Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Yote ya yote Mimi na familia yangu nafaidika na serikali ya ccm kwa kuwa inanilipa mshahara, na Kuna wengine humu wanafaidika na chadema kwa kuwa inawalipa mshahara, sifungamani na upande wowote, na Kura yangu itabaki kuwa siri. Japo CCM hawajawah kupata Kura yangu since 95.

Hii michezo ya kisiasa ninayoiona Ni ya KIJINGA SANA KUPATA KUTOKEA
Wanaokulipa ni wananchi sio serikali ya ccm
 
Hii habari imeishachuja! Rais ALIOMBWA NA NDUGU WA MSIGWA awasaidie mchango wa kumlipia ndugu yao kutoka jera! Rais alikuwa anatekeleza ombi la hao wazee hivyo mambo ya alikuwa kaishalipiwa hama la!! hayamuhusu Rais!
Walimuomba lini? na kupitia wapi? na polepole alifuata nini? chezeni michezo ya kikubwa basi achaneni na ya kitoto
 
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa amekataa kupanda gari la serikali lililopelekwa gerezani Segerea ili kumchukua baada ya kulipiwa faini.

Awali kulitokea mzozo kati ya wafuasi wa CCM wakiongozwa na Ndugu Humphrey Polepole ambao walitaka Msigwa apande gari ya serikali kwa madai kuwa amelipiwa faini yake na Rais JPM, lakini wafuasi wa Chadema wakamtaka apande gari aliloandaliwa na Chadema kwa kuwa chama hicho ndicho kimemlipia faini kupitia michango ya watanzania.

Wafuasi hao walidai kwamba wakati Rais JPM anapeleka fedha tayari Chadema ilikua imeshamlipia Msigwa na hivyo fedha hiyo irudishwe kwa Rais ili ikafanye shughuli nyingine za maendeleo.

Kufuatia mzozo huo wafuasi wa Chadema walizuiwa kuingia gerezani humo na wafuasi wa CCM wakiongozwa na Polepole waliingia wakiwa kwenye magari ya serikali tayari kumlaki Msigwa.

Lakini Msigwa alikataa kupanda gari ya serikali aliyoandaliwa na kutembea kwa mguu hadi nje ya gereza walikokuwa wafuasi wa Chadema ambao wamemlaki kwa shangwe na sasa anaelekea makao makuu ya Chadema, eneo la Kinondoni ili kufanya mkutano na wanahabari.!
Hivi ni kweli Rais anahusika kwa hiki? Mbona naona ni siasa za kishamba ndizo zinazoendelea. Mwaka huu tutaona mengi ya hovyo yakifanyika.
 
Yote ya yote Mimi na familia yangu nafaidika na serikali ya ccm kwa kuwa inanilipa mshahara, na Kuna wengine humu wanafaidika na chadema kwa kuwa inawalipa mshahara, sifungamani na upande wowote, na Kura yangu itabaki kuwa siri. Japo CCM hawajawah kupata Kura yangu since 95.

Hii michezo ya kisiasa ninayoiona Ni ya KIJINGA SANA KUPATA KUTOKEA
Acha fikra za darasa la nne. Mishahara yote tunakulipa sisi wananchi tunaotoa kodi. Na hao unaowasifu eti wanakulipia wangekuwa kweli wanakupenda ungeshakuwa na mshahara mara 4 ya uupatao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom