango cha juu?
 
Kama wewe si mwanarufiji tulia please acha kuwa Malaya wa majimbo 🤣
 
Vipaumbele vyenu ni kukata viuno mkuu? amkeni amkeni mkuu
Vijana wamepata ajira, vijana wameenda shule, hosp na vituo vya afya vya kutosha na sasa Kuna mpango wa kujenga hosp kubwa zaidi

IKWIRIRI inaenda kuwa mamlaka ya mji wa rufiji, barabara ya lam inajengwa ambayo ilipigiwa kelele miaka nenda rejea

Shule zipo za kutosha kuanzia English medium mpam kidato cha Sita za wavulana kwa wasichana

Viwanda vya kuchakata sukari nk

Veta ipo vijana wanapata elimu ya ufundi

Kituo cha radio watu wanapata taarifa muhimu kuhusu nchi yao pamoja na Burdani

Na mambo kedekede yanakuja

Karibu rufiji mkuu
 
Halafu nani aajiriwe kwenye hivyo viwanda?Watatoka watu wa Kigoma,Tabora na Iringa kuajiriwa.Wewe waache wapate the real musique studio.😂😂
 
Mkuu hivi Rufiji wenyeji huwa ni kabila gani? nimesoma hapo Dar 2013-2016 sikuwahi kusikia mtu chuoni kwetu anatoka Rufiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…