PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hii mbona kama inataka kuchafua taswila nzuri ya nchi yetu,au kuna watu wanataka kumuharibia Rais ...siamini haya kama anabariki mh Rais wetu.
Kuna watu mko honest mpaka mnaboa.
Bado unaamini Kuna taswira
Bado unaamini kuna watu wanajali kuhusu wewe

Hii unayoongelea ni nchinya kufikirika
 
Kelele zote za Mdude mitandaoni kumbe anakaa maporini
 
Inaumiza sana yaani mtu anachukuliwa nyumbani kwake kirahisi kabisa anapigwa kwani kama sheria imevunjwa na mtu husika si afikishwe mahakamani kuna ulazima gani wa kuumiza watu kwa namna hii?
Huyu jamaa ana mdomo mchafu sana dhidi ya watu anaowatukana.
Huko uraiani ana mdomo mchafu kuliko humu mitandaoni.
Uje uishi nae jirani halafu uwe hata mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM utajuta. Utatamani kuhamia mbali nae.
Jamaa si wa mchezo mchezo, unaweza ukaua.
 

Yaani police wanavunja mpaka milango. Hii nchi sijui inaelekea wapi...!? Halafu kuna watu wanazungumxia amani ... hivi ni amani gani hiyo? Nchi ina amani lakini raia wake hawana amani....!!
 
Unaweza kunieleza hata sababu moja ambayo inamfanya astahili kupigwa?
Wewe unafikiri wanaompiga hawana akili? Mbona wewe hawakupigi bila sababu, unawwza kunitajia sababu moja inayokufanya usipigwe kama Mdude?
 
Usiku huu, ndugu yetu @mdudenyagali amenyakuliwa na watu waliojitambulisha ni maafisa wa polisi akiwa katika makazi yake Mbeya usiku huu. Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.😑😑😑
 
Usiku huu, ndugu yetu @mdudenyagali amenyakuliwa na watu waliojitambulisha ni maafisa wa polisi akiwa katika makazi yake Mbeya usiku huu. Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.
 
Hii mbona kama inataka kuchafua taswila nzuri ya nchi yetu,au kuna watu wanataka kumuharibia Rais ...siamini haya kama anabariki mh Rais wetu.

Huyo unayedai wanataka kumuharibia yuko kimya. Kila akizungumza anapiga mkwara. Kwa Mzee kibao alikwenda mbali zaidi na kudai kifo ni kifo tu .... ni lazima anahusika.
 
Bado tunajiuliza kina nani walimvamia Padri nanii, Hawa jamaa hawaziwezi tena siasa za ushindani, ndiyo haya yanayotokea. Wako radhi kubaki madarakani kwa nguvu na gharama na yoyote ile.
 
πŸ«’πŸ™„πŸ™„πŸ”Š
 

Inashangaza sana pamoja na matishio yote na historia yake huyu jamaa hakufunga hata camera za siri au za wazi nyumbani kwake? Gps trackers, virecord sauti ambavyo kwa sasa vinapatikana vya kila namna. Angalau kupatikanage hata clue tu inapotokea tukio. Na inasemekana ni mtu wa tech? Bado tuna masikhara sana na maisha yetu wakati nchi ishakua inaenda kwa rule of the jungle! Tuamke wandugu hamna aliye salama, jilinde mwenyewe kabla hujaomba msaada popote ulipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…