Mchezo wa Simba na Yanga kuchezwa tena, Mashabiki kurudishiwa tiketi zao

Warudishe pesa za mashabiki kwanza, halafu kila mshabiki ataamua mwenyewe kama atataka kuingia mechi itakayofuata ama la.
 
Bado kanuni na taratibu za kusogeza mchezo mbele zinaitaka TFF / Bodi ya Ligi kufanya hivyo masaa 24 kabla.
Kabla hujakomalia kitu mkuu hakikisha Una uhakika, hiyo kanuni ya 15 haijaishia hapo Tu, kwahiyo we hujawahi kuona mechi imepelekwa mbele Kwa masaa kadhaa kisa mvua au shida yoyote Ile, kasome tena hiyo kanuni utajua tofauti ya postpone na Delay
 
Kwa mfano TFF, wameikatilia Serikali, huo mpira ungechezwa uwanja gani?
Uwanja huo huo uliokuwa umeandaliwa. Kwani si hata mashabiki walishaingia uwanjani tokea saa 4 asubuhi. Kama TFF wangekataa ombi la Serikali, hiyo Serikali ilikuwa haina uwezo wa kuzuia mechi isichezwe. Kanuni na taratibu zilikuwa zinawapa nguvu TFF kukataa ombi la Serikali. Tatizo TFF waliamua kwa makusudi kukiuka kanuni na taratibu zilizowekwa.
 
Mechi inarudiwa vipi wakati sheria inaitaka TFF kuipatia Yanga SC pointi tatu maana walifika uwanjani muda wa mchezo na Simba SC hawakutokea. Yanga SC nitawashangaa wakicheza huu mchezo.
Hapo sasa shida haitakuwa kanuni tena, shida itakuwa ni uoga tu[emoji28].
 
futiboli haihusiani na elimu....
Muone huyu nae, hapa duniani kitu pekee ambacho hakihusiani na elimu(maarifa) ni swala la kufanya mapenzi tu, kwakua hata panzi, mbwa, kuku, Bata wanafanya bila hata kufundishwa.

Soka linahitaji watu wenye weledi na Elimu.
 
Fifa inasema serikali isijihusishe na mchezo wa soka.

Yanga andikeni barua.

Yanga ipi,hii hii ya kina Msolla? Huwatakii mema wewe,unadhani wao hawajipendi.
 
Kwa mfano TFF, wameikatilia Serikali, huo mpira ungechezwa uwanja gani?
Uwanja huo huo uliokuwa umeandaliwa. Kwani si hata mashabiki walishaingia uwanjani tokea saa 4 asubuhi. Kama TFF wangekataa ombi la Serikali, hiyo Serikali ilikuwa haina uwezo wa kuzuia mechi isichezwe. Kanuni na taratibu zilikuwa zinawapa nguvu TFF kukataa ombi la Serikali. Tatizo TFF waliamua kwa makusudi kukiuka kanuni na taratibu zilizowekwa.
Ndugu yangu dawa ya jipu ni kulitumbua tu. Hao TFF ni jipu lililoiva na wakulitumbua ni YANGA.
Yanga Sc sasa hivi amepata golden chance ya kurudisha heshima ya mpira Tanzania. Ni kweli kutakuwa na maumivu wakati jipu likitumbuliwa lakini ni bora maumivu ya muda mfupi kuliko kuacha uchafu wa TFF uendelee kuwepo.
Mimi nawashauri Yanga kama watanyimwa points 3 basi wapeleke malalamiko yao FIFA.
 
Mwenyekiti wa yanga ndio aliowachuuza yanga alikubali na alipewa taarifa saa mbili asubuhi
Kanuni inasema taarifa inapaswa kuja masaa 24 kabla. Labda kama kuna dharura inayohatarisha usalama wa watu lakini hakukuwa na dharura yoyote sababu hata mashabiki walianza kuingia uwanjani kuanzia saa 4 asubuhi.
 
