Unashangaza, unakiri bunge limeshindwa kufanya kazi yake halafu hautaki Rais alaumiwe, sasa unataka tufanyeje?! au tuzubae tu hapo!.
Kwanini Rais analaumiwa?
1. Yeye ndie huwaweka sehemu kubwa ya hao watendaji wanaoharibu, hivyo anaweza pia kuwaondoa kisheria.
2. Rais ni sehemu ya bunge, hivyo ana uwezo wa kuinfluence anachotaka kikafanywe na bunge lakini hafanyi hivyo, hii nayo ipo kisheria.
3. Rais ana uwezo wa kulivunja bunge lisipofanya vile anataka, hii maana yake Rais yupo juu ya bunge.
Kaisome Katiba ya JMT uone mamlaka ya kimalkia aliyopewa Samia na Katiba ya 1977.
Hii tabia yenu ya kumkwepesha Rais na majukumu yake nawaona wengi wenu mna lengo la kumfichia udhaifu wake tu, nothing else.