Mdude Nyagali: Bil 600 zimekwapuliwa huku makarani wakinyimwa posho na bado zoezi halijakamilika kwa wakati

Mwaka 2010 China ilifanya Sensa na kutumia Yuan Milion 700, sawa na shilingi za kitanzania bilion 236 kwa exchange rate ya leo.
Lakini kinchi kidogo kama Tanzania ambacho ni kama jimbo moja tu la china kinafanya sensa kwa shilingi bilioni 629

Hapa kuna harufu ya wizi!
Mkuu hela ni nyingi huko hazina kumbuka GePG system inawezesha 95% ya malipo ya serikali kuingia hazina. Iwe loss report, passport, leseni na kila kitu ambacho kinahusisha malipo ya serikali. Bado tozo zinaingiza hela nyingi mno wala sio 4OB kwa mwezi kama alivyodanganya bwana yule.
 
Sasa ni dhahiri huko serikalini kila mmoja anakula kwa urefu wa kamba yake, sijui kwanini Rais hakuwahi kuitolea ufafanuzi ile kauli.

Kwa wale mnaopenda kumlaumu Mdude "anatukana", naona hapo katumia neno vibaka, na kila anayekwapua jina lake ni either mwizi, au kibaka, hapo msimlaumu.

Hii nchi tuseme ukweli imemshinda Samia, matokeo ya kauli zake anazotoa bila kuzichuja naona ndio yametufikisha hapa.

Tuhuma za aina hii zinazidi kuongezeka kila siku, huku Mwigulu na tozo, pale sensa, kule Makamba na $30 million za maintanance, hawa anaowaita wanangu naona sasa wanamuibia mama yao.

Haya yasipochukuliwa hatua mapema ndio yanazidi kuongezeka, inaonekana na wengine nao wanaona kama yule alichota pale hakufanywa kitu, ngoja nami nichote hapa.

Matokeo yake Samia anapozidi kuchelewa ku-react anajikuta anashindwa kuwaadhibu kwa kuogopa kuonekana anawaonea wengine, na serikali yake ndio itazidi kuchafuka na kupoteza imani kwa watanzania, naona sasa tunarudi kule kwa JK.
Hapa ndio waTanzania tunafeli!! Wala shida sio ya Rais, shida ipo kwa Bunge wao ndio fimbo yetu dhidi ya serikali ila wameshindwa kazi Yao kuwa oversight.

Kipindi Cha Kikwete licha ya ufisadi kuwa mwingi but bunge lilifanya kazi yake kiasi kwamba mawaziri walikua wanalazimishwa kujiuzulu karibu Kila miezi 3!!

Ilipaswa suala kama sensa bunge iundie kamati, ifanye audit, na wahusika wote wawekewe maazimio ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria!!

Tukulaumu Rais itafika 2025 watatupa fisadi mwingine huku bunge likijaa wapiga meza tu!! Business as usual.
 
Tutazidi kulalamika kila siku na kufungua thread kila uchwao pasi kuchukua atua stahiki hakika taifa hili lina kwenda shimoni huu ni wizi wa wazi wazi kabisa na kwa sababu Watanzania hatuna uchungu na pesa za umma acha waibe maana chama kimejaa wezi nani atasimama kumsema mwenzake? Mwisho ina kuwa Kama day dream tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja niendelee kupiga capuchinooo
Huku napanga mipango yangu

Ova
20220830_100649.jpg
 
Hapa ndio waTanzania tunafeli!! Wala shida sio ya Rais, shida ipo kwa Bunge wao ndio fimbo yetu dhidi ya serikali ila wameshindwa kazi Yao kuwa oversight.

Kipindi Cha Kikwete licha ya ufisadi kuwa mwingi but bunge lilifanya kazi yake kiasi kwamba mawaziri walikua wanalazimishwa kujiuzulu karibu Kila miezi 3!!

Ilipaswa suala kama sensa bunge iundie kamati, ifanye audit, na wahusika wote wawekewe maazimio ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria!!

Tukulaumu Rais itafika 2025 watatupa fisadi mwingine huku bunge likijaa wapiga meza tu!! Business as usual.
Waziri akijiuzulu then nini kinabadilika?
 
Wakati mporipori anamkataa huyu mtu,chama kikamkazia akaona anyway sio ishu,kumbe alijua siku moja itabidi amuachie kijiti😁😁😁
Kama nchi tuzame kwenye maombi.
 
Mzunguko wa pesa ukikosekana mtaani mnaanza kulalamika
Hawa watu ni kulalamika kila kitu.Hizo pesa,zitakuwa kwenye mzunguko hapa hapa Tanzania,na zitamfikia mpaka huyo anayelalamika,bora asiwe mvivu wa kufanyakazi,biashara,kuajiriwa,kujiajiri nk.
Fursa za kazi zipo nyingi sana,kwa mfano sehemu kunavuliwa samaki wa biashara,kuna vijana, wazee,wanawake,wanatengeneza pesa,wao wanakuwa ni madalali,baina ya mvuvi na mnunuzi wa jumla na rejareja,na wanapata kipato kizuri tu.Kwa mfano mvuvi anauza kilo 5000,dalali anamuuzia mwingine 7000,ni kutokana na huyu mnunuzi kushindwa kufuatilia samaki ndani ya maji,kuliko chombo cha uvuvi.Je akiuza kila 20 kwa siku,amepata karibia 40,000.
 
Tutazidi kulalamika kila siku na kufungua thread kila uchwao pasi kuchukua atua stahiki hakika taifa hili lina kwenda shimoni huu ni wizi wa wazi wazi kabisa na kwa sababu Watanzania hatuna uchungu na pesa za umma acha waibe maana chama kimejaa wezi nani atasimama kumsema mwenzake? Mwisho ina kuwa Kama day dream tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Usitegemee watakuwa na uchungu na pesa za umma wakati AKILI NA nguvu zinawaza SIMBA NA YANGA,NA KUBET
 
Hawa watu ni kulalamika kila kitu.Hizo pesa,zitakuwa kwenye mzunguko hapa hapa Tanzania,na zitamfikia mpaka huyo anayelalamika,bora asiwe mvivu wa kufanyakazi,biashara,kuajiriwa,kujiajiri nk.
Fursa za kazi zipo nyingi sana,kwa mfano sehemu kunavuliwa samaki wa biashara,kuna vijana, wazee,wanawake,wanatengeneza pesa,wao wanakuwa ni madalali,baina ya mvuvi na mnunuzi wa jumla na rejareja,na wanapata kipato kizuri tu.Kwa mfano mvuvi anauza kilo 5000,dalali anamuuzia mwingine 7000,ni kutokana na huyu mnunuzi kushindwa kufuatilia samaki ndani ya maji,kuliko chombo cha uvuvi.Je akiuza kila 20 kwa siku,amepata karibia 40,000.
Sikubaliani na shutuma anazotoa huyu mwehu mdude kwa serikali. Mdude ni mtu ambaye hana akili. Ila nakurekebisha sehemu moja

Kuna kitu mnachanganya sana, uchumi wa nchi hauendeshwi na pesa zinazoibwa. Utofauti wetu na wenzetu walioendelea ndio upo hapo, wao wameweza kudhibiti pesa inayoibwa.

Moja ya kazi nzito aliyonayo mama Samia ni kupunguza na kuzuia pesa kuibiwa na anafanya vizuri eneo hilo. Hii ya kusema pesa inayoibwa sijui ndio inaingia mtaani ni mtu mjinga pekee anayeweza kufikiria kitu Kama hicho.

Bil 600 kuingia kwake mtaani sio kupitia sensa tu au kuibiwa, Bali inaweza kuingia mtaani kupitia uzalishaji na hapo ndio uchumi wa nchi na uchumi wa mmoja mmoja huwa mkubwa.
 
Sasa hivi utasikia mtoto akilia “siyo mimi, siyo mimi, siyo mimi ni tangia Magufuli ziliibiwa“!
 
Mzunguko wa pesa ukikosekana mtaani mnaanza kulalamika
Hoja ya mdude ni mufilisi, Ila pia mzunguko wa peda hautokani na pesa kupigwa bali unatokana na uzalishaji. Hata raisi mwenyewe hawezi kukubali kuona pesa inaibiwa.

Akili Kama zako ndio zinapatikana huku shithole countries tu, mnaamini mzunguko wa pesa mtaani unatokana na pesa kuibwa badala ya uzalishaji
 
Hapa ndio waTanzania tunafeli!! Wala shida sio ya Rais, shida ipo kwa Bunge wao ndio fimbo yetu dhidi ya serikali ila wameshindwa kazi Yao kuwa oversight.

Kipindi Cha Kikwete licha ya ufisadi kuwa mwingi but bunge lilifanya kazi yake kiasi kwamba mawaziri walikua wanalazimishwa kujiuzulu karibu Kila miezi 3!!

Ilipaswa suala kama sensa bunge iundie kamati, ifanye audit, na wahusika wote wawekewe maazimio ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria!!

Tukulaumu Rais itafika 2025 watatupa fisadi mwingine huku bunge likijaa wapiga meza tu!! Business as usual.
Tatizo la nchi yetu ni ubovu wa mifumo ya utendaji kazi. Lakini kwanini rais analaumiwa? Ni kwa sababu kwa nchi zetu hizi za "shithole" rais ana nguvu kubwa ya ku influence na ku override mambo.
Hatujawahi kuwa na rais mwenye dhamira ya dhati ya kubadilisha mfumo mbovu wa nchi hii kuanzia kwenye utendaji mpaka uwajibikaji. Hakuna! Si Kikwete, si Magufuli, si huyu mzenji, si Mkapa. Hakuna!
Ni watawala wanaoongoza kana kwamba wameazimwa au kulazimishwa.
 
Hoja ya mdude ni mufilisi, Ila pia mzunguko wa peda hautokani na pesa kupigwa bali unatokana na uzalishaji. Hata raisi mwenyewe hawezi kukubali kuona pesa inaibiwa.

Akili Kama zako ndio zinapatikana huku shithole countries tu, mnaamini mzunguko wa pesa mtaani unatokana na pesa kuibwa badala ya uzalishaji
Jamaa kanichekesha yaani yeye kwake mzunguko wa pesa unatokana na pesa za umma kukwapuliwa. Haha ipo mambo!
 
Back
Top Bottom