Chezeni mshinde, Ili mpewe hizo point acheni uoga.
 
Ndugu unazifahamu vizuri kanuni na taratibu za kuahirisha mechi au kusogeza muda mbele?
Kabla ya kuahirisha mechi au kusogeza muda mbele ni lazima kuwe na sababu za msingi kufanya hivyo. Je, ni sababu zipi za msingi zilizotolewa na TFF?
Ukifuatilia kanuni hata Simba wanamakosa sababu kwa kufuata kanuni hawakupaswa kukubaliana na TFF. Kama Simba wangeikatalia TFF basi leo tungesema hakuna wa kupewa points 3. Lakini kitendo cha Simba kushirikiana na TFF kuvunja kanuni za soka ndiyo kinawapatia nguvu Yanga kudai points 3 na magoli 3.
 
Mkuu ata kama ungesema ukweli kuwa wewe ni shabiki wa Yanga bado haiondoi maana kuwa umeandika kitu usichokielewa vizuri au kama unaelewa basi umeamua kuandika kinazi, na sio kwamba serikali haitakiwi kuingilia mpira issue ni kwamba imeingilia kwenye issue ipi? Kwani serikali iliposimamisha michezo kipindi cha Corona FIFA ilisemaje? Unajua kilichofanya Namungo mechi na Agosto isichezwe kwao ichezwe Tanzania ni nini?

Anyway turudi kwenye mada mkuu, Anaetoa points 3 na magoli sio chama cha soka ni mwamuzi wa mchezo husika baada ya taratibu zote kuwa zimefatwa Kabla ya mchezo husika kuanza, kwahiyo team inatakiwa kukaguliwa,kuthibisha kikosi cha kuanza na akiba, kwahiyo kabla ya kudai points3 jiulize mwamuzi alikuepo?
 

Usiwadaganganye wenzio wakati wewe hapa huo ujasiri hata wa kutumia Jina lako halisi huna. Yanga watapeleka Team na mechi itachezwa vizuri tu
 
Ticket huwa wanachanachanaa mlangoni na mteja habakiwi na kielelezo cha malipo sasa hili liwe funzo kuwa mteja anatakiwa abakiwe na risiti kutokana na malipo aliyofanya
 
Hivi mbona wanakwepa sana kusema ni nini kilisababisha kughairi huu mchezo?

Kwanini hatuambiwi tatizo lilikuwa nini?
ni nani alietoa agizo hilo .. huyu ndio wa kum'bana aseme alitumwa na nani na aeleze sababu ya kusogeza mbele hii game ilikuwa ni nini?

na kwa nini hawataki kuwaibishana?
 
Kanuni inasema taarifa inapaswa kuja masaa 24 kabla. Labda kama kuna dharura inayohatarisha usalama wa watu lakini hakukuwa na dharura yoyote sababu hata mashabiki walianza kuingia uwanjani kuanzia saa 4 asubuhi.
Kuna hili pia.....Michezo iliyo na mazingatio maalum, muda wa kuaanza mchezo (kickoff) zitazingatia mazingira husika...
 
"Mpira sio wa kila mtu mzee" na unashindwa kutambua sheria ya kuhairisha au kusogeza mchezo ni masaa 24? TFF walifuata kanuni ipi?

Nikiona kijana anatumia emojis na maneno kama 'Ko' nafahamu fika amejawa na tabia za Uswahili.
Unadhani hiyo kanuni ina apply kila mahala?
Mfano kuna threat ya kiusalama imebainika masaa mawili kabla ya mchezo, napo tutadai masaa 24 kuahirisha mchezo?
 
Kanuni inasema taarifa inapaswa kuja masaa 24 kabla. Labda kama kuna dharura inayohatarisha usalama wa watu lakini hakukuwa na dharura yoyote sababu hata mashabiki walianza kuingia uwanjani kuanzia saa 4 asubuhi.
Unaijua sababu ya kupelekwa mbele ya ule mchezo? Tujuze mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…