Zamani vita, utumwa na ukoloni zilikuwepo kwenye jamii nyingi karibu zote hapa duniani na yule ambaye ni mnyonge ndio alikuwa wakuonewa.
Hata USA alipitia ukoloni, ila leo hii ndio super power.
Ukoloni ni Excuse ya waafrika wazembe na wavivu.
Ambao hadi leo mna karibu miaka 63 ya kujiongoza na kujitawala wenyewe, ila hakuna kilichofanyika kwa ufasaha zaidi ya maraisi wa kiafrika kulia lia njaa na kutembeza bakuli kuomba misaada na mikopo kutoka kwa wazungu.
Hapa Afrika tu jamii nyingi sana zilikuwa zinapigana, zinauana na kunyang'anyana ardhi.
Kwanza leo hii hapa Afrika ukoloni bado unaendelezwa, Mfano wale wa Masai wa Ngorongoro wamefukuzwa kijanja kwenye ardhi yao.
Watu wengi tu hapa Afrika wanamiliki ardhi kinyamera bila hata kufuata utaratibu na sheria.
Ndio maana kesi za mashamba, viwanja ni endless kwa Afrika.