Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

hii haimaanishi hawakupenda kumzika au walimtelekeza, kimaro ni mpotoshaji sana, anatafuta kufungiwa tena. kumiliki kaburi enzi hizo halikuwa jambo dongo manake lilihusisha kumiliki ardhi hapo unapochimba kaburi. wanafunzi wa Yesu hawakuwa matajiri, wengi walikuwa wavuvi na watu wa kawaida na walipoteza muda wao mwingi kuhubiri na Yesu hawakuwa matajiri, Yesu mwenyewe hakuwa tajiri ndio maana hata walipoombwa kodi ya kaisari alimwambia petro akavue samaki atakuwa mdomoni mwake kuna dinari ya fedha wakatoa sadaka kwa kaisari.

huwezi kuchimba tu popote, ndio maana Yusufu tajiri alishanunua kipande pale na akachimba kaburi lake, na kwasababu alikuwa mwanafunzi wa siri wa Yesu, aliamua kuuomba mwili akazika kwenye kaburi alilokuwa ameshalichimba. kina petro na wengine wangechimba lingine la nini sasa wakati tayari limetolewa?

na hata petro na wenzake wangekuwa wamemkimbia nisingeshangaa manake Yesu alikufa kifo cha aibu mno na wanafunzi wake walikuwa terrified, kama kweli walikimbia haimaanishi hawakupenda kumzika. alikufa kifo cha aibu na cha kutisha na wanafunzi nao walihofia kukamatwa kuwekwa msalabani. kimaro awe makini na mahubiri matamu ambayo hayaokoi, no wonder walimsimamisha. anawaza tu hela hela all the time. kwani kuzikwa ni nini hata angezikwa kimasikini unafikiri asingefufuka?

vilevile, Yesu kuzikwa na tajiri ilishatabiriwa na Isaya 53, pale lilikuwa linatimia Neno tu la Mungu. manake kama Neno lisingeandikwa, basi pengine masikini wangemzika. msimsikilize kimaro, Yesu alizikwa na tajiri ili kutimiza unabii wa Isaya 53 na kila maisha aliyoishi alikuwa anaishi akitimiza aliyoandikiwa. makanisani hatuhitaji tajiri, tunahitaji watu walioamua kumfuata Mungu, tunahitaji watu wanaomwabudu Mungu, awe tajiri au masikini wote mbingi inatuhitaji.

shida kubwa ya kimaro ni kwamba hajaokoka na mahubiri yake anatumia elimu ay dunia hii na akili ya kibinadamu, hahubiri kwa Roho Mtakatifu ndio maana siku zote anahubiri mahubiri ya kupendezesha watu na motivations, hayo yanajenga mwili ila sio roho.
 
Kutunza makaburi ni ajira halali kama ajira zingine watu wameajiriwa kutunza makaburi na serikali naye kaanza dharau kama Godblless lema kusema kazi ya bodaboda ni laana

Huyu naye kaanza kuponda watunza makaburi.Watu wanaishi kwa mishahara hiyo anawaponda .Wengine hao watunza makaburi ni waumini wa KKKT anawapelekea ujumbe wa dharau hivyo Hawatendei haki
 
Niko peramiho karibu tulime. Naona tangu tuzike chato hujawa sawa hadi leo
 
Wapi kawadharau? Acha chuki za kimaskini
 
Endelea kuishi kwa kukariri. Ndo mana maskini hadi leo na unachukia tajiri akisifiwa
Nakariri wapi kijana.

Usidhani unavyoandika andika hapa Kuna watu hawakujui.

Tunakujua sema tunakausha tu.

Haya endelea kudanganya watu hapa JF.
 
Aliposema wakristo wasikubali kuwa walinda makaburi hizo ni dharau

Wakristo wengi wameajiriwa na serikali kwa kazi ya kulinda makaburi nchi nzima

Kadharau kazi ya kulinda makaburi na wenye kazi hiyo ambao ni wakristo
Umesoma biblia kujua walinda makabuli walikuwa kina nani? Au unaropoka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…