DUBULIHASA
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 6,138
- 11,989
Kweli mkuu japo sio lazima kwake akusaidie lakini kibinadamu inaumiza sana... ndo maana tunaambiwa unapotoa msaada usi-expect chochote kwa uliyemsaidia.. unakuta kweli huku expert chochote lakini unakuta imefika stage kwenye maisha umekosa hata buku 2000 ununue dagaa za watoto wale ila mshakaji akashindwa kukusev Kweli.πππ It's hurting
Ya zamani!Watoto wako wanatumia majina yako mapya au ya zamani?
sele mwalimu kosakosa ana miaka isiyopungua 34Wewe hujui kuna umri wa uwanjani na kuna umri wa mtaani ni vitu viwili tofauti unaweza kuamini kuwa sele gomez anamiaka 20 kweli? Hahahaha
Hapa ana owezo wa kujitetea yeye sio wewe hata kama majina yanafanaNilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.
Duchu rudisha jinaKitu kingine kilichochochea wewe kutaka kurudishiwa jina lako ni kumuona mwenzako yupo Simba.
Angekua hana kazi ya kueleweka hata usingejisumbua kudai jina lako.
Hakuna kesi ya kwenda polisi hapa labda kama umejiandaa na wewe kupoteza.
Sawa SelemaniDuchu rudisha jina
Huwezi kumhukumu kwa hisia zako .Mi naona kuna ishara za wivu na tamaa , ulimpa jina mwenyewe hukumpa kipaji, unadai unaathirika embu elezea vizuri kama sio ndugu zako wanataka mgao na wao⦠kama mwanao malizana nae kama mlivyoanza acha Tamaa
Aliyezingua ni duchu,mtoa mada hana cha kupoteza kama ilivyo kwa Duchu.Mwamba kazingua huwezi mjibu hivyo rafiki yako mwamba alitaka chochote kitu kwenye swala la kubadili jina kurudi ndio mtiti ulipo sasa kesi kule NIDA na sheria iko wazi kutoa taarifa za uongo kuna faini na kufungwa jera cha msingi wayamalize wao kwa wao wasifike huko maana wote wamekiuka sheria
Tusaidie picha ya huyo manziIla huyu Duchu ana manzi mkali laana. Halafu naona msimu huu kaanza vizuri
Wayamalize....mtoa mada ana haki maana ni stakeholder kwenye mafanikio ya duchuSawa Selemani
Kwa mtaji huu, halafu CCM wakichakachua uchaguzi tunalalamika?Ukisoma vizuri itakuwa waliahidiana posho jamaa hakutoa posho.
All in all kama umewahi kucheza soka ligi za wilaya Kununua majina ni issue za kawaida.
Aisee kuna watu wanaishi na siri nzito mioyoni mwao! Kwa ushahidi huu, nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kama umeleta taarifa ya uongo! Sema tu kuna makosaa umefanya kutokana na kukosa elimu ya uraia.Naitwa David Frank Kameta, baada ya kupata wakati mgumu muda mrefu ikiwepo kusalitiwa na mtu ambaye nilimuamini, sasa naona ni bora Dunia ijue kinachoendelea. Hapa nazungumzia usaliti wa rafiki yangu Emmanuel Robert Kakoti jina lake maarufu wengi mnalijua, kwa sasa ni mchezaji maarufu katika klabu kubwa katika Ligi Kuu Bara.
Alichukua jina langu kwa makubaliano maalum kuwa atalitumia muda mfupi lakini amenigeuka na kuendelea kulitumia kwa miaka mingi, hataki kurejea katika jina lake halisi huku akinisababishia hasara nyingi na mzozo katika familia yangu.
Stori yetu ipo hiviβ¦
Tuliishi pamoja Mbeya, tulisoma wote ingawa alikuwa mbele yangu darasani, mimi umri wangu ni miaka 32 (nilizaliwa 1994), yeye mwenzangu alianza kucheza mpira tukiwa wadogo, hayo hayakuwa mambo yangu.
