Mchungaji: Baba ndio anapaswa kutoa Baraka kwa watoto na si Mama

Mchungaji: Baba ndio anapaswa kutoa Baraka kwa watoto na si Mama

Kama hujawahi kumjua hata baba yako ni nani au hakuna hata hilo kaburi la baba??
Hapo Yoda unakuwa ni uzembe wako we litoto na mamaako.

Hakuna mtoto asie na baba.

Beijing ikae mbali hapa ni scriptural facts tu!
 
Moja ya mijadala iliyokuwa na maoni mbalimbali ni hii video clip ya Mchungaji mmoja nchini Tanzania akisema kuwa Baba au Mwanaume ndio anapaswa kutoa Baraka na si Mama.

Watu wengi wameunga mkono na wengine kupingana nae.

Wengine walienda mbali na kurejea visa mbalimbali kwenye biblia

Mwanzo 27:27–29 — Isaka anambariki Yakobo

Isaka alimbariki Yakobo kwa kumtamkia mafanikio, mamlaka na maisha yenye baraka. Hili lilikuwa tukio muhimu katika historia ya baraka za baba kwa mtoto wake katika Agano la Kale.

Mwanzo 48:15–20 — Yakobo anawabariki wana wa Yosefu

Yakobo aliwawekea mikono Efraimu na Manase na kuwabariki. Hata aliweka mkono wake wa kuume juu ya Efraimu, mwana mdogo, badala ya Manase, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza.

Mwanzo 49:1–28 — Yakobo anawabariki wanawe kumi na wawili

Yakobo aliwakusanya wanawe na kutamka maneno yaliyohusu maisha na mustakabali wao.

Nini maoni yako mdau

View: https://www.instagram.com/reel/Dec0ePXjILq/?vrfl=aXh4M2EzOXAzbXY4

ShesRise_1 , binti kiziwi nchi ina upuuzi mwingi sana hii 🚮🚮🤦🏾‍♀️

giphy-downsized-medium.gif
 
Yaan aliye beba mimba miezi 9, na akajifungua kwa uchungu, akanyonyesha ziwa lake kwa miaka kadhaa, na kumlea kwa mapenzi na kila hali, eti asitoe baraka,

Kuna mama m1 tu, ila kuna baba wengi.

Mfumo Dume ni janga kuu kwa sasa. Huyo Mchungaji ajitafakari kwa kina. Kwa hayo mahubiri yake.
Baba yako alikubeba kwenye korodani zake miaka mingapi? Hiyo miezi 9 tu kwa mama!
Huyo Mchungaji amenukuu maandiko, si maneno yake
 
wewe ndio ujitafakari, umewekewa had vifungu vya biblia! Tatzo ubinafs ndio umekujaa, wanawake kama niny ndo mnawamezeshaga sumu kuwachonganisha watoto na baba il baba aonekane hana umhm
 
Kuna watu walikuwa Waislamu wametengewa na familia zao, hao sio yatima.
Wanazipataje baraka za baba ?
Kwani Waislamu si wana MUNGU, baraka unazipata kwa MUNGU pia... sio lazima kwa Baba yako mzazi hawepo
 
Yaan aliye beba mimba miezi 9, na akajifungua kwa uchungu, akanyonyesha ziwa lake kwa miaka kadhaa, na kumlea kwa mapenzi na kila hali, eti asitoe baraka,

Kuna mama m1 tu, ila kuna baba wengi.

Mfumo Dume ni janga kuu kwa sasa. Huyo Mchungaji ajitafakari kwa kina. Kwa hayo mahubiri yake.
Baraka ya mama ni automatically ila ya baba ni vizuri akaitamka
 
Wala hata si mchungaji bali ni maandiko... taja kwenye biblia ni mwanamke gani aliyewai kubariki watoto wake
Maandiko gani? Haya haya mnayo pinga kuwa yamepitwa na wakati, na ni uongo? Nyie wanaume acheni UNAFIKI.
 
Baraka, laana, karma ni imani za kufikirika tu hazina uhalisia wowote. Ukiwa mjinga utaamini zipo na zinafanya kazi.
Tatizo ni kuchanganya mambo matatu tofauti: imani, falsafa na ukweli unaoweza kuthibitishwa kisayansi. Ni kweli kwamba baraka, laana na karma hazijathibitishwa kisayansi kama nguvu zisizoonekana zinazoweza kuathiri maisha ya mtu kwa namna ya kimiujiza. Lakini kusema kila anayeziamini ni mjinga ni kushambulia watu badala ya kujibu hoja. Mtu anaweza kuwa na elimu kubwa na bado akawa na imani za kiroho.

