Pre GE2025 Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa wote simamieni mfumo wa Kidijitali wa kuwatambua Madereva Bodaboda na Bajaji

Pre GE2025 Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa wote simamieni mfumo wa Kidijitali wa kuwatambua Madereva Bodaboda na Bajaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinsta.app_449520229_18333825907193701_829146848693952830_n_1024.jpg
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha wanajenga vituo vya bodaboda vya kupaki pikipiki vyenye uwezo wa kuzuia jua na kuwakinga na mvua wanaposubiri wateja.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na bajaji wa Jiji la Dar es Salaam.

“Ninaelekeza vituo hivi vijengwe mara moja ili kuwasaidia bodaboda kupata eneo salama la kupaki wakati wakisubiria wateja,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewahimiza Wakuu wa Mikoa nchini nchi nzima kusimamia uandaaji wa mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa kuwatambua madereva Bodaboda na bajaji kama ilivyofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuwalinda na kuwathamini maafisa usafirishaji hao maarufu kama madereva bodaboda na bajaji, kama ambavyo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza.

Sanjari na hilo, Mchengerwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuweka utaratibu utakaowawezesha maafisa usafirishaji hao kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri ambao unawalenga wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Snapinsta.app_449696354_18333825886193701_909536788201318377_n_1024.jpg

Snapinsta.app_449696731_18333825937193701_7062424550124851990_n_1024.jpg
“Wakurugenzi wa halmashauri wekeni utaratibu mahususi utakaowawezesha maafisa usafirishaji kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri zenu kwa kundi la wanawake, vijana na wenye ulemavu,” Mhe. Mchengerwa amehimiza.

Waziri Mchengerwa ameelekeza mchakato wa kutoa mikopo ya asilimia 10 uanze mara moja ndani ya mwezi huu wa Julai, 2024 ili walengwa wanufaike na mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
 
Uchaguzi ,uchaguzi uchaguzi ,kura kwa mama mkwe za urais lazima zipatikane kwawingi ,toka kwa bodaboda
 
Back
Top Bottom