Jibu ni HAPANA, sijaiona hiyo 'press conference' ya Msigwa, na ni muhimu kuwa sina nia kabisa ya vitu vya aina hiyo tena toka huyo jamaa ajiondoe akili kichwani.
Msigwa sikuwahi kuwa na matumaini makubwa naye sana, toka siku nyingi; pamoja na kwamba baadhi ya matukio, kama yale yaliyofanyika chini ya Magufuli, yalichanganya akili kidogo juu yake.
Sasa kinacho umiza kichwa, ni kuona dalili zile zile toka ndani ya chama kilicho tegemewa kutuondolea uozo kama huu unao utaja kufanyiwa mchungaji, udhalilishaji!
Sasa haitakuwa udhalilishaji wa mtu mmoja mmoja kama huyo Mchungaji, chama kizima kitadhalilishwa!.
Najua, wakati huo utakapo wadia, kutakuwa na tungo za ngonjera nyingi sana za kupindisha akili za wanao taka kupindisha akili.
Taratibu tunaanza kuyaona haya.