Mchezo wa Simba na Yanga kuchezwa tena, Mashabiki kurudishiwa tiketi zao

Mchezo wa Simba na Yanga kuchezwa tena, Mashabiki kurudishiwa tiketi zao

Utopolo unajifichaje kupitia kagera sugar?

Ukiona nyani anang'ang'ania shamba la miwa ni kwa vile ana njaa.Maana hawezi kukwea miwa
Kufikia sasa Yanga SC ndio imebeba hatima ya mpira kwa Tanzania aidha ifungiwe au lah! Yanga SC wakilisogeza hili CAF au FIFA, mpira utaanza kusahaulika.

Mimi sio shabiki wa vilabu hivi ni shabiki wa Kagera Sugar lakini TFF imekuwa na mambo ya hovyo yanayokera, nashangaa watu kulichukua hili kwa mapenzi kuliko mtazamo wa kiuhalisia.
 
Utopolo wanajua haya!Wengi ni vilaza sana
Umeongea vzur ,rejea ata mechi ya namungo ambayo alitakiwa acheze kule angola kimsing serikal yao ndio ilikua sababu ya ile mechi kutochezwa kule baadae caf wakatoa taarifa kwamba wao wanaanza kueshimu taratibu na sheria za nchi kwanza mwsho mechi ikarudiwa kama ingekua kila serikal ikiusika bas kufungiwa nadhan nchi nyng zingekula ban kila cku ,kutofutisha mpra na serikal ni kutaka tu kuwe na mgawanyo wa majukum na madaraka pamoja na kuheshimiana lakn iv vtu lazma viingiliane sana ndio maana nchi nyng zina wizara ya michezo au taasisi inayousika na michezo
 
Hivi mbona wanakwepa sana kusema ni nini kilisababisha kughairi huu mchezo?

Kwanini hatuambiwi tatizo lilikuwa nini?
Si rahisi mkubwa kujivua nguo mbele ya kadamnasi! Itoshe tu kuwa serikali imeomba radhi!! Ukidai zaidi ya hapo utakuwa na lako jambo!
 
Serikali itambua kuwa pamoja na kuagiza mfumo wa ticket uwanja wa Benjamen Mkapa kuwarudishia mashabiki ticket zao kwa mechi ya Simba na Yanga pia watambua mtaani ni hivyo hivyo.

Tangu saa 5 asubuhi watu walikuwa wanachukua siti kwenye mabanda umiza ili kuweza kuangalia mechi hiyo.

Wasimamizi wa mabanda umiza walikuwa wameanza kuchukua kiingilio kati ya sh 500 na 2000 kulingana na sehemu husika.

Tunaitaka serikali itoe tamko kuwa siku ya mechi ya Simba na Yanga mabanda umiza yote waonyeshe mechi hiyo bure maana si rahis kujua ni nani alilipa kulingana na mfumo wao usio na ticket.

Tunaitaka serikali itoe tamko kwa nchi nzima kwa mabanda yanayoonyesha mechi hizo.
 
Hivi ikitokea shabiki akaiandikia FIFA malalamiko yake na akaweka ushahidi kuhusu kuvurugwa kwa mechi ya simba na yanga, je FIFA inaweza kuchukua hatua?

Ila TFF warudishe viingilio vya watu. Wasiporudisha ni wizi wa kuaminiwa. Na ni aibu kwa mamlaka kuwatapeli wananchi.

Pia tujifunze kukata tiketi za kimtandao, ili mechi ikihairishwa basi unakuwa refunded haraka. Ni kukomandi tu.
 
Utopolo unajifichaje kupitia kagera sugar?

Ukiona nyani anang'ang'ania shamba la miwa ni kwa vile ana njaa.Maana hawezi kukwea miwa
Bro mie shabiki wa Kagera Sugar na kwa uwazi sipendi kuona hivi vilabu vikiwa juu maana vimevuruga mpira wa Tanzania na hasa Kagera Sugar.

Msimu Kagera Sugar tuliomaliza nafasi ya tatu tulifanyiwa hujuma nyingi mno, msimu ule kombe la ligi lilikuwa letu. Na kuona hivyo msimu uliofuata TFF, Wallace Karia na Bodi ya Ligi walihitaji kutushusha daraja.
 
Unaijua sababu ya kupelekwa mbele ya ule mchezo? Tujuze mkuu
Sababu iko wazi na inajulikana. Hata wewe unaijua pia. Ni sababu ya kijinga isiyokuwa na maana ndiyo maana hata hao Serikali wanaona aibu kuisema hadharani.
Iko hivi : siku ile Mzee Mwinyi alikuwa anazindua kitabu chake na ndiyo maana wakaona wasogeze mchezo mbele mpaka saa moja jioni.
Sasa kama walifahamu ratiba ya mpira itaingiliana na uzinduzi wa kitabu kwanini hawakupanga tarehe ya mechi iwe siku nyingine?
 
Na ile bendi uwanjanì ilikuwa ya nn?
 
Back
Top Bottom