KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sheria ipi inakuruhusu kumpa mtu jina lako kisha baadae akurudishie? Huoni kuwa wewe ni sehemu ya udanganyifu?

Unaumia kwa sababu mhusika anapata pesa ndefu. Pole lakini
Hawa wote ni waharifu,yaleyale ya DAB.Penal code inesema unaweza kufuungwa miaka Saba Kwa kosa Hilo.Bwana David Ulishiriki jinai hivyo wote ni waharifu
 
Wewe ni David Frank Kameta uliyezaliwa Mbeya 1994 Muuza Parachichi.
Na Huyo rafiki yako ni David Frank Kameta (DUCHU), Footbaler aliyezaliwa 2001
Watu wawili tofauti.
Mifumo inawatambua hivo japo kuna huo udanganyifu.
 
Tatizo namba moja unahisi ni haki yako jamaa kukupa pesa kama shukrani hapo ndiyo umefeli, kama uliamua kumsaidia na sio kusubiri shukrani kaa kimya tu.

Tatizo la pili jamaa amekua "star" hapo ndiyo unachanganyikiwa na haokoti simu zako.

La tatu hakuna athari yoyote ambayo wewe unaipata kwa jamaa kutumia jina lako, kwani majina mengi yanafanana.
 
Indoa hii post myamalize kiume.
 
1994
2001 ni watu wawili tofauti swali ni je cheti kilibadilishwa vipi iwe 2001 badala ya 1994?
Mtoa mada ameleta kesi ya identity theft.

Kaelezea kilichotokea. Mpaka picha kaweka kuthibitisha walikuwa marafiki.

Huo mwaka kubadilishwa si issue, issie hapa kuna case ya identity theft msione hakuna kesi.

Sasa, katika hiyo kesi ndiyo watachunguza vyote pamoja na huo mwaka umebadilishwaje.
 
Mtoa mada ameleta kesi ya identity theft.

Kaelezea kilichotokea. Mpaka picha kaweka kuthibitisha walikuwa marafiki.

Huo mwaka kubadilishwa si issue, issie hapa kuna case ya identity theft msione hakuna kesi.
Kwa maelezo yake kuna David wa 1994, na David wa 2001 ni watu wawili tofauti. Labda kama anataka kumchafua mwana! Tufanye ni kweli, yeye anathirika vipi na majina kufanana? Ingemake sense kama wangekua mapacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…