Huo ukuu uko kwenye nini? Mbona kila mara mungu mkuu, mungu mkuu, huo ukuu uko kwenye nini kama magonjwa tu hawezi kuyaondoa wala kutibu watu wake?
Rais ni mkuu wa nchi kwa sababu inaweza kutokea njaa akaamuru watu wote walioathirika na njaa wapewe chakula, au wajengewe nyumba kama wamepata mafuriko na watu wakaona na wakakiri kweli huyu ni mkuu wa nchi. Sasa Mungu ukuu wake uko wapi? Mbona hauonekani?
Huyo Mungu ambae hawezi kuzuia magonjwa, njaa, vita, mafuriko, majanga ya asili ukuu wake uko wapi? Yaani anakua mkuu huku hawezi kufanya jambo lolote la maana likaonekana?