KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Huyo Emmanuel kakoti alifungiwa asijighusishe na mpira maisha, hii ndo kesi kubwa
 
Huyo Emmanuel kakoti alifungiwa asijighusishe na mpira maisha, hii ndo kesi kubwa
Kama alikula hela za watu akalipe. Siamini kama kwa wakati kuna kosa lilisababisha mchezaji mwenye jina lake kufungiwa maisha na mamlaka za soka. Unaweza kukuta ni hao Mbeya City ndiyo walimpiga pini baada ya kugudundua dogo anataka kuwafanyia uhuni.
 
Kumepambazukaa
Nasemaje kumepambazukaaaa..

Hii inafanana na moja hv:

Nikiwa ofisini namalizia malizia, sms ya classmate wangu ambaye ni headmaster shule moja hv ikaingia inasomeka hv "hongera nimeona jina lako umepangiwa wilaya ya mafia"...kwa bahati sana nilikuwa na mh waziri mmoja hv, nikamuuliza mkeka umetoka? Na imekuaje ni mm? Akaniambia haujatoka vip? Nikamuonyesha sms na yeye akahamaki.. Nikamrudia huyo classmate nikamuulza vp? Akanijibu broo umepangiwa kama afsa uvuvi...aisee nikamuuliza uchumi na uvuvi wapi na wapi ijapo napenda mambo ya diving na marine tour...nilipata shida sana, nikamfuatilia yule dogo wa mafia, nikamtumia naul akaja nilipokuwa ...kweli majina yote yanafanana sana... Lakn yeye kazaliwa 2000...kwao ni wilaya nyngne na mm nyngne ijapo mkoa mmoja. nikamrudish

USHAURI: mtafute nje kwanza kabla ya mifumo ya kisheria myamalize, unless otherwise hata wewe kitakulamba kwa maana moja ama nyingine.
-labda siku umemtafuta ndo alikuwa amepgwa redcard, kwa sababu ya hasira akakujibu hvo.
 
Mawakili wa yanga wamewahi kushinda kesi ipi?
 
Kulingana na alichoandika, inaonyesha kabisa huyo mchezaji ni kweli aliazima jina (pengine kwa makubaliano ya malipo) halafu baada ya kujanjaruka akaona anaweza kuendelea kutumia jina lake bila madhara. Kama ulivyoelezea, majina matatu kufanana siyo issue kubwa. Kitu cha kuangalia ni: nakala za vyati vya kuzaliwa zinafanana data? (Hapa nahisi mchezaji alishagushi akapata cheti kipya kinachoendena na jina lake). All in all, kama wahusika wakiamua kutenda haki, ni rahisi sana kujua ukweli kwani wanaweza kufuatilia historia ya maisha yao tangu wakiwa wadogo.
 
Watu kibao wamerudia shule wakanunua majina ya watu na wakafanikiwa akina Mwinyigulu, Bashite, Andrea Kigwangwalombo, nk pia kesi yakonni kama Sospter Bajana na David Bryson Raphael ila kama ulimpa kwa roho moja muachie aendelee na maisha yake. Binadamu huwa hatuna shukrani hata mimi huyu Emmanuel Kakoti ndio nimemkumbuka sasa. Wema mtendee mbuzi unawez kumla mchuzi sio binadamu ukienda kushitaki utakula mvua wewe na yeye
 
Inaumiza sana sema watu hawajui..
 
Nenda Kwa mwanasheria atakwambia nini cha kufanya
 
Kuna vitu vina maswali mengi ya kujiuliza.

Mfano amefungiwa mtu au jina?

Kama kafungiwa mtu hata akibadili jina si ni mtu yule yule na safari hii ataonekana anatumia njia za uongo kuzunguka kifungo?

Hivi mtu unafungiwaje maisha? Unafutwaje kwenye ulimwengu wa mpira? Kwa kosa gani? Huko Ulaya watu hawafungiwi maisha na wana kesi nzito.

Na ni kivipi hakutumia njia nyepesi tu ya kubadili jina kisheria kama kutumia la mtu mwingine ilikua dawa nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…