Lete ukweli
Sent from my Nokia 8.1 using
JamiiForums mobile app
Ukweli ni huu:- Adam na baadaye Eva hawakuwa watu wa kwanza kuumbwa duniani bali Adam alikuwa ni mtu wa kwanza kupewa utume na Mungu kwa ajili ya watu aliokuwa akiishi nao huko Babylon Iraq ya kale (Kati ya mto Euphrate na Tigris), Adam alikuwa mtu wa kwanza kupata mafundisho ya kumjua Mungu kutoka kwa Mungu na hivyo anakuwa ni mtu wa kwanza duniani kuwa civilized na ndiyo maana sisi watu wa baadaye tunaitwa Wanadamu (human beings), human being is a civiized man. Wanaadamu ni sawa na Wana wa Adamu na hii ni sifa ya kiroho tuliyoirithi kutoka kwa huyo Baba yetu wa kiroho Adam na wala sio kwamba huyo Adamu ndiye baba wa kimwili wa watu wote hapa duniani. Huyo Adam ameishi hapa duniani takriban miaka 6000 iliyopita lakini hapa Tanzania fuvu la mtu wa kale Zinanthropus Boisei lilifukuliwa huko Oldivai gorge na kuonekana kwamba lina umri wa miaka 1000,000---- unaweza kuona huo utofauti??!!, hii maana yake ni kwamba kabla ya Adam HAJAZALIWA kulikuwepo na watu isipokuwa walikuwa uncivilized.
Kuhusu Yesu kupaa juu mbinguni, yakupasa ukumbuke kuwa Injili zinazozungumzia habari mbalimbali za Yesu zikiandikwa na waandishi miaka mingi baadaye baada ya tukio la msalabani (the crucifixion) na hakuna hata muandishi mmoja wa injili alishuhudia tukio hilo bali katika kuandika Injili zao hao waandishi walitegemea habari za kusimuliwa kutoka kwa watu waliodhaniwa kuwa wanajua ukweli wa mambo ya Yesu, mfano Injili ya Luka ni Barua aliyoiandika Luka juu ya habari za Yesu kwenda kwa mfalme Theophile (luka 1:1).--- sasa katika habari za aina hiyo tunatakiwa tuwe wachunguzi kuliko kubeba kila habari kama ilivyo:
Yesu alikuwa ni mtu mkubwa wa Mungu na hawezi kuongea uongo, tunapata katika injili akisema kwamba; kuna kondoo wengine nao si wa zizi hili nami yanipasa niwakusanye chini ya mchungaji mmoja,---- hata amepata kusema; kuna kondoo yapasa wasikie sauti yake.
Alipokuwa akihubiri Injili kwa wana wa Israeli Yesu alipatwa na misukosuko kadhaa na mkubwa kuliko yote ni kupigiliwa msalabani na aliposhushwa msalabani inasemwa alikuwa kisha kufa na baadaye akafufuka, hapa ndipo mjadala unapoanza, Ukweli ni kwamba Yesu aliposhushwa msalabani hakuwa AMEKUFA kwani aliposhushwa yule askari alimchoma mkuki mbavuni na MARA damu na maji vikatoka, hii ni ishara kwamba Yesu alikuwa hai ila tu alikuwa kazimia kwani Damu kamwe haiwezi kutoka katika mwili uliokufa kwani mwili uliokufa moyo hausukumi tena damu, na hapo tunaona jinsi Mungu alitaka kumuokoa Yesu na hivyo kwa ujinga wa yule askari akashindwa kugundua hilo.
Mwili wa Yesu alipewa Yusufu wa Armateo aliyekuwa daktari na mfuasi wake wa siri na ukawekwa pangoni pango lililochongwa na huyo Yusuf na humo mwili huo ukapazwa marhamu (Jesus ointment) za uzito wa ratili 100, swali hizo marhamu zote zilikuwa za nini kwa Mwili ulioisha kufa??-- na kwa nini Mwili wa Yesu apewe mtu binafsi ilhali yeye alihukumiwa kunyongwa (kusulubiwa) na serikali ya Kaisari??.
Kwa siku tatu Yesu alikuwa akipata huduma ya tiba mle pangoni na siku ya tatu "AKAFUFUKA"-- neno hilo kufufuka ndilo linaloleta shida ukweli ni kwamba neno hilo limetumika kwa maana kwamba Yesu aliposhushwa msalabani alidhaniwa KAFA na mtu aliyekufa anapopata uhai huwa inasemwa amefufuka--- japo jambo la mtu kufa na kufufuka ni mada nyingine-- itoshe kusema kwamba Yesu hakufufuka bali ALIZINDUKA kutoka katika hali ya kuzimia baada ya kupata tiba mle pangoni.
Kufupisha hadithi ni kwamba Yesu alipozinduka akapanga mpango wa kuhama kwasababu kuendelea kuishi pale haikuwa salama tena na kwa mara ya mwisho akakutana na wanafunzi wake ambao walipomuona kwa mara ya kwanza baada ya tukio la msalaba walidhani ni pepo au mzimu "uliofufuka" kwani nao waliamini amekufa naye akawatoa shaka akawaonyesha majeraha ya misumari na akawambia wamshike kwani pepo hana mwili wakipomshika wakaamini.ndiye yeye na isitoshe wakampa Samaki akala mbele yao, hapo ndipo alipoagana na wanafunzi wake na ikasemwa "ALIPAA"---- kwanini ilisemwa alipaa???, jibu ni hili; Yesu kama nilivyosema alikuwa na mpango wa kuhama pale yeye pamoja na mama yake Bi Mariam na Maria Magdalene hivyo kuwaficha askari na watu wabaya wasiweze kuwafuatilia na kumkamata ili akatumikie tena Adhabu ya kifo ilibidi utengenezwe UONGO kwamba KAFUFUKA na AMEPAA MBINGUNI hii ilikuwa ni strategy ya kuwaonyesha maadui wa Yesu kwamba Yeye ni mtu wa Mungu kashinda kifo na kapaa mbinguni na kamwe hawawezi kumpata pia ilikuwa ni njia kuwaficha maadui ili wasijue kaelekea wapi.
Hadithi hii ni ndefu sana, ila nafupisha, Yesu alihama yeye na Mama yake na maria Magdalena kupitia Pakistani kuelekea Kashmiri, mama yake alifariki wakati wakiwa safarini a alizikwa chini ya milima inayoitwa (Muree mountains) yaani Mary's Mountain ilipewa jina hilo kwa heshima ya huyo mama, Yesu akaendelea hadi akafika Sri nagar ambako kuna Waisraeli wengi huko na wakampokea na akaendelea kuwahubiria Injili (kondoo wengine wasiokuwa wa zizi lile) hadi kifo kilipomkuta huko akazikwa kwa heshima kubwa huko.
Huko aliitwa Yuz Asaf, na kaburi lake hadi leo lipo katika mtaa wa khan yar huko Sri nagar.
Watalii wengi sana kutoka sehemu mbalimbali duniani huenda kulizuru hilo Kaburi, ni Kaburi maarufu sana huko Kashmiri,
Nenda youtube na angalia ROZABAL SHRINE.
HILO NDILO KABURI LA YESU.
KAMWE YESU HAKUPAA MBINGUNI.