Hayo makabila mengine yaliyobaki yote ni ya CCM na hayahusiki na uchaguzi huo wa CDM.
JF inaanza kupoteza watu wanaojibu/leta hoja nzito. Mkuu uwe unauliza ama unafikiri kabla ya kutenda. Karibu 50%+ ya wabunge kutoka mkoa wa Mara, walitoka CDM kabla ya hamahama huu ni mfano mdogo tu
BUNDA
TARIME MJINI
TARIME VIJIJINI
SERENGETI
Unawezaje kusema kuwa huku watu hawahusiki na uchaguzi wa chama fulani ilhali chama kilisimika wagombea enzi hizo? Kitu ambacho kitaimaliza CCM ni kubweteka sawa tu na upinzani walivyobweteka hadi walipojikuta wanatakiwa kuunga juhudi ilhali hata sasa wakiulizwa nia hasa ya kuhama chama ili kuunga juhudi ilkuwa nn, hawawezi kuwa na majibu yenye tija.
Sikatai watu kuhamia kwetu, ila nina wasiwasi baada ya upinzani kufa, tutaanza kupingana wenyewe kwa wenyewe. Ikumbukwe upinzani halisi sio rangi/jina la chama. Upinzani maana yake ni kutokukubaliana katika jambo fulani. Familia fulani zikikinzana katika nyanja tofauti, ni sawa kabisa. Lakini ndani ya familia yakifanyika mambo yanayoigawa familia (tuchukulie mfano mdogo tu, MIRATHI) hasa kwa extended family, ni hatari sana.
Heri ukipambana na adui unayemuona ni rahisi kumshinda, kuliko kupambana na adui usiyemuona wala kumfahamu. CCM itaangushwa na wanaccm wenyewe kwakuzoea dezo. Tujiulize siku mwenyekiti wa sasa akistaafu akaja mwingine asiyetupa dezo na upendeleo mkubwa kiasi hiki, tutaweza? Wanaounga juhudi leo, wataendelea kutuunga? Au ndio watarudi kwao kwakisingizio cha mwenyekiti mpya kufanya tofauti na huyu wa sasa?