Mdude CHADEMA: Hii katiba haifai, Wazanzibari wanakuwa wakuu wa wilaya Tanzania bara huku Watanganyika hawaruhusiwi kuwa wakuu wa wilaya Zanzibar

Mdude CHADEMA: Hii katiba haifai, Wazanzibari wanakuwa wakuu wa wilaya Tanzania bara huku Watanganyika hawaruhusiwi kuwa wakuu wa wilaya Zanzibar

Mtanzania yeyote akiishi Zanzibar kwa miaka 5 mfululizo anakuwa Mzanzibari. Ila ni sheria za ajabu sana za kumpokonya uraia mtu kwa kuwa haishi huko. Kama Uzanzibari waweza kuitwa uraia.
Asante sana mkuu. Na mimi nilifikiri kuwa kuna masharti ya ukaazi yanayoweza kumpa mtu wa bara Uzanzibari, lakini nikatukanwa kwamba sijui kitu hapa.

Zanzibar haina uraia, kwa sababu si nchi kamili. Uraia ni jambo la Muungano, kuna uraia wa Tanzania tu. Uraia wa Zanzibar ulikufa baada ya Muungano, kama uraia wa Tanganyika.

Kule kuna ukaazi tu.

Nafikiri ukaazi huu, angalau kinadharia tu, unafanya hii distinction ya "Mzanzibari" isiwe na maana kubwa.

Kwa sababu, in theory, kila Mtanzania anaweza kuwa Mzanzibari, sema kuna wengine wamezaliwa Zanzibar hawana masharti ya kukaa miaka hiyo inayotakiwa kabla ya kupata ukazi, na wengine wanatoka bara inawabidi wakae miaka hiyo.

Na hiyo miaka imewekwa hivyo, kwa sababu Zanzibar hawataki watu wa bara waende kwa wingi kupiga kura Zanzibar na kubadili matokeo ya uchaguzi bila kuwa wakazi, pamoja na kudhibiti watu wengi wa bara wasije kununua ardhi kwa sana na kuibadilisha Zanzibar.

Sasa, tukimkatalia Shaka kuwa Mkuu wa Wilaya bara, na Mndengereko atakayehamia Zanzibar naye akataliwe kuwa Mkuu wa Wilaya bara?

Wale kina Sepetu kina Wema baba yao alikuwa Zanzibar sana, kina Adam Mwakanjuki wamekaa sana Zanzibar mpaka SMZ walikuwepo.

Hawa nao wapigwe marufuku vyeo vya serikali ya Muungano kama vya ukuu wa Wilaya bara?

Ukianza siasa hizo maana yake nini? Utasema wakuu wa wilaya za Dar wote wawe Wazaramo? Wasije Wabondei kuwa wakuu wa Mkoa wala wilaya Dar?

Hapo hamuoni mnaanza dhambi ya ubaguzi aliyoisema Nyerere (probably akirejea mfano wa Simba walawatu wa Tsavo kutoka kitabu cha "The Man Eaters of Tsavo" cha John Henry Patterson) kuwa ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huachi utabagua watu mpaka kwenye koo na familia?
 
Mzanzibari alimuuwa nani? Mbona nyinyi mlituuwa kwa maelfu katika uvamizi wenu, na kila miaka 5 mnatuletea vifaru na majeshi ya wahutu wa Burundi kuja kumweka kibaraka wenu

..kuwa mkweli.

..Watanganyika hawawezi kuingia Zanzibar wakauwa wananchi bila msaada wa wenyeji Wazanzibari.

..hata ukisema kuwa mapinduzi ni uvamizi, jiulize walioshika madaraka baada ya uvamizi huo ni nani kama sio Wazanzibari?

..Vifaru mnavyoletewa kila baada ya miaka 5 si kwa ajili ya kusimika Wazanzibar wenzenu madarakani?

..Mimi nashauri kauli zako uzilenge kwa wahusika wanaofanya uovu dhidi yenu, usizielekeze kwa Watanganyika wote.
 
