Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Uliambiwa na nani kuwa Mch. Msigwa huwa anaishi kwa misaada ya Magufuli!!!?
 
JPM kamlipia faini? Kwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiufupi ni kwamba, mtoto wa JPM ameoa mtoto wa dada yake Msigwa. Inaonekana ndugu wa Msigwa wameenda kuomba msaada kwa JPM wakiwa na kianzio cha 2M.
Sasa hawa ndugu, kwanini hawakuipeleka ofisi za CDM hiyo 2M ili iunganishwe na michango mingine ya wananchi kumtoa ndugu yao?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Great thinking, thanks
 
Hii siasa kweli yaani chadema waanze na kumtoa msigwa bila mwenyekiti wake na katibu mkuu ambao ndo wenye majukumu makuu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mnifunge halafu mtake kuchukulia ujiko kutoka kwangu!!!!
Mbona CCM ina michezo ya kitoto sana?? Hii CCM inaelekea wapi?

..hii michezo ya KIJINGA anafanya Gerson Msigwa na Humphrey Polepole.

..kama Jpm alichangia kama familia hakukuwa na haja ya Gerson Msigwa na Muhidin Michuzi kumrekodi kaka yake Mch.Msigwa.

..Na hakukuwa na sababu yoyote ya Humphrey Polepole kwenda segerea kumchukua Mch.Msigwa. Familia wangeachiwa wafanye kila kitu.
 
Ukweli ni upi, CHADEMA ndio wamelipia faini au Rais Magufuli? Je, kuna ushahidi CCM ilipeleka gari la Serikali kumchukua Msigwa kutoka gerezani, kiongozi akiwa Polepole? Taarifa ifuatayo inatoa jibu.

 
Ukweli ni upi, CHADEMA ndio wamelipia faini au Rais Magufuli? Je, kuna ushahidi CCM ilipeleka gari la Serikali kumchukua Msigwa kutoka gerezani, kiongozi akiwa Polepole? Taarifa ifuatayo inatoa jibu.

Ushahidi mwingine nani kalipa faini ya Msigwa

 
Me mwenyewe najiuliza. Hili ni jambo la kichama, inakuwaje gari za serikali zihusike kwenye issue hii? Je pole pole ni kiongozi mwandamizi wa serikali au wa chama? Kwa hiyo kodi yetu inatumika kwa issue za chama ama zinapaswa kutumika kwenye shughuli za kiserikali?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini unawaza matatizo kwa Msigwa tu?Huyo JPM mwenyewe hawezi kupata shida?Halafu msaada gani wa masharti namna hiyo?Ingetosha tu kulipa na kutoa taarifa kwa wahusika,ila unalipa unaita vyombo vya habari,unamtangaza kuwa umemlipia,unaenda gerezani na makamera kumpokea pamoja na makada wa CCM !Sasa huo ni msaada au unataka umtumie ndugu yako kwa malengo yako binafsi?Hata mimi ningekuchenga!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…