Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na bajaji wa Jiji la Dar es Salaam.
Mhe. Mchengerwa amewahimiza Wakuu wa Mikoa nchini nchi nzima kusimamia uandaaji wa mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa kuwatambua madereva Bodaboda na bajaji kama ilivyofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuwalinda na kuwathamini maafisa usafirishaji hao maarufu kama madereva bodaboda na bajaji, kama ambavyo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza.
Sanjari na hilo, Mchengerwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuweka utaratibu utakaowawezesha maafisa usafirishaji hao kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri ambao unawalenga wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Waziri Mchengerwa ameelekeza mchakato wa kutoa mikopo ya asilimia 10 uanze mara moja ndani ya mwezi huu wa Julai, 2024 ili walengwa wanufaike na mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali ya Awamu ya Sita.