Mdude Nyagali kupatikana tena ni 5%. Poleni sana Watanzania

Mdude Nyagali kupatikana tena ni 5%. Poleni sana Watanzania

Uharakati wa Bongo ni sawa na kuchungulia kaburi.

Nitumie nafasi hii kutoa pole kwa Wanaharakati wote. Pole kwa Marafiki zake Mwabukusi na Dr. Slaa na Wanachama wote wa JamiiForums wasiokubaliana na Sela za CCM. Matamanio ya kila Mtu ilikuwa kumuona Mdude_Nyagali akishuhudia CCM ikiondolewa Madaraka. Tumemtafuta kila sehemu. Hadi nimekata tamaa, moyo wangu umekua mweusi, Macho mekundu, mdomo umenikauka na njaa hainiumi. Mwili wangu umekufa ganzi.

Mdude aliamua kufa amesimama kuliko kuishi amepiga Magoti.

Kaacha kitabu ambacho kataja changamoto anazokutana nazo kwenye harakati zake.

Hata hivyo hata hao Polisi hawataishi milele.

Kitu mtu unatakiwa umfanyie mtu ni UPENDO. Unamuua Mtu leo kesho nawe unakufa.

Inauma sana Vijana wa Nchi wanaothubutu kuona wanateketea.

Yote yana Mwisho. Mbele yetu Nyuma yake.

A luta continua, vitória é certa'.
View attachment 3322862
Maneno ya Mwisho ya Mdude CHADEMA.
View attachment 3322864
View attachment 3322865
Mdude kaacha alama.

Uongozi unafaida kama Machozi yanawatoka Wananchi wako na Karo lako la Maji machafu limejaa damu mbichi za watu Unaowaongoza?

Baadhi ya Thread za Mdude ambazo sichoki kuzisoma;

1. Barua ya wazi kwa ndugu, jamaa na watanzania kwa ujumla baada ya kupata vitisho vya kuniteka, kuniuwa na kunipoteza

2. Kidnapping Chain

3. Ni kweli Watekaji hawajulikani?
Inasikitisha Sana.
 
Hivi mtu akikutukana kama sio ujinga unapungukiwa nini? Sasa methali ya ukubwa ni jalala mtu utaitumia wapi? Ukishakua Rais unakuwa rais wa Wote. Vichaa na Wasio vicha. Wasomi na Wasio wasomi. Washamba na wajanja.

Mjinga tu ndo atabagua.
Nashauri wana JF tuachane na siasa za matusi, bora kuangalia challenge ya wimbo wa "KUNA" Tiktok
 
Ni kweli. Sidhani kama atapatikana tena hai. Tunachoweza kufanya ni kuchunguza kwa undani na kujua walau watu walio nyuma ya huu unyama. Mkuu wa polisi wa mkoa anahusika na anajua kila kitu.
Tatizo wanaopaswa kuchunguza ni watuhumiwa namba moja.
 
Hawezi kuuliwa na yoyote, alichotafuta amekipata.
Unapokuwa third world country na kuendeleza siasa chafu kwa watawala lolote laweza kutokea
Wajaribu mahabusu huko hawatamkosa.
 
Dah huyu mwamba kama mpaka sasa haonekani inaogopesha sana
 
Back
Top Bottom