Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama amesema Tajiri Yusuf wa Almathaya ndio aliyemzika Yesu katika kaburi lake la kifahari
Kimaro amesema Kanisa linawahitaji Matajiri kwa sababu ndio wanaoliondolea Kanisa aibu Wakati wa uhitaji
Hivyo tusiwape majina mabaya Matajiri kwa kuwaita Mafisadi, Wahujumu Uchumi au Freemason Kwani utajiri ni baraka hata katika level ya familia Kwani ndio wanaofuta aibu za familia, amesisitiza mchungaji Kimaro
Kimaro amesema Watu wengi ni walinzi tu wa makaburi kama wale Walinzi wa Pilato waliotumwa kulinda kaburi la Yesu, hivyo wewe kama mkristo usikubali kuwa Mlinda makaburi
Nawatakia Pasaka Njema!
hii haimaanishi hawakupenda kumzika au walimtelekeza, kimaro ni mpotoshaji sana, anatafuta kufungiwa tena. kumiliki kaburi enzi hizo halikuwa jambo dongo manake lilihusisha kumiliki ardhi hapo unapochimba kaburi. wanafunzi wa Yesu hawakuwa matajiri, wengi walikuwa wavuvi na watu wa kawaida na walipoteza muda wao mwingi kuhubiri na Yesu hawakuwa matajiri, Yesu mwenyewe hakuwa tajiri ndio maana hata walipoombwa kodi ya kaisari alimwambia petro akavue samaki atakuwa mdomoni mwake kuna dinari ya fedha wakatoa sadaka kwa kaisari.
huwezi kuchimba tu popote, ndio maana Yusufu tajiri alishanunua kipande pale na akachimba kaburi lake, na kwasababu alikuwa mwanafunzi wa siri wa Yesu, aliamua kuuomba mwili akazika kwenye kaburi alilokuwa ameshalichimba. kina petro na wengine wangechimba lingine la nini sasa wakati tayari limetolewa?
na hata petro na wenzake wangekuwa wamemkimbia nisingeshangaa manake Yesu alikufa kifo cha aibu mno na wanafunzi wake walikuwa terrified, kama kweli walikimbia haimaanishi hawakupenda kumzika. alikufa kifo cha aibu na cha kutisha na wanafunzi nao walihofia kukamatwa kuwekwa msalabani. kimaro awe makini na mahubiri matamu ambayo hayaokoi, no wonder walimsimamisha. anawaza tu hela hela all the time. kwani kuzikwa ni nini hata angezikwa kimasikini unafikiri asingefufuka?
vilevile, Yesu kuzikwa na tajiri ilishatabiriwa na Isaya 53, pale lilikuwa linatimia Neno tu la Mungu. manake kama Neno lisingeandikwa, basi pengine masikini wangemzika. msimsikilize kimaro, Yesu alizikwa na tajiri ili kutimiza unabii wa Isaya 53 na kila maisha aliyoishi alikuwa anaishi akitimiza aliyoandikiwa. makanisani hatuhitaji tajiri, tunahitaji watu walioamua kumfuata Mungu, tunahitaji watu wanaomwabudu Mungu, awe tajiri au masikini wote mbingi inatuhitaji.
shida kubwa ya kimaro ni kwamba hajaokoka na mahubiri yake anatumia elimu ay dunia hii na akili ya kibinadamu, hahubiri kwa Roho Mtakatifu ndio maana siku zote anahubiri mahubiri ya kupendezesha watu na motivations, hayo yanajenga mwili ila sio roho.