Asante sana mkuu. Na mimi nilifikiri kuwa kuna mashartoi ya ukaazi yanayoweza kumpa mtu wa bara Uzanzibari, lakini nikatukanwa kwamba sijui kitu hapa.

Zanzibar haina uraia, kwa sababu si nchi kamili. Uraia ni jambo la Muungano, kuna uraia wa Tanzania tu. Uraia wa Zanzibar ulikufa baada ya Muungano, kama uraia wa Tanganyika.

Kule kuna ukaazi tu.

N nafikiri ukaazi huu, angalau kinadharia tu, unafanya hii distinction ya "Mzanzibari" isiwe na maana kubwa.

Kwa sababu, in theory, kila Mtanzania anaweza kuwa Mzanzibari, sema kuna wengine wamezaliwa Zanzibar hawana masharti ya kukaa miaka hiyo inayotakiwa kabla ya kupata ukazi, na wengine wanatoka bara inawabidi wakae miaka hiyo.

Na hiyo miaka imewekwa hivyo, kwa sababu Zanzibar hawataki watu wa bara waende kwa wingi kupiga kura Zanzibar na kubadili matokeo ya uchaguzi bila kuwa wakazi, pamoja na kudhibiti watu wengi wa bara wasije kununua ardhi kwa sana na kuibadilisha Zanzibar.

Sasa, tukimkatalia Shaka kuwa Mkuu wa Wilaya bara, na Mndengereko atakayehamia Zanzibar naye akataliwe kuwa Mkuu wa Wilaya bara?

Wale kina Sepetu kina Wema baba yao alikuwa Zanzibar sana, kina Adam Mwakanjuki wamekaa sana Zanzibar mpaka SMZ walikuwepo.

Hawa nao wapigwe marufuku vyeo vya serikali ya Muungano kama vya ukuu wa Wilaya bara?

Ukianza siasa hizo maana yake nini? Utasema wakuu wa wilaya za Dar wote wawe Wazaramo? Wasije Wabondei kuwa wakuu wa Mkoa wala wilaya Dar?

Hapo hamuoni mnaanza dhambi ya ubaguzi aliyoisema Nyerere (probably akirejea mfano wa Simba walawatu wa Tsavo kutoka kitabu cha "The Man Eaters of Tsavo" cha John Henry Patterson) kuwa ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huachi utabagua watu mpaka kwenye koo na familia?

..tatizo ni kuwepo kwa sheria ya ukaazi ya Zanzibar wakati hakuna sheria inayofanana na hiyo huku Tanganyika.

..ili HAKI itendeke inabidi sheria ielekeze kwamba Mzanzibari anapaswa kukaa Tanganyika miaka 5 mfululizo kabla ili aweze kutambulika kama mkaazi.
 
Nakuelewa mkuu.

Ila, tangu mwanzo, muungano umekaa kui protect Zanzibar isimezwe na Tanganyika na haukuona kwamba kuna hofu ya Tanganyika/ Bara kumezwa na Zanzibar.

Kwa mfano, Zanzibar ni sehemu ndogo ambayo watu wa bara wakiamua kuhamia kwa mkumbo inaweza kubadilika ndani ya miaka michache ule uzanzibari ukapotea kabisa, utamaduni, identity etc.

Wakaona kwamba hakuna tishio kama hilo kwa bara, kwamba Wazanzibari wanaweza kuja kujazana bara mpaka wakaijaza na kuibadilisha.

Hiyo ndiyo rationale yao.

Sisemi kwamba naiunga mkono, naielezea tu.

Ukija kwenye mambo ya vyeo, watu wa bara wanaona watu wa Zanzibar wana double dip kwa mtindo wa "chako changu, changu changu". Na hapo ndipo kwenye tatizo.
 
Natoa ushauri kwa CHADEMA watu kama mdude CHADEMA na wengine wenye aina yake ya siasa hawaisaidii CHADEMA Bali wanaiharibia kabisa.