Pia, karma inaeleweka tofauti na baraka na laana katika dini mbalimbali. Huwezi kuvichanganya vyote na kuvihukumu kwa sentensi moja. Kama una ushahidi kwamba havina uhalisia, uweke mezani. Na kama mtu anadai vinafanya kazi, naye aonyeshe ushahidi. Kutokuamini jambo si uthibitisho kwamba halipo, kama ambavyo kuliamini si uthibitisho kwamba lipo. Hoja hujengwa kwa ushahidi, si kwa kuwaita wengine wajingTatizo ni kuchanganya mambo matatu tofauti: imani, falsafa na ukweli unaoweza kuthibitishwa kisayansi. Ni kweli kwamba baraka, laana na karma hazijathibitishwa kisayansi kama nguvu zisizoonekana zinazoweza kuathiri maisha ya mtu kwa namna ya kimiujiza. Lakini kusema kila anayeziamini ni mjinga ni kushambulia watu badala ya kujibu hoja. Mtu anaweza kuwa na elimu kubwa na bado akawa na imani za kiroho.

Pia, karma inaeleweka tofauti na baraka na laana katika dini mbalimbali. Huwezi kuvichanganya vyote na kuvihukumu kwa sentensi moja. Kama una ushahidi kwamba havina uhalisia, uweke mezani. Kutokuamini jambo si uthibitisho kwamba halipo, kama ambavyo kuliamini si uthibitisho kwamba lipo. Hoja hujengwa kwa ushahidi, si kwa kuwaita wengine wajinga.
 
Kuna watu hawaujui hata ukoo wao, walitupwa au walipatikana kwa one night stand na mama yao hajui baba yao ni yupi.
Mkuu huwa una challenge kila kitu!
Kwenye hiyo semina mchungaji aliongelea nguvu ya gender ya kiume na inayotoa baraka ni ume.
Na sikama akina mama wanavyoamini kwenye 50/50 full stop.
 
Baraka, laana, karma ni imani za kufikirika tu hazina uhalisia wowote. Ukiwa mjinga utaamini zipo na zinafanya kazi.
Subiri wanaume wenzio wakupopoe hapa.
😂😂😂😂
 
Maandiko gani? Haya haya mnayo pinga kuwa yamepitwa na wakati, na ni uongo? Nyie wanaume acheni UNAFIKI.
Nani anayesema maandiko yamepitwa na wakati... kwa hiyo ni katiba

Maandiko yamekuwepo Karne nyingi hata kabla ya hiyo simu kuvumbuliwa
 
Maandiko gani? Haya haya mnayo pinga kuwa yamepitwa na wakati, na ni uongo? Nyie wanaume acheni UNAFIKI.
Sio wote wanaopinga maandiko pia ukishaweka akili yako kupinga ,itakutengenezea energy yakupinga kila kitu
 
Kuna watu hawaujui hata ukoo wao, walitupwa au walipatikana kwa one night stand na mama yao hajui baba yao ni yupi.
Sio lazima Baraka zitoke kwa Baba mzazi, Mungu pia anaweza kutoa Baraka
 
Hapo Yoda unakuwa ni uzembe wako we litoto na mamaako.

Hakuna mtoto asie na baba.

Beijing ikae mbali hapa ni scriptural facts tu!
Watoto wengi tu duniani hawana baba zao kwa sababu nyingi sana.
 
Hakuna Baraka.

Baraka ni illusions tu.

Halafu dini zina pendelea sana wanaume kwa sababu waanzilishi wa hizi dini ni wanaume.
 
Baba yako alikubeba kwenye korodani zake miaka mingapi? Hiyo miezi 9 tu kwa mama!
Huyo Mchungaji amenukuu maandiko, si maneno yake
Maandiko gani haya haya mnayo yabananga kila uchwao humu ndani? Au yepi?

Mnasumbuliwa na mfumo dume, unao zaa UNAFIKI.
 
Watoto wengi tu duniani hawana baba zao kwa sababu nyingi sana.
Kutokuwa na Baba haimaanishi uwezi kubarikiwa... MUNGU utoa Baraka hata muda mwingine bila kuombwa
 
Back
Top Bottom