Mwaka 2017 au 2018 (sikumbuki vizuri), Emmanuel akiwa timu ya Mbeya City alionyesha utovu wa nidhamu, uongozi ukamfungia usajili pamoja na kufungiwa kutumia majina yake yote halisi kwenye soka. Hiyo ilimfanya aonekane kama amefutwa kwenye Ulimwengu wa soka.
View attachment 3657241
Kikosi cha Mbeya City cha Msimu wa 2017/2018 ambacho Emmanuel Robert Kakoti alikuwepo (jina la nne kutoka juu).
Kuna siku ilikuwa deadline ya usajili, Emmanuel aliniomba, "Mwanangu, usajili unafungwa leo na nimekosa nafasi, naomba nisaidie cheti chako cha kuzaliwa nitumie kwenda Mbeya Kwanza. Nikianza tu kucheza, nitabadilisha jina kwenye leseni na kurudisha jina langu halisi."
View attachment 3657249Sababu ya urafiki na huruma, nilimpa cheti changu, akafanikiwa kusajiliwa Mbeya Kwanza kwa jina langu la David Frank Kameta. Aliendelea na maisha yake ya soka katika timu ya Lipuli ya Iringa, lakini ilikuwa ni kinyume na ahadi yetu, hakubadilisha jina hilo. Nilimsisitiza kuwa anatakiwa kurejea katika jina lake halisi lakini aligoma.
View attachment 3657251
View attachment 3657252
Picha enzi zetu tukiwa washkaji
Aliposajiliwa katika timu yake ya sasa ya Kariakoo, akaanza kunikwepa, akawa ananipa majibu ya mkato. Huku nyuma mimi nikaingia katika mgogoro wa kifamilia wakiniambia nimeuza jina.
Baada ya msiba wa mzee wangu, familia ilikaa kikao na kunisema sana, nilipompigia simu Emmanuel mbele ya familia hakupokea. Nilituma ujumbe kumtaka ache kutumia jina langu, alinijibu kwa dharau: "Fata sheria yoyote, mimi siachi kulitumia."
Nilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.
Hali hiyo imeniletea athari kubwa sana kiakili na kisheria kwani jamii inaamini niliuza utambulisho wangu na kuna fursa kadhaa nimezikosa kwa sababu yake, nimeamua kuandika hapa baada ya kuona uungwana wangu umeniponza na mtu ananiletea dharau.
Hawezi mkuu,Hapa ana owezo wa kujitetea yeye sio wewe hata kama majina yanafana
Mbona Sospeter Bajana aliyekuwa akitumia jina la Bryson Rafael hakufungwa wala kupotezwa!! Aliendelea kucheza Azam Fc na msimu uliopita akajiunga na JKT Tanzania kama sijakosea.Basi ndo kishamlamba tena kwa ushamba wake anaweka vyeti tin mpaka na picha kabisa kama anamtumia babaake kudadadeki kumbe analichonga kaburi lake mwenyewe ngoja wanayanga waamke walivalie njuga ataelewa athari zake soon, maana sababu inaonekana alitaka amfanye mwenzie kitega uchumi mwenzake amemchomolea may be kwa kuchoka kwa vizinga
Na ndiyo kawaida yao. Nilishawahi kuwa kocha wa timu za vijana enzi hizo kijijini kwangu! Ilikuwa ni kawaida kijana mwenye umri wa miaka 22 kumjumuisha kwenye timu ya U17.Duhh kapunguza miaka 7ππ
AiseeππNa ndiyo kawaida yao. Nilishawahi kuwa kocha wa timu za vijana enzi hizo kijijini kwangu! Ilikuwa ni kawaida kijana mwenye umri wa miaka 22 kumjumuisha kwenye timu ya U17.
Kwenye U20 tuliangalia zaidi wale wachezaji waliodumaa na ambao wanachelewa kuota ndevu! Hao ukimmwapata, wanapita moja kwa moja! πAiseeππ
Huu ugonjwa upo karibu afrika yote.Kwenye U20 tuliangalia zaidi wale wachezaji waliodumaa na ambao wanachelewa kuota ndevu! Hao ukimmwapata, wanapita moja kwa moja! π