Bila amani huwezi fanya kitu Mchungaji Kimaro kapotoka kwenye hilo
Amani ni kitu cha kwanza kabisa ili vingine vifanyike
Biblia inasema kwenye Mwanzo 1:2-3
"Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru."
Nchi ilipokuwa imejaa ukiwa na utupu na giza Roho ya Mungu ilitakiwa kuwa na amani kwanza ndipo akaanza kuumbs nuru nk
Bila amani hakuna kiwezacho fanyika iwe haki au chochote
Israel walipoona jeshi la farao liko nyuma na mbele kuna bahari walichanganyikiwa wakaambiwa wawe na amani ili wauone uwezo wa Mungu
Penye amani vingi vyaweza fanyika
Nchi kama kongo wana mali za asili zote ukosefu wa amani tu ndio kipengele kinawafanya wasiendelee na ukiwauliza wanasema wazi hitaji lao kubwa ni amani