Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huko ndiko kukomaa kisiasa kwa Chadema, jambo ambalo CCM ni marufuku kukata rufaa.
 
Hapo Mbeya nani anauzika zaidi ya Sugu mtaje hapahapa. Kwamba huyo mtu wako akisimama dhidi ya Sugu anamshinda
 
Kadanganye wajinga wenzio huko kwenye vijiwe vya mama John na Ilemi na Mabatini. Sugu hana mchango wowote kwenye upanuzi wa hizo hospitali na hakuwa na uwezo wa kumshawishi ULISUBISYA.

Yeye ni mtu wa yoyo man tu na kugongesha bangi vijiweni
 
Hapa tunaongea lugha moja. Akigombea ubunge Mbeya mjini hatiboi
 
Alichofanya Msigwa ni haki yake, kama hajaridhishwa na namna Sugu alivyoshinda na ana sababu za mantiki kupinga ushindi wake, sioni ubaya wowote kwa Msigwa kukata rufaa.

Simply anachofanya Msigwa anataka haki ifuatwe, kama KK itaamua kumpa ushindi Sugu au kumpoka, bado sioni kama kuna jambo zito la kupigania hapo.

Sijui huko Chadema labda mwenyekiti wa kanda anapokea mshahara kwa hiyo nafasi, lakini kwa namna navyoona mambo yanaenda, binafsi sioni sababu yoyote ya kuwepo na ugomvi kati ya hao wawili, nachokiona ni muendelezo wa kuonesha ukomavu wa demokrasia.

Demokrasia haipo tu pale kwa Msigwa kukubali kushindwa, atakubali kushindwa kama kweli anaona ameshindwa kihalali, lakini kama anatilia shaka ushindi wa mwenzake sioni sababu kwanini asipiganie haki yake.
 
Kukata Rufaa ndio unaitisha Press nyumbani kwako?

Huyo ameshaaga 🐼
 
Hapo Mbeya nani anauzika zaidi ya Sugu mtaje hapahapa. Kwamba huyo mtu wako akisimama dhidi ya Sugu anamshinda
Wangekuwa hawapo basi kusingekuwa na zoezi la kuchukua fomu za uteuzi ndani ya chama. Yaani mtu angepita tu. Siwezi kuwataja sasa wenye uwezo bali subiri wakati mwafaka utawaona. Kuwataja sasa hivi ni kuwaharibia
 
Katiba ya Chadema inatakiwa kuzingatiwa kama hamjui kuendesha chama mkodi watu kutoka CCM wawasaidie uchaguzi ndani ya Chadema ni suala la kikatiba kukata rufaa sio kitu Cha kwenda kwenye vyombo vya habari
Yaani cdm wakafundishwe na hicho chama kinachoprint fomu Moja?! Siku cdm watakosea eti wajifanye wanapewa darasa la uongozi na ccm, nitawadharau kupita maelezo.
 
Yaani cdm wakafundishwe na hicho chama kinachoprint fomu Moja?! Siku cdm watakosea eti wajifanye wanapewa darasa la uongozi na ccm, nitawadharau kupita maelezo.
Mumeshindwa kuweka ukomo wa mtu kushika Cheo kikubwa Ona Sasa Msigwa anawasumbua mngeweka ukomo.miaka kumi mfano Msigwa angepisha Wengine mjifinze CCM kuweka ukomo wa mtu kushika cheo
 
Katiba ya Chadema inatakiwa kuzingatiwa kama hamjui kuendesha chama mkodi watu kutoka CCM wawasaidie uchaguzi ndani ya Chadema ni suala la kikatiba kukata rufaa sio kitu Cha kwenda kwenye vyombo vya habari
Wakati Membe amefukuzwa ccm na dhalimu Magu na kuitisha press, mbona hao walimu wa siasa huko ccm hawakujitokeza na kumpa utaratibu wa kukata rufaa?
 
Mumeshindwa kuweka ukomo wa mtu kushika Cheo kikubwa Ona Sasa Msigwa anawasumbua mngeweka ukomo.miaka kumi mfano Msigwa angepisha Wengine mjifinze CCM kuweka ukomo wa mtu kushika cheo
Ccm ukomo uko kwenye cheo cha mwenyekiti tu, na lengo ni Ili mwenyekiti awe rais, Wala sio suala la demokrasia kama unavyotaka tuamini. Ingekuwa Kuna demokrasia tusingeona mwenyekiti wa ccm akaipata kura 100% kinyume na uhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…