Kwa mujibu wa katiba ,uteuzi wa wakuu wa wilaya unafanywa na Rais kama ulivyo kwa uteuzi mwingine wowote wa kikatiba.

Mfano, aliyekuwa katibu mkuu wizara ya nishati Tanzania bara mhandi Zena, Rais Dkt. Mwinyi alipoingia tu madarakani alimteua kuwa katibu mkuu kiongozi na katibu wa mabaraza la Mapinduzi la Zanzibar, cheo cha juu kwa utumishi wa umma Zanzibar.

Sasa Kama mtanganyika amepewa cheo Cha juu kabisa Cha utumishi wa umma, ni kweli
Mkuu wa wilaya hawezi kuteuliwa?

Acheni upotoshaji CHADEMA mtapoteana mtafute mchawi
Acha uongo, Mhandisi Zena ni Mzanzibari
 
Hakuna mtanzania Nusu. Kwanini watanganyika wanajimilikisha Tanzania?
 
Nakuelewa mkuu.

Ila, tangu mwanzo, muungano umekaa kui protect Zanzibar isimezwe na Tanganyika na haukuona kwamba kuna hofu ya Tanganyika/ Bara kumezwa na Zanzibar.

Kwa mfano, Zanzibar ni sehemu ndogo ambayo watu wa bara wakiamua kuhamia kwa mkumbo inaweza kubadilika ndani ya miaka michache ule uzanzibari ukapotea kabisa, utamaduni, identity etc.

Wakaona kwamba hakuna tishio kama hilo kwa bara, kwamba Wazanzibari wanaweza kuja kujazana bara mpaka wakaijaza na kuibadilisha.

Hiyo ndiyo rationale yao.

Sisemi kwamba naiunga mkono, naielezea tu.

Ukija kwenye mambo ya vyeo, watu wa bara wanaona watu wa Zanzibar wana double dip kwa mtindo wa "chako changu, changu changu". Na hapo ndipo kwenye tatizo.
Hilo swala la identity, utamaduni wangeufany na bara kama ni muhim. Si sawa kupoteza utamaduni wa wachaga kwa kuruhus wahaya kuhamia uchagan huku unalinda utamaduni wa wazanzibar kwa kumminya mtanganyika huko zanzibar.

Mtanzania yoyote lazima awe na haki sawa sehem yoyote nchi.Watafute jina lingine watoe ilo muungano.

Zanzibar ni mkoa haipaswi kuwa na rais.[emoji41]
 
Wazanzibari tumeshawazoea. Wenyewe siku zote ni waumini wa ule msemo wa changu changu, chako changu.

Kiukweli hawa jamaa ifikie wakati wajitawale tu, ili na sisi Watanganyika tupumue.
katiba mpya na nchi yetu Tanganyika irudi ila nahakika mkianza kusema haya mikutano inaweza futwa mapema kabisa inatakiwa muwe wabishi na roho ngumu sio mkitishwa kidogo tu mnakimbilia ubelgiji na kanada
 
utakuta wilaya moja ya huko zanzibar inakuwa na watu mia mbili (200) tu, sasa hao wakuu wa wilaya wanini
Kila mtaa una mbunge, mjumbe wa baraza la wawakilishi na mkuu wa wilaya.
In short Zenji almost every household ina kiongozi, mishahara na marupurupu ni kodi zenu machogo.
 
Hilo swala la identity, utamaduni wangeufany na bara kama ni muhim. Si sawa kupoteza utamaduni wa wachaga kwa kuruhus wahaya kuhamia uchagan huku unalinda utamaduni wa wazanzibar kwa kumminya mtanganyika huko zanzibar.

Mtanzania yoyote lazima awe na haki sawa sehem yoyote nchi.Watafute jina lingine watoe ilo muungano.

Zanzibar ni mkoa haipaswi kuwa na rais.[emoji41]
Mlaumu Nyerere ambaye aliingiza Tanganyika kwenye Muungano huu na Zanzibar bila hata kupata baraka za bunge.

Nimemsoma Profesa Issa Shivji na wenzake hapa wakieleza maisha ya Nyerere kwenye vitabu vyao vitatu vile, nimegundua kwamba Nyerere aliiburuza Tanganyika na Tanzania kuliko nilivyofikiri.

Ubaya au uzuri Watanzania wengi hawasomi tu, wangesoma Nyerere angeonekana mtu tofauti sana kulinganisha na Watanzania wengi wanavyomchukulia.

Yani kuna sehemu hata sera zake za Ujamaa zilipoanza kunawiri kwa nguvu za watu bila kupitia TANU Nyerere alipiga marufuku vijiji vya Ujamaa hivyo kwa sababu tu havikuwa chini ya TANU.

Tuliwekwa kwenye bonge la political experiment na mtu mmoja bila hata ridhaa.
 
Tumieni akili acheni uvivu, ile ni serikali ya Zanzibar, hii ni serikali ya muungano. Ndiyo maana mlishindwa hisabati mapema sana. This is simple logic.
Your "simple logic" is absolutely unlogic because you trying to tell people something you don't know about!!

Nani kakuambia Kila kitu ni cha Muungano? Unajua ma - DC wako chini ya wizara gani?

Kama hujui, tukujulishe kuwa, wako chini ya wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa..

Sasa tuambie hii ni wizara ya Muungano? Kwanini Rais wa JMT hateui wakuu wa mikoa na wilaya kule Zanzibar?

Jibu ni rahisi tu. Hana mamlaka ya kikatiba kufanya vile Kwa mambo yasiyo ya Muungano..!!

Wazanzibar wanapaswa kufanya kazi huku Tanganyika kwenye wizara zile za Muungano tu; mathalani Ulinzi & JKT, Mambo ya nje, Mambo ya ndani nk

Huyu Shaka kama kweli ni Mzanzibar na kawa DC huku Tanganyika, basi yuko hapo kimakosa, ame - trespass na aliyemteua amevunja katiba!!!
 
Halafu kutwa nzima mnalalamika kuwa hakuna ajira wakati wanapewa wazanzibar pambana na hali zenu.
 
Mlaumu Nyerere ambaye aliingiza Tanganyika kwenye Muungano huu na Zanzibar bila hata kupata baraka za bunge.

Nimemsoma Profesa Issa Shivji na wenzake hapa wakieleza maisha ya Nyerere kwenye vitabu vyao vitatu vile, nimegundua kwamba Nyerere aliiburuza Tanganyika na Tanzania kuliko nilivyofikiri.

Ubaya au uzuri Watanzania wengi hawasomi tu, wangesoma Nyerere angeonekana mtu tofauti sana kulinganisha na Watanzania wengi wanavyomchukulia.

Yani kuna sehemu hata sera zake za Ujamaa zilipoanza kunawiri kwa nguvu za watu bila kupitia TANU Nyerere alipiga marufuku vijiji vya Ujamaa hivyo kwa sababu tu havikuwa chini ya TANU.

Tuliwekwa kwenye bonge la political experiment na mtu mmoja bila hata ridhaa.

Nyerere aliapa kulinda katiba ya Tanganyika, akaishia kuchukua chakula cha watoto wa Tanganyika chote na kuwapa watu wa nchi jirani ya Zanzibar nao wale bure!. Halafu akawaambia watu wa nchi jirani kuwa nyie mnaweza kuchangia chakula chenu kidogo tu ila kilichobaki kuleni nyie peke yenu!!.

Yule mzee hakuwashirikisha wananchi wa Tanganyika katika huu muungano. Waliamka asubuhi na kukuta imeshakuwa fact on the ground!
 
Wazanzibari wana katiba na sheria zao ambazo Katiba ya Tanzania haizigusi wala haina mandate nazo! Iko hivi; mzanzibari ni mtanzania ila sio kila mtanzania ni mzanzibari.
Mzanzibari + Mtanganyika = Mzanzibari
Mtanganyika + Mtanganyika= Mtanzania
 
Back
Top Bottom