Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tunataka mbunge anayeweza kuleta maendeleo.
Mbunge anayaleta maendeleo kutoka wapi? Mbunge alete maendeleo!!!? Hii ni fikra ya kijinga sana. Mbunge ni mwakilishi wa hoja na mawazo ya wananchi. Baaasi!!!

Mbunge hakusanyi kodi wala siyo mfadhili. Hakuna pahala mbunge anaweza kuyabeba maendeleo ili awaletee wananchi.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)...
Huyu naye?

Haelewi kuwa kila lenye mwanzo halikosi mwisho, kakaa na hiko cheo kwa muda gani?

Kuna nini cha kung'ang'ania hadi mikesi kwenye uenyekiti huo wa kanda?

Asitufanye tuanze kunusanusemo!

Na pia aelewe kama kuna rough ya ngawila, basi rough hiyo hiyo itachezwa tena kwenye vikao vya maamuzi ama mahakamani kwa jinsi nchi yetu ilivyokuwa currupt kila kona.

Hapo anawatafutia tu watu ulaji pamoja na missunderstandings zisizokuwa na ulazima wowote.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)

Ametangaza kukata rufaa kwenye Kamati Kuu ya Chama chake kupinga ushindi huo wa Sugu, bado haijajulikana kama Kamati Kuu ikiridhishwa na Madai yake nini kitatokea, Sugu atanyang'anywa Ushindi na kupewa Msigwa au Uchaguzi utarudiwa

Binafsi nampongeza Mchungaji huyu kwa uamuzi wake huu, maana hii ndio njia Sahihi iliyowekwa na Chama chake ya kudai haki.

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Kumekucha: Mchungaji Msigwa amkataa John Mrema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi Kanda ya Nyasa

- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa

Hapo ndio unaona umuhimu wa demokrasia kwa vitendo sisiemu usiporidhika unatakiwa uhame na hili ndio mmelileta hata kwa tume ya uchaguzi hamtaki matokeo ya urais yapingwe hata kama kuna kasoro
 
Na huyu jamaa (John mrema) mbona amekaa muda mrefu sana kwenye hiki cheo?
Kumbe ulikuwa hujui ,ni shemeji yake Mzee mbowe ,mkee wa Mrema katoka kwa akina Mbowe
 
Huyu naye?

Haelewi kuwa kila lenye mwanzo halikosi mwisho, kakaa na hiko cheo kwa muda gani?

Kuna nini cha kung'ang'ania hadi mikesi kwenye uenyekiti huo wa kanda?

Asitufanye tuanze kunusanusemo!

Na pia aelewe kama kuna rough ya ngawila, basi rough hiyo hiyo itachezwa tena kwenye vikao vya maamuzi ama mahakamani kwa jinsi nchi yetu ilivyokuwa currupt kila kona.

Hapo anawatafutia tu watu ulaji pamoja na missunderstandings zisizokuwa na ulazima wowote.
Embu muulize Mzee Mbowe kwa nini ni Mwenyekiti kwa miaka thelathini?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa aliyemaliza muda wake na kushindwa katika Uchaguzi uliompa ushindwa Joseph Mbilinyi (Sugu), Mchungaji Peter Msigwa amekata rufaa kupinga Uchaguzi huo akidai ulivurugwa
-
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Msigwa amesema Uchaguzi huo ulitawaliwa na Mbinu Chafu ikiwa ni pamoja na Wasimamizi wa Uchaguzi kuwazuia Makatibu Watatu wa Mabaraza kupiga Kura kinyume na Katiba ya Chama hicho

#JamiiForums #Democracy #JFDemocracy #CivilRights
Mod kuna uzi nilishwahi kuleta humu kuhusu Msigwa ,hastahili kuwepo kwenye hiki chama ambapo kwa ujengaji wa hoja hakuna mwanchadema yoyote anaeweza kumfikia ,Ni bahati mbaya sana akili kubwa kama Msigwa yupo kwenye genge la Wachagga
 
Urafiki wa Msigwa na ASAS una historia ndefu tangu 1980s hivyo kumfadhili siyo kumnunua
Nasubiri tu sasa kusikia neno toka kwa Mwenyekiti juu ya haya yote ili nikamilishe ile 'hypothesis' niliyoanza kuijengea hoja baada ya mazungumzo ya maridhiano.
Ujanja wa Mwenyekiti nadhani umefikia kikomo sasa, sidhani kuwa bado anazo mbinu zaidi ya hizi alizozitumia kwa muda mrefu kuzubaisha watu.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)

Ametangaza kukata rufaa kwenye Kamati Kuu ya Chama chake kupinga ushindi huo wa Sugu, bado haijajulikana kama Kamati Kuu ikiridhishwa na Madai yake nini kitatokea, Sugu atanyang'anywa Ushindi na kupewa Msigwa au Uchaguzi utarudiwa

Binafsi nampongeza Mchungaji huyu kwa uamuzi wake huu, maana hii ndio njia Sahihi iliyowekwa na Chama chake ya kudai haki.

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Kumekucha: Mchungaji Msigwa amkataa John Mrema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi Kanda ya Nyasa

- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa

- Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Sikuingia CHADEMA kutafuta Vyeo bali Kuwatumikia Wananchi, nitaendelea kukitumikia chama Katika Jimbo lolote mtakalonihitaji!

Why this!??
Halina afya jambo hili!?
 
Embu muulize Mzee Mbowe kwa nini ni Mwenyekiti kwa miaka thelathini?
Kwanini mnataka aondoke? Mna maslahi gani na kuondoka kwake? chadema ife? Waje akina Mwambe? Ngoja tupate katiba ambayp Rais hatakuwa Sultani/ Malkia. Hatakuwa na pesa za kuchota toka hazina kununa wapinzani, then Mbowe can go!
 
Kumbi ziko za kutosha lakini angeenda kuongelea kwenye ofisi za chama!
Lakini mbona watendaji wa chama eneo hilo alikuwa nao hapo hapo, au ofisi nzima ya chama wanaondoka naye?
CHADEMA wachezewe akili na mahasmu wao na bado wasitambue, mbona hili litakuwa jambo la kushangaza sana!
 
Ni AIBU kubwa kwa CHADEMA kumchagua Sugu badala ya Peter Msigwa. Hata mukiniambia kuwa Sugu alikuwa na fedha chafu na kagawa kwa wajumbe, fedha unapokea lakini kura unapiga kwa kutumia akili yako.

Naiombea hiyo rufaa ipite ili IWASAFISHE CHADEMA.

Unamuachaje mtu kama Msigwa ana madini, amenyooka, hanunuliki na ana VISION na kwenda kumpa kura mvuta bangi, mtu wa matusi, mvaa mlegezo??

Mimi SIYO CHADEMA ila you people ARE NOT SERIOUS!!

Kwa taarifa yenu, mukirudia makosa haya kwenye Ubunge wa Mbeya Mjini mkamismamisha SUGU 2025, JIMBO MNALIPOTEZA.

TULIA hakubaliki Mbeya ukiacha maeneo ya Uyole, Itezi, Igawilo na Iduda anakogawa hela na T-shirt. Lakini zile kata asilia za Mbeya Mjini yaani kuanzia Mwakibete hadi Iyunga, Sisimba, Mwansekwa Tulia Ackson si lolote.

Tafuteni mtu anayeuzika ila siyo SUGU
Abdul
 
Unaweza ukawa na haki na kweli. Lakini kwa hali iliyopo ambapo CCM/serikali inatafuta upenyo wa kuiua chadema, usingelifanya hivyo. Umewapamaadui wa chadema mahali pa kuania. Unadhani covid 19 sasa hivi wana furaha kiasi gani?

MSIGWA Hapa umekosea.

WACHUNGAJI HAWAFANYI HIVI
 
Jamaa anafikiri Mbowe amekuwa mwenyekiti miaka yote hiyo bila hila!!? Watu wenye nguvu za kutishia maslahi yake lazima awapoteze.
 
Mbunge anayaleta maendeleo kutoka wapi? Mbunge alete maendeleo!!!? Hii ni fikra ya kijinga sana. Mbunge ni mwakilishi wa hoja na mawazo ya wananchi. Baaasi!!!

Mbunge hakusanyi kodi wala siyo mfadhili. Hakuna pahala mbunge anaweza kuyabeba maendeleo ili awaletee wananchi.
Hii ni nadharia ya CCM ili kuwapumbaza wananchi. Mbunge hata siku moja hashuhuliki kuleta maendeleo.Mbunge kazi yake ni kusimamia serikali kuhakikisha inaleta maendeleo.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom