Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014

Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014

CCM imetia aibu kwa lipi? Kilichofanyika leo kimetoa mwanga kwa kila mtu. CCM imeuanzisha mchakato wa katiba na itaumaliza salama salmini
Kweli wametoa mwanga kwa ccm na wafuasi wake wote ni vibaka wa mchakato huu wa katiba kwa kukataa kufata kanuni na kujadili hoja ambayo haiko mezani.
Wote tumepata huo mwanga.
 
hawezi towa maelezo yoyote maana ukweli umedhihili ni kamati kuu ya ccm iliandaa.

serikali nzima ilikua pale. tamthilia nyingine bana zinachekesha kweli.tena kwa hustadi mkubwa sana na kujitapa bw lukuvi anasema tunakwenda kuimalizia katiba na kuwapatia watanzania katiba nzuri. kweli nimegundua anguko la farao ccm limewadia kwenye sanduku la kura 2015 hawata pona kwa hili.
 
Waliokuwa wanafuatilia mdahalo wa Leo wamemuona lukuvi akiongea kwa jeuri na kejeli nyingi na kusema hata huyo warioba kaleta mapendekezo mapya ya kuongezwa kwenye rasimu aliyo isimamia mpaka imepatikana.
Kesho kutakuwa na mdahalo mwingine na Mzee warioba atakuwepo tunakuomba Mzee wetu uje uthibitishe hili kwa sababu ccm kwa propaganda awajambo kwa sababu wamesomea.
 
Huyo mwigulu ni mnafiki tu. Yeye kwani hakulijua hilo
 
Nini? Sijaelewa hili!

quote_icon.png
By ntahagaye

mh. lukuvi amedai kuwa mzee warioba amepeleka mapendekezo mapya mengine juu ya katiba Mpya


Kesho tutaelewa propaganda, ukweli na uwongo, Warioba, polepole na salimu wanaattend mdahalo wao

watakuwa nanafasi nzuri kufafanua jambo hili.
 
kwa mengi lakini lakuudhi zaidi

Ni kada wa ccm, waziri ofisi ya rais W. Lukuvi

Pamoja na mawazo ya wasomi na wantazania wengine anasema wao (ccm) wanaenda kupitisha maamuzi.


Huu ni zaidi ya ujinga, anajifanya anamadaraka na maamuzi zaidi ya watanzania? anadhani hili taifa nila ccm peke yake?

Huko nikutia aibu yaani Maamuzi ya ubabe, lazima na udikiteta.
Yap...kwani kasema uongo? Hapo kuna aibu gani? Kumbuka CCM imepewa dahamana na wananchi ya kuiongoza hii nchi. Na nchi yetu wananchi wengi ni CCm.Wao kama wawakilishi wa wananchi...maamuzi yao ni sahihi. CCM inachokifanya ni kuheshimu tu maoni ya wachache(minority) ndio maana tunawasihi UKAWA warudi bungeni
 
Kwa mara ya kwanza leo nimemsikiliza na kumuelewa koz hajasimamia upande mmoja na hivyo ndivyo anavyotakiwa kuwa kiongozi......kwangu mie nampa point 1 bado 99 zinamsubiri maana nyingi zimejikita kwenye mikakati yake ya chini kwa chini

Hongera kwa leo maana siasa sio ugonvi

kiukweli hata Mimi tangu nizaliwe nileo nimemuona mwiguru ameongea maneno ya maana
 
Hapa nimeona wanafunzi wa vyuo mbalimbali hasa IFM nadhani watakuwa wameletwa, walichokosea sana ni zomeazomea na kupigia makofi vitu ambavyo si vya msigi.

ndg kuna wakati mwingine unaweza kufikiria hivi ni nani ametuloga wagalatia {galatia 3:1}??? maana kuna mambo mengine hata mungu mwenyewe anatushangaa. na muunga mkono askofu kakobe 100%100 wakati mwingine watanzania tunatakiwa kutolewa pepo. maana wazi wazi watawala wanaminya maoni yetu alafu cc tunawashangilia? yaani hata ccm wanatucheka kama manamba.
 
Watanzania bado tunacheza tu ngoma ya wapigania Madaraka aisee! Lait kama tutayazangitaia waliyoyaongea Kitila na Mpangala naamini tutajikwamua hapa tulipokwama.
 
Yap...kwani kasema uongo? Hapo kuna aibu gani? Kumbuka CCM imepewa dahamana na wananchi ya kuiongoza hii nchi. Na nchi yetu wananchi wengi ni CCm.Wao kama wawakilishi wa wananchi...maamuzi yao ni sahihi. CCM inachokifanya ni kuheshimu tu maoni ya wachache(minority) ndio maana tunawasihi UKAWA warudi bungeni


1. wamepewa dhamana ya kuandaa katiba?

2. Dhamana hii wamepewa wakati gani endapo kura 2010 ziliombwa kwa ilani ambayo haikuwa na suala la katiba?

katiba sio sera wala halikuwepo kwenye ilani ya ccm, niwanchigani mnawakilisha kwa kitu ambacho sio chenu?
 
Kweli wametoa mwanga kwa ccm na wafuasi wake wote ni vibaka wa mchakato huu wa katiba kwa kukataa kufata kanuni na kujadili hoja ambayo haiko mezani.
Wote tumepata huo mwanga.
Tatizo Tundu lishu ameshawalisha mavi. Kila kitu mnaona mnaonewa na kila kitu mnaona kimebadilishwa. BTW mpinzani aachi asili...kila kitu kazi yake ni kupinga regardless kina manufaa kwake au hakina
 
kinachonishangaza sana mimi ni kile kitendo cha akina wasira na lukuvi kujiweka kwenye nafasi ya kujiona kwamba Tanzania ni yao na wao ndio wenye uwezo wa kuamua watakavyo
 
Utafanyika kituo gani na saa ngapi?huo sio wa kukosa@zamlock
 
Mh. Lukuvi amesema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya rasimu ya katiba jaji Simbe Warioba, amepeleka maoni ya nyongeza serikalini na kuomba yakajadiliwe BMK.
Hayo maoni YAKAJADILIWE? na ameyatoa wapi? Inaruhusiwa yakajadiliwe kule BMK?
 
Back
Top Bottom