Gobole Lenye Risasi
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,519
- 23,693
Naitwa David Frank Kameta, baada ya kupata wakati mgumu muda mrefu ikiwepo kusalitiwa na mtu ambaye nilimuamini, sasa naona ni bora Dunia ijue kinachoendelea. Hapa nazungumzia usaliti wa rafiki yangu Emmanuel Robert Kakoti jina lake maarufu wengi mnalijua, kwa sasa ni mchezaji maarufu katika klabu kubwa katika Ligi Kuu Bara.
Alichukua jina langu kwa makubaliano maalum kuwa atalitumia muda mfupi lakini amenigeuka na kuendelea kulitumia kwa miaka mingi, hataki kurejea katika jina lake halisi huku akinisababishia hasara nyingi na mzozo katika familia yangu.
Stori yetu ipo hivi…
Tuliishi pamoja Mbeya, tulisoma wote ingawa alikuwa mbele yangu darasani, mimi umri wangu ni miaka 32 (nilizaliwa 1994), yeye mwenzangu alianza kucheza mpira tukiwa wadogo, hayo hayakuwa mambo yangu.
Mwaka 2017 au 2018 (sikumbuki vizuri), Emmanuel akiwa timu ya Mbeya City alionyesha utovu wa nidhamu, uongozi ukamfungia usajili pamoja na kufungiwa kutumia majina yake yote halisi kwenye soka. Hiyo ilimfanya aonekane kama amefutwa kwenye Ulimwengu wa soka.
View attachment 3657241
Kikosi cha Mbeya City cha Msimu wa 2017/2018 ambacho Emmanuel Robert Kakoti alikuwepo (jina la nne kutoka juu).
Kuna siku ilikuwa deadline ya usajili, Emmanuel aliniomba, "Mwanangu, usajili unafungwa leo na nimekosa nafasi, naomba nisaidie cheti chako cha kuzaliwa nitumie kwenda Mbeya Kwanza. Nikianza tu kucheza, nitabadilisha jina kwenye leseni na kurudisha jina langu halisi."
View attachment 3657249Sababu ya urafiki na huruma, nilimpa cheti changu, akafanikiwa kusajiliwa Mbeya Kwanza kwa jina langu la David Frank Kameta. Aliendelea na maisha yake ya soka katika timu ya Lipuli ya Iringa, lakini ilikuwa ni kinyume na ahadi yetu, hakubadilisha jina hilo. Nilimsisitiza kuwa anatakiwa kurejea katika jina lake halisi lakini aligoma.
View attachment 3657251
View attachment 3657252
Picha enzi zetu tukiwa washkaji
Aliposajiliwa katika timu yake ya sasa ya Kariakoo, akaanza kunikwepa, akawa ananipa majibu ya mkato. Huku nyuma mimi nikaingia katika mgogoro wa kifamilia wakiniambia nimeuza jina.
Baada ya msiba wa mzee wangu, familia ilikaa kikao na kunisema sana, nilipompigia simu Emmanuel mbele ya familia hakupokea. Nilituma ujumbe kumtaka ache kutumia jina langu, alinijibu kwa dharau: "Fata sheria yoyote, mimi siachi kulitumia."
Nilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.
Hali hiyo imeniletea athari kubwa sana kiakili na kisheria kwani jamii inaamini niliuza utambulisho wangu na kuna fursa kadhaa nimezikosa kwa sababu yake, nimeamua kuandika hapa baada ya kuona uungwana wangu umeniponza na mtu ananiletea dharau.
🤣Na hili yanga lazima watalipata tu.
Yeaha shida inaanzia hapo.Kitu usichokijua hao jamaa wamegeukana inaonekana walikuwa kwenye makubaliano lakini mmoja wao amekiuka.
Atulie sasa aache wivu.Kubadili mwaka sio ishu Tz.
Nina vyeti vya kuzaliwa viwili na vyote vina tarehe ya kuzaliwa tofauti ni mwezi tu ndo inalingana.
Vyote ni og ila kimoja nilipata nilivyozaliwa kingine nilipata nikiwa chuo.
Hawezi kumuharibia, yeye ni 1994 mwenzake ni 2001.au unataka mshahara wake mgawane sawa ndio maana amekuwa mkali? inshort wote mna makosa hata kama utamwaribia mambo yake.
Shida gani mtu anaelekea kustaafuSiyo mtaalamunsana wa maswala ya Sheria za soka, ila hii inaweza kumletea Duchu shida kwenye soka lake
Nimemshangaa sana jamaa na ukoo wake😂😂😂 wanataka Duchu wagawane mshaharaBWEGE MMOJA KILAZA NWENYE NJAA. SI AMESHAKUAMBIA FUATA SHERIA. FUATA SASA. UNALETA HUKU KULIA LIA KWANINI? HUNA AKILI ALIKUZIDI AKILI. ACHA AFAIDI WEWE KILAZA SANA. JINA LAKO KWA SASA UNAITWA NANI?
Hivi hii kupost kama Anonmaz(Guest) unafanyaje fanyaje?Hapo ni huruma ya mods tu ila wanaoingia jf kama guest hawawezi kufuta wala kureply.ukipost umepost
Hahaha eti chama ana miaka 35? Uongo Uongo Uongo.Ligi ya Tz mchezaji anaweza cheza hata akiwa na umri wa 40. Uongo ni mwingi sana Kwa wachezaji ktk umri.
Anapoteza muda,itakula kwakwe, yeye anasema amezaliwa2001 na jamaa kaweka 2000 ,pia majina kufanana kupo tu,akipeleka kesi mahakamani atapigwa tatu bila huyu mjinga.Tafuta wakili,?? Atakupa mwongoz upate haki yako! Acha kupost personal info zako mhimu kwa kila mtu kitakulamba.
True ,ilitakiwa Duchu angekubaliana naye kwamba natumia vyeti vyako nakupa labda milio 20 ila nakupa 5 kwa awamu nne kisha tusijuane....ila ila ya kumtoa toa vilaki laki lazima wafike hapo.Hapa it seems kulikuwa na mutual agreement ila inaonekana huyo mwamba kakiuka makubaliano so ndo inabidi jamaa ajaribu kumwaga mboga.
Kivipi iwe identity theft wakati walikubaliana?Hii ni kesi ya identity theft. Kesi kubwa sana.
Shida gn atapata duchu?,Siyo mtaalamunsana wa maswala ya Sheria za soka, ila hii inaweza kumletea Duchu shida kwenye soka lake
Bingwa wa hizi mbanga ni Taribo West yule beki mstaafu wa Nigeria,Inter Milan,Derby Country. Mwamba alipunguza miaka 10+ kwenye cheti chake cha kuzaliwa.Ligi ya Tz mchezaji anaweza cheza hata akiwa na umri wa 40. Uongo ni mwingi sana Kwa wachezaji ktk umri.
Kukubaliana hakuondoi identity theft.Kivipi iwe identity theft wakati walikubaliana?
Kwa mujibu wa mtoa post.
Kosa lipo wp?mleta mada njaa imemtoa mafichoni.
Wewe nae hujitambui,sheria gani inaruhusu kutumia vyeti vya mwenzako?Kivipi iwe identity theft wakati walikubaliana?
Kwa mujibu wa mtoa post.
Kosa lipo wp?mleta mada njaa imemtoa mafichoni.