Mdude Nyagali: Bil 600 zimekwapuliwa huku makarani wakinyimwa posho na bado zoezi halijakamilika kwa wakati

Mkuu hela ni nyingi huko hazina kumbuka GePG system inawezesha 95% ya malipo ya serikali kuingia hazina. Iwe loss report, passport, leseni na kila kitu ambacho kinahusisha malipo ya serikali. Bado tozo zinaingiza hela nyingi mno wala sio 4OB kwa mwezi kama alivyodanganya bwana yule.
 
Hapa ndio waTanzania tunafeli!! Wala shida sio ya Rais, shida ipo kwa Bunge wao ndio fimbo yetu dhidi ya serikali ila wameshindwa kazi Yao kuwa oversight.

Kipindi Cha Kikwete licha ya ufisadi kuwa mwingi but bunge lilifanya kazi yake kiasi kwamba mawaziri walikua wanalazimishwa kujiuzulu karibu Kila miezi 3!!

Ilipaswa suala kama sensa bunge iundie kamati, ifanye audit, na wahusika wote wawekewe maazimio ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria!!

Tukulaumu Rais itafika 2025 watatupa fisadi mwingine huku bunge likijaa wapiga meza tu!! Business as usual.
 
Tutazidi kulalamika kila siku na kufungua thread kila uchwao pasi kuchukua atua stahiki hakika taifa hili lina kwenda shimoni huu ni wizi wa wazi wazi kabisa na kwa sababu Watanzania hatuna uchungu na pesa za umma acha waibe maana chama kimejaa wezi nani atasimama kumsema mwenzake? Mwisho ina kuwa Kama day dream tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja niendelee kupiga capuchinooo
Huku napanga mipango yangu

Ova
 
Waziri akijiuzulu then nini kinabadilika?
 
Wakati mporipori anamkataa huyu mtu,chama kikamkazia akaona anyway sio ishu,kumbe alijua siku moja itabidi amuachie kijiti😁😁😁
Kama nchi tuzame kwenye maombi.
 
Mzunguko wa pesa ukikosekana mtaani mnaanza kulalamika
Hawa watu ni kulalamika kila kitu.Hizo pesa,zitakuwa kwenye mzunguko hapa hapa Tanzania,na zitamfikia mpaka huyo anayelalamika,bora asiwe mvivu wa kufanyakazi,biashara,kuajiriwa,kujiajiri nk.
Fursa za kazi zipo nyingi sana,kwa mfano sehemu kunavuliwa samaki wa biashara,kuna vijana, wazee,wanawake,wanatengeneza pesa,wao wanakuwa ni madalali,baina ya mvuvi na mnunuzi wa jumla na rejareja,na wanapata kipato kizuri tu.Kwa mfano mvuvi anauza kilo 5000,dalali anamuuzia mwingine 7000,ni kutokana na huyu mnunuzi kushindwa kufuatilia samaki ndani ya maji,kuliko chombo cha uvuvi.Je akiuza kila 20 kwa siku,amepata karibia 40,000.
 
Usitegemee watakuwa na uchungu na pesa za umma wakati AKILI NA nguvu zinawaza SIMBA NA YANGA,NA KUBET
 
Sikubaliani na shutuma anazotoa huyu mwehu mdude kwa serikali. Mdude ni mtu ambaye hana akili. Ila nakurekebisha sehemu moja

Kuna kitu mnachanganya sana, uchumi wa nchi hauendeshwi na pesa zinazoibwa. Utofauti wetu na wenzetu walioendelea ndio upo hapo, wao wameweza kudhibiti pesa inayoibwa.

Moja ya kazi nzito aliyonayo mama Samia ni kupunguza na kuzuia pesa kuibiwa na anafanya vizuri eneo hilo. Hii ya kusema pesa inayoibwa sijui ndio inaingia mtaani ni mtu mjinga pekee anayeweza kufikiria kitu Kama hicho.

Bil 600 kuingia kwake mtaani sio kupitia sensa tu au kuibiwa, Bali inaweza kuingia mtaani kupitia uzalishaji na hapo ndio uchumi wa nchi na uchumi wa mmoja mmoja huwa mkubwa.
 
Sasa hivi utasikia mtoto akilia “siyo mimi, siyo mimi, siyo mimi ni tangia Magufuli ziliibiwa“!
 
Mzunguko wa pesa ukikosekana mtaani mnaanza kulalamika
Hoja ya mdude ni mufilisi, Ila pia mzunguko wa peda hautokani na pesa kupigwa bali unatokana na uzalishaji. Hata raisi mwenyewe hawezi kukubali kuona pesa inaibiwa.

Akili Kama zako ndio zinapatikana huku shithole countries tu, mnaamini mzunguko wa pesa mtaani unatokana na pesa kuibwa badala ya uzalishaji
 
Tatizo la nchi yetu ni ubovu wa mifumo ya utendaji kazi. Lakini kwanini rais analaumiwa? Ni kwa sababu kwa nchi zetu hizi za "shithole" rais ana nguvu kubwa ya ku influence na ku override mambo.
Hatujawahi kuwa na rais mwenye dhamira ya dhati ya kubadilisha mfumo mbovu wa nchi hii kuanzia kwenye utendaji mpaka uwajibikaji. Hakuna! Si Kikwete, si Magufuli, si huyu mzenji, si Mkapa. Hakuna!
Ni watawala wanaoongoza kana kwamba wameazimwa au kulazimishwa.
 
Jamaa kanichekesha yaani yeye kwake mzunguko wa pesa unatokana na pesa za umma kukwapuliwa. Haha ipo mambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…