Mchumba wangu wa miaka 5 anafunga ndoa kesho inaniuma sana, nifanyaje?

Mchumba wangu wa miaka 5 anafunga ndoa kesho inaniuma sana, nifanyaje?

Kama ungefanikiwa kumuoa ungejuta Sana.

mshukuru MUNGU amekuepusha maumivu makali zaidi ya unayopitia Sasa.

Pamoja na hayo utampata bora zaidi ya huyo aliyekuacha.

Tumia hasira zako kupambana uwe Bora zaidi , kiuchumi, endelea kujifunza uwe mwelewa zaidi .
JE UKIMFANYIA FUJO UTAMPATA⁉️
Uwe na uhakika UKIMFANYIA FUJO KILa mtu ataelewa kuwa hujawahi kumfaa.
Na katika miaka 5 aliyokupatia hukuwa kumfaa ( KWA mtazamo wake).

Jipe pole. Utakuwa sawa. Ni jaribu ni mitihani umekupata. UNAPASWA KUSHINDA.
 
Aisee yule binti niliemuacha sijui alijihisije sikujua kuwa kumuacha mtu kunauma kiasi hicho

Mkuu wanaume huwa tunaumia zaidi kama umemhudumia mwanamke halafu hujamgusa tupu yake kisha akakuacha kama ulimgusa nakuhakikishia atarudi tu kama mchepuko
 
Mwingine alimpatia mtaji Mkubwa mchumba wake na akaachwa.

Mwingine alimjengea nyumba mchumba wake na akaachwa.

Mwingine alimnunulia gari mchumba wake na akaachwa.

Hujasikia yule alidonate figo, Mchumba alipopona akamuacha.

Sifagilii kuachana.
Ila kuachana katika hatua ya uchumba ni Bora zaidi ukilinganisha na (mfano) Angekuacha t
Mkubwa na Watoto 2?

Mkuu una bahati Sana. Mshukuru MUNGU na utoe sadaka ya shukrani unakoabudu.
 
Hao wahuni achana nao, heshimu tu uamuzi wa huyo mchumba, ni chaguo lake. Wanawake wapo wengi, tafuta mwingine. Nenda kwenye harusi na umpongeze.
 
Mapenzi yanauma kuliko chochote sababu hayana dawa kabisa. Huyu binti nilimpenda kupenda, anatembea na nusu ya uhai wangu.

Tumekuwa kwenye mahusiano muda mrefu na tulipanga mengi, nilijitahidi kumridhisha katika mahitaji yake ya kimwili, kihisia na kiroho. Kwa bahati isiyo yangu binti katamka kuwa hanitaki yaani amekutana na better half hivyo anafunga ndoa.

Alivyo na jeuri kanipa na kadi kabisa. Hapa nimepanga na wahuni wa kitaa tukamharibie. Yaani hawezi niacha kizembe hivi. Ameanzisha lazima nimalizie, ngoja leo nilewe kabisa.
Miaka mi5,hukua muoaji wewe,ukipata mwanamke kama umemuelewa na mmependana kweli usimalize mwaka oa,wanawake wanakimbizana na menopause
 
Niko salama wa afya ,sijafanya come back yoyote ila nimegundua kuwa haitakiwi Mimi nimpende mwanamke wa kuoa ila anipende yeye baada ya kumpata mdada mzuri mmoja wa mji wa mbeya ili nimuoe ,akanipiga kibuti baada ya kumvutia hela afanye biashara ,akaenda kuolewa na mlina asali huko Tabora .
Itoshe kusema nipo kama Jana ,sielewi moja Wala mbili ila kiafya nimejaa tele na Sina mpango wa Mambo hayo kwasasa
Duu Kwa hiyo, umepigwa za uso mara 2, pole sana
 
Niko salama wa afya ,sijafanya come back yoyote ila nimegundua kuwa haitakiwi Mimi nimpende mwanamke wa kuoa ila anipende yeye baada ya kumpata mdada mzuri mmoja wa mji wa mbeya ili nimuoe ,akanipiga kibuti baada ya kumvutia hela afanye biashara ,akaenda kuolewa na mlina asali huko Tabora .
Itoshe kusema nipo kama Jana ,sielewi moja Wala mbili ila kiafya nimejaa tele na Sina mpango wa Mambo hayo kwasasa
Umezira au sio!
 
Title imekaa kuwa unaomba ushauri ufanyeje ila ndani ya uzi tayari una uamuzi wako sasa sijui kipi ni kipi. Ila kama hicho ulichoandik ndicho kweli unapanga kukifanya sidhani kama ni sahihi. Kitakupa ahueni ya muda mchache lakini baada ya muda fulani utakuja ujutie na kujiona mjinga.

Nenda harusini, kula, shiba, cheza amapiano, rudi kalale. Kama huwezi kaa ndani kwako liaaa mpaka uchungu uishe na baada ya muda utakuwa sawa...

Naomba kuwasilisha...
Story ya kutunga hii mkuu,mtoa mada hana hata kumbukumbu
 
Mapenzi yanauma kuliko chochote sababu hayana dawa kabisa. Huyu binti nilimpenda kupenda, anatembea na nusu ya uhai wangu.

Tumekuwa kwenye mahusiano muda mrefu na tulipanga mengi, nilijitahidi kumridhisha katika mahitaji yake ya kimwili, kihisia na kiroho. Kwa bahati isiyo yangu binti katamka kuwa hanitaki yaani amekutana na better half hivyo anafunga ndoa.

Alivyo na jeuri kanipa na kadi kabisa. Hapa nimepanga na wahuni wa kitaa tukamharibie. Yaani hawezi niacha kizembe hivi. Ameanzisha lazima nimalizie, ngoja leo nilewe kabisa.
Hapo kwenye kutembea na nusu ya uhai wako ndipo ulipofeli
 
Back
Top Bottom