Bank wahuni sana. Mwaka jana mwanzoni nilienda kuweka 1.3M kwenye account yangu ya NMB. Tukahesabu fresh, then baada ya kumaliza nikasepa.
Baadae yule teller wakati anafunga mahesabu, akawa inapelea laki 1. Kila akijaribu kuangalia ile loss inatokea wapi, hapati jibu. Mwisho wa siku akapitisha wazo kuwa mimi hela niliyopeleka ilikuwa 1.2M na sio 1.3M. Akajaribu kunipigia simu, sikuwa hewani. Kwavile alikuwa anataka kufunga hesabu, akaandika slip mpya, inayoonesha nimeweka 1.2M then akafoji sahihi yangu. Kwakifupi akatoa laki moja kwenye account yangu.
Nilipopata ujumbe baada ya kuwasha simu kuwa alinitafuta , ikabidi kesho yake mapema niende.Kufika pale ananipa slip aliyojaza yeye akisema tulikosea kuhesabu. Nikamwambia labda ukosee wewe, zile hela nilihesabu kabla sijatoka home. Tukabishana sana hadi kwenda kwa Manager. Yule teller anakomaa kuwa hata kwenye camera zimeonesha kuwa mimi na yeye tulikosea kuhesabu. Vutana sana pale, baadae kuna mmama mmoja nae ni mfanyakazi pale ndio akamuita ndani. Yule mama akamuonesha kosa lilipotokea, kumbe baada ya mimi kuondoka, kuna mtu alikuja na kutoa elfu 50, ila yeye akamuandakia kaweka elfu 50, it means loss ikajidouble.
Baada ya hapo jamaa akaniomba sana msamaha, mpaka natoka getini jamaa yupo ananiomba msamaha tu. Siku hiyo ndio nikajua kumbe bank inaweza kutoa hela kwenye account yako na usiletewe ujumbe.
Wezi sana.