Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Ila naona hata undugu utapungua sana sasa, Msigwa akipata tu shida kuanzia sasa Mh. Rais hawezi kabisa msaidia kwa hili lililotokea, na hata ingefaa Msigwa angetoa neno la shukrani kwa Mh. Rais, sasa hizo hela zikirudishwa kwa Mh. Rais navyojua hatakubali tena kutoa msaada hata huko kwao nyumbani, sbb atasema niliingiwa na huruma nikatoa msaada baada ya ndugu zenu kunijia, ila nikapata fedheha. Yaani Msigwa shauri yake
Uliambiwa na nani kuwa Mch. Msigwa huwa anaishi kwa misaada ya Magufuli!!!?
 
JPM kamlipia faini? Kwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiufupi ni kwamba, mtoto wa JPM ameoa mtoto wa dada yake Msigwa. Inaonekana ndugu wa Msigwa wameenda kuomba msaada kwa JPM wakiwa na kianzio cha 2M.
Sasa hawa ndugu, kwanini hawakuipeleka ofisi za CDM hiyo 2M ili iunganishwe na michango mingine ya wananchi kumtoa ndugu yao?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa kubwa kafanya rais. Ukishakuwa mtu mkubwa, kiongozi wa nchi hupaswi hata kidogo kuonyesha upendeleo kwa familia yako na ndugu zako. Nyetere alikemea sana hili. Rais ni baba wa watanzania wote na teye ndite custodian wa hazina yote ya nchi. Sasa akianza kufanya vitendo kama hivi inatilia madhaka uadilifu wake. Kwa nafadi yake alipaswa haya kama ni kusaidia afanye kimya kimya isijulikane. Lakino yeye kaona kutangaxa ni sifa kumbe inamharibia. Ni watanzania wangapi wapo magereza wakiwa wameshindwa kulopa faini? Kwa hiyo wao wataozea magereza kwa sababu hawana undugu na rais? Hii ilikuwa move ya hovyo sana.
By the way, mbona michango ilokuwa inaenda vizuri tu huko chadema na hakina mahali walitangaza wameshindwa kipata pesa ya kutosha kuwatoa. Hiki kihetehere cha nini? Kwa kweli washaurivwa rais wamemuaibisha!
Great thinking, thanks
 
Yaani mnifunge halafu mtake kuchukulia ujiko kutoka kwangu!!!!
Mbona CCM ina michezo ya kitoto sana?? Hii CCM inaelekea wapi?

..hii michezo ya KIJINGA anafanya Gerson Msigwa na Humphrey Polepole.

..kama Jpm alichangia kama familia hakukuwa na haja ya Gerson Msigwa na Muhidin Michuzi kumrekodi kaka yake Mch.Msigwa.

..Na hakukuwa na sababu yoyote ya Humphrey Polepole kwenda segerea kumchukua Mch.Msigwa. Familia wangeachiwa wafanye kila kitu.
 
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa amekataa kupanda gari la serikali lililopelekwa gerezani Segerea ili kumchukua baada ya kulipiwa faini.

Awali kulitokea mzozo kati ya wafuasi wa CCM wakiongozwa na Ndugu Humphrey Polepole ambao walitaka Msigwa apande gari ya serikali kwa madai kuwa amelipiwa faini yake na Rais JPM, lakini wafuasi wa Chadema wakamtaka apande gari aliloandaliwa na Chadema kwa kuwa chama hicho ndicho kimemlipia faini kupitia michango ya watanzania.

Wafuasi hao walidai kwamba wakati Rais JPM anapeleka fedha tayari Chadema ilikua imeshamlipia Msigwa na hivyo fedha hiyo irudishwe kwa Rais ili ikafanye shughuli nyingine za maendeleo.

Kufuatia mzozo huo wafuasi wa Chadema walizuiwa kuingia gerezani humo na wafuasi wa CCM wakiongozwa na Polepole waliingia wakiwa kwenye magari ya serikali tayari kumlaki Msigwa.

Lakini Msigwa alikataa kupanda gari ya serikali aliyoandaliwa na kutembea kwa mguu hadi nje ya gereza walikokuwa wafuasi wa Chadema ambao wamemlaki kwa shangwe na sasa anaelekea makao makuu ya Chadema, eneo la Kinondoni ili kufanya mkutano na wanahabari.!
Ukweli ni upi, CHADEMA ndio wamelipia faini au Rais Magufuli? Je, kuna ushahidi CCM ilipeleka gari la Serikali kumchukua Msigwa kutoka gerezani, kiongozi akiwa Polepole? Taarifa ifuatayo inatoa jibu.

 
Ukweli ni upi, CHADEMA ndio wamelipia faini au Rais Magufuli? Je, kuna ushahidi CCM ilipeleka gari la Serikali kumchukua Msigwa kutoka gerezani, kiongozi akiwa Polepole? Taarifa ifuatayo inatoa jibu.

Ushahidi mwingine nani kalipa faini ya Msigwa

 

Attachments

  • ES7EmC5XQAANYFD.jpeg
    ES7EmC5XQAANYFD.jpeg
    103.7 KB · Views: 1
  • ES7Em4FXkAAGxLJ.jpeg
    ES7Em4FXkAAGxLJ.jpeg
    79.8 KB · Views: 2
Me mwenyewe najiuliza. Hili ni jambo la kichama, inakuwaje gari za serikali zihusike kwenye issue hii? Je pole pole ni kiongozi mwandamizi wa serikali au wa chama? Kwa hiyo kodi yetu inatumika kwa issue za chama ama zinapaswa kutumika kwenye shughuli za kiserikali?
Matumizi mabovu ya mamlaka na Mali za umma.Magari ya serikali ya nini huko na Polepole ni kiongozi wa chama au?
Hongera Mch.Msigwa,huo ndiyo uzalendo unaotakiwa,siyo hao waigizaji.Hii inaonyesha mikakati iliyoandaliwa kupitia kesi hii na hukumu yake.Wameshindwa na kulegea.Aibuuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila naona hata undugu utapungua sana sasa, Msigwa akipata tu shida kuanzia sasa Mh. Rais hawezi kabisa msaidia kwa hili lililotokea, na hata ingefaa Msigwa angetoa neno la shukrani kwa Mh. Rais, sasa hizo hela zikirudishwa kwa Mh. Rais navyojua hatakubali tena kutoa msaada hata huko kwao nyumbani, sbb atasema niliingiwa na huruma nikatoa msaada baada ya ndugu zenu kunijia, ila nikapata fedheha. Yaani Msigwa shauri yake
Kwanini unawaza matatizo kwa Msigwa tu?Huyo JPM mwenyewe hawezi kupata shida?Halafu msaada gani wa masharti namna hiyo?Ingetosha tu kulipa na kutoa taarifa kwa wahusika,ila unalipa unaita vyombo vya habari,unamtangaza kuwa umemlipia,unaenda gerezani na makamera kumpokea pamoja na makada wa CCM !Sasa huo ni msaada au unataka umtumie ndugu yako kwa malengo yako binafsi?Hata mimi ningekuchenga!!!
 
Back
Top